satininus
Senior Member
- Feb 11, 2021
- 135
- 171
Baada ya kukaa miaka karibia sita bila kuwa ya wafanyakazi wa umma kupewa nyongeza ya mshahara na increments katika awamu ya tano,wafanyakazi walikata tamaa kabisa ya maisha Bora na kujiingiza katika madeni makubwa ambayo yanawatesa hadi sasa.
Kuingia kwa awamu ya sita wafanyakazi walipata matumaini makubwa sana kwa rais ambaye waliamini kuwa atawapa ahueni katika maslahi yao ambayo kimsingi ni haki yao.Mei mosi ya mwaka 2021 wafanyakazi waliahidiwa kumpa muda rais ambaye ndio kwanza alikuwa na miezi miwili tu tangu aingie madarakani, wafanyakazi kwa ujumla wao walimwelewa sana Mama na kumshukuru kwa kuwapa japo kali za matumaini kinyume mtangulizi wake.
Mwaka 2022 ni mwaka ambao wafanyakazi wote wa watanzania walikuwa na matumaini makubwa sana kwa serikali yao na wakaahidiwa ongezeko la mshahara ambalo lingepunguza sana machungu ya maisha. Lakini kilichotokea kila mtu anajua, hivyo mei mosi ya mwaka huu 2023 hakuna mfanyakazi mwenye matumaini yeyote yale na huenda wengi wao hawajui hata mahali itakayofanyika mwaka huu.
Nategemea serikali itafanya juu chini kurudisha matumaini kwa wafanyakazi ili kuongeza utendaji kazi ma ufanisi kazini ili kuleta tija nchini.Kazi iendelee.