Huyu kijana mwenzetu kabebewa mbeleko la aina yake. Makosa anayoyafanya hadharani bila kukemewa, kuonywa na kuadabishwa Kama wanavyofanyiwa viongozi wengine kwake ni ndoto kwenye awamu hii hii inayosifiwa kwa kutenda haki. Makonda amefanya mengi ya kuudhi na kuvunja sheria.
Ni Makonda aliyevamia clouds, ni Makonda aliyetukana bunge, ni Makonda aliyetuhumu watu hadharani kwa dawa za kulevya na kuharibia watu haiba zao, ni Makonda anayebaguwa wachaga.
Hata hivyo ni muda mrefu watu wamesema hakuna hatua yoyote anayochukuliwa zaidi ya kupongezwa na kukingiwa kifua. Makonda huyu habadiliki na anarudia makosa Yale Yale.
Sasa anasemwa hadharani na katibu mkuu wake wa chama, na makanisani. Anasemwa na Kila kundi la jamii. Si wapinzani, si chama tawala, si maaskofu, si wanahabari, si wanajamii peke yao lkn anasemwa na Kila kundi.
Hilo taulo la kumbeba Makonda limechoka, limetoboka. Sasa ni wakati kumbadilishia mbeleko. Wakati ni Sasa kabla hajaendelea kulitia hasara taifa.