Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,445
- 7,816
Televisheni ya Taifa imekata matangazo ya Bunge la Bajeti na sasa wanarusha kongamano la viongozi wa dini kumuombea na kumpongeza Rais Samia kwa uongozi bora linalofanyika ukumbi wa mikutano wa Tughimbe mkoani Mbeya. Wapo viongozi wa dini, Serikali na waimbaji kutoka kona mbalimbali za nchi hiii. Pia TBC imepeleka timu yake kulirusha tukio husika live kutoka Mbeya.
Siku za karibuni hizi vitu zimeongezeka sana na haya ni yale machache yanayoonekana, makongamano haya achilia mbali posho tena na vile zitapanda, yatazidi kuongezeka.
Pia gharama za kukodi kumbi, kuziandaa, kutengeneza mabango, machapisho na gharama za kuyaleta magari ya viongozi wa Kiserikali kutoka mikoani huwa gharama hasa ukijumuisha na wahusika kujiwekea asilimia zao kwenye bei.
Serikali ikumbuke kuweka fedha nyingi zaidi kwenye bajeti ya maendeleo kuliko matumizi ya kila siku.
Viongozi wenyewe wa dini hawajaja na akili huru, wote wamekuja kuimba mapambio ya watawala.