Makonda: Walimu kusafiri bure


Polisi bure, wanajeshi bure, wanafunzi nusu nauli..... sasa waalimu nao bure, kisha itakuja manesi wauguzi na madaktari nao watataka kusafiri bure. Makonda ana mamlaka hayo ya kuamua jambo kubwa kama hili. Je hili si sula la SUMATRA na serikali?
 
Wanajeshi, Polisi na Askari Magereza wanasafiri bure. Sasa inapendekezwa Walimu nao wasafiri bure. Baadaye kidogo itapendekezwa Madaktari na Wauguzi nao wasafiri bure. Hautapita muda mrefu kila mtu atakuwa na kitambulisho cha Mwl au Daktari/Muuguzi.

Nani atalipa nauli kwenye daladala?
 
Labda wawape transport allowance itasaidia kuliko kusema wasafir bure mm kama mmiliki wa gari hilo siwezi kulikubali kwa sababu nalipa mapato makubwa tra sio kwaajir ya kutoa huduma bure bali kufanya biashara.
 
Sijui kama anajua kinachoendelea! Wamiliki wa daladala wako ktk utaratibu wa kuhakikisha polisi na wanajeshi wanalipa nauli kwani kwa miaka nenda rudi walikuwa hawalipi! Pia wanafunzi walipe nusu ya nauli ya mtu mzima kama sharia inavyosema! sasa huyu anakuja na suala la walimu nao iwe bure! Sidhani kama anajua kinachoendelea hapa jijini!
 
huyu mkuu wa wilaya ni bure kabisa
 
Mkuu wa wilaya ya.kinondoni amesema yupo kwenye mpango wa kuwezesha walimu kusafiri bure kwenye daladala kwenda kazini kama njia ya kuwasaidia kuwahi na kuwapunguzia makali ya maisha.

Makonda ameyasema hayo wakati wa hafla ya kumuaga mke wa raisi mwl Janet Magufuli ambaye amekiri kuwa kwa sasa anamajukumu mengi hasa yakumsaidia mheshimiwa raisi.

Sasa hapa najiuliza hawa wamiliki wa magari watakubali? Na je walimu watakuwa na unifomu.au watalazimika kila wakati kuonesha vitambulisho? Na je hilo litakuwa suluhisho la kudumu? Na je watumishi wengine wao watajisikiaje ? Source Azam tv- habari ya saa 2 usiku.

Yupo kwenye mchakato amekuambia, maswali yote ya nini? Kwani askari na jeshi waliporuhusiwa we ulijisikiaje??
 
Kinachotakiwa Ni kupiga hesabu ya gharama wanazotumia walimu kama nauli then hiyo Pesa walipwe kila mwezi.Hili la bure litaleta shida sana kwa wamiliki wa magari kwa sababu walimu hawana uniform ambazo zinaogopeka na RAIA wengine kiasi kwamba kuna watu watatumia hiyo gap kujifanya nao Ni walimu na wakawa wanasafiri bure..
 
Walipeni Waalimu Mishahara Mizuri itakayowawezesha kumudu gharama za Maisha.


Ugumu wa Maisha sio ktk Kusafiri tu.


Makonda hapo umetoa pumba





===========================


KIPIMO CHA MAGUFULI
CHAWAGONGANISHA
WAZIRI, DC TEMEKE



Siku mbili baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema Wilaya ya Temeke inaongoza mkoani Dar es Salaam kwa kuwa na wagonjwa sita wa kipindupindu,

Mkuu wa wilaya hiyo (DC), Sophia Mjema amesema hadi jana
hakukuwa na mgonjwa hata mmoja.
 
Hii hoja ya bure kila kitu kwa wamiliki wa daladala siliungi mkono ingawa nakubali kimsingi kwamba walimu wanatakiwa kuangaliwa kwa jicho la tatu kimaslahi
 


Ningemuona ana akili kama angeishauri serikali kuwaongezea walimu transport allowance
 
Mimi naona ni Good idea, Kama mwanajeahi au askari anasafiri bure.. Kwa nini mwalimu asidafiri bure na yeye? Wawe na vitambulisho tu... Mwalimu ni mtu muhimu sana ...
sasa ikitokea kua gari Zima wamepanda walimu maana watakua hawana uniform itakuaje?
 
Hitaji la walimu ni nyogeza ya mishahara na teaching allowance Hera za rikizo,kupanda madaraja,na makazi kwa maana ya nyumba nani kamwambia makonda kua hitaji la walimu ni kulipiwa nauli za daladala? Amekaa nao wakamwambia hivo? Badala wapunguze kodi kwenye mishahara yetu anasema nauli za daladala?shitiii
 
Yaani hapo sipati picha konda anataka nauli yake alafu unamwambia we mwalimu, anaanza kugomba sasa kwa sauti kubwa watu wote wanakugeukia wewe, utatamani uwe sisimizi
na hapo tukifuata haki , yule aliyetoa hela ambaye ni mwanafunzi ni lazima akae kwenye kiti na huyo mpenda vya bure ambaye ni mwalimu asimame .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…