Makonda: Marufuku kudai nyongeza ya mshahara! Nashangaa watu wanapita na mabango, mie ningewachapa

Na support Kauli yake.
Ipo sahihi kabisa.. usiitafsiri moja kwa moja.. hapo anachomaanisha ni kuwalenga watumishi ambao hawatimizi majukumu yao.

Kama hujawahi kukutana na hawa watumishi hasa hasa kwenye halmashauri zao basi usiombe ukutane na hawa Miungu watu kwenye hizi halmashauri. Ukiwa na shida.. utakoma kuringa
Ikiwa Mtumishi anakwamisha au anazungusha
Kwa nni usionane na Mkuu wake au Mkurugenzi wa hiyo Halmashauri

Watanzania mpaka lini mtaendelea kulalamika tuuu?
 
Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dsm wanapitia kipindi kigumu sana.

Bashite hajui May Mosi ni siku ya kuzungumzia Masuala ya Wafanyakazi sio Wateja wa Wafanyakazi
Arrogance imeshamuingia ........ Ana bahati Watanzania ni kama Mbwa koko wa katuni ya Kipanya.

Hivi ingekuwa nchi kama RSA, Bashite angeweza kuongea hivyo mbele ya maafisa wa serikali. Tena wengine wanaonekana wamemzidi sana Kiumri ...... eti ningewapiga viboko!! Seriously!? Hii ni dharau ya hali ya juu.

Tatizo Watanzania wengi hajui haki zetu ... ndiyo maana hatuwezi kuzidai!!
 
yaani mtu kudai nyongeza ya mshahara ndio achapwe
tz hii nchi imekosa nini lakini
viongozi tunaenda kuwa nao ndio type hii kweli?
 
Bila mijeledi reli ya kati isingekuwepo ni njia pekee ambayo inaeleweka.
 
Mbona wale wakurugenzi wanaoambiwa wasihamishe wafanyakazi bila kuwapa stahiki zao wao hawajachapwa viboko hao wanao omba haki yao ndo wachapwe viboko,yaani anaenyima mtu haki yake na pia kukaidi agizo la Rais hajachapwa anaeomba na ni haki yake achapwe!!?
 
KATI YA MAMBO NINAYOYAFURAHIA NI WATUMISHI WA SERIKALI KUCHELEWESHEWA MISHAHARA/KUNYIMWA NYONGEZA YA MISHAHAYA AU KUTOPEWA KABISA MISHAHARA. you know why (wana nyodo makazini mwao)
 
Makonda mzalendo sana, nahisi kuna siku atapunguza mshahara wake awe sawa na walimu,na manesi na aachane na kutembelea magar mazur ili awe sawa na wananchi anaowaongoza ili wasje sema hajui anachokiongea ,,,makonda ni mzalendo sana na ni mchapa kazi kwel kwel !!
 
inauma bana! mtu anamka tandale kwa tumbo saa 11 anakabwa anachaniwa nguo, bado anakomaa anafka job kumsaidia mtanzania mwenzake wa hal ya chn! akiomba nyongeza walau atoke akapange hata kinondon imekuwa shda! huyu chocochannel dawa yake mungu anaichemsha! akiipua ataisoma namba
Take my words the innocent dies very easily but the evil lives again and again....
 
Makonda mzalendo sana,naisi kuna siku atapunguza mshahara wake awe sawa na walimu,na manesi na aachane na kutembelea magar mazur ili awe sawa na wananchi anaowaongoza ili wasje sema hajui anachokiongea ,,,makonda ni mzalendo sana na ni mchapa kazi kwel kwel !!
Mali alizojikusanyia toka kwa waarabu muda mfupi akiwa madarakani unamuita mzalendo?Nyerere angeshamtimua huyu kwa kupokea vijizawadi
 
Back
Top Bottom