Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,869
Tutofautishe nyakati
Tutofautishe nguvu
Tutofautishe ubabe
Tutofautishe uthubutu
Tutofautishe nafasi za kimamlaka serikalini na kwenye chama cha siasa
Ukatibu mwenezi wa chama ni tofauti kabisa na u DC ama u RC.. Ukiwa DC wewe ndio rais wa wilaya.. Yaani kiwilaya hakuna mamlaka mengine ya juu zaidi
Ukiwa RC wewe ndio rais wa mkoa hakuna nafasi ya juu zaidi kimkoa kuzidi hiyo.. Vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko chini yako na una amri ya kimamlaka juu yao
Ukiwa katibu mwenezi wa chama huna madaraka ya kimamlaka na cycle ya watu inayowajibika kwako ni ndogo sana.. Na huna say ya mwisho kwenye lolote.. Ni lazima upokee maagizo kutoka juu
Kwenye hiyo nafasi ya kichama hakuna kamati ya usalama yenye kukusikiliza wewe ..na huna uwezo wa kusweka watu ndani utakavyo!
Makonda alipaishwa kipindi cha mkono wa chuma usioogopa kitu naye akapaa na kuenea vema.. Maguvu na ubabe bila staha kwa mkubwa wala mdogo ndio vilikuwa hobby yake! Alijisikia furaha sana,kudhalilisha yeyote kutokana na madaraka ya kimamlaka aliyokuwa nayo
Sasa hizi ni nyakati tofauti sana na zile.. Na nafasi aliyonayo haina nguvu ya kuamrisha kama zile nyingine... Na kibaya zaidi ndani ya chama kuna mipasuko kama ardhi ya kiangazi.. Huko hakuna ubabe na kuamrisha.. Na kuteuliwa kwake kumezidisha mipasuko.. Kwahiyo ni mwendo wa mitifuano nyuma ya zulia na mitafutano...
Mpaka hapo keshapwaya pakubwa.. Badala ya kung'ara na kuwika anaweza kufunikwa na wanazi wa chama asisikike wala asifurukute kabisa.. Kwakuwa hata ndani ya chama ana maadui wa kutosha sana!
Kitakachomuokoa labda awe kawekwa hapo kwa muda ili kusoma upepo kabla hajapewa nafasi inayoendana na kaliba yake ya kupayuka, kudhalilisha na kutumia maguvu hata panapohitaji diplomasia
Akiachwa hapo atakonda mpaka atapepesuka mwisho tukamuokote Makondeko
Sent using Jamii Forums mobile app