Makonda asipokonda basi ataishia Makondeko

Makonda asipokonda basi ataishia Makondeko

Tutofautishe nyakati
Tutofautishe nguvu
Tutofautishe ubabe
Tutofautishe uthubutu
Tutofautishe nafasi za kimamlaka serikalini na kwenye chama cha siasa

Ukatibu mwenezi wa chama ni tofauti kabisa na u DC ama u RC.. Ukiwa DC wewe ndio rais wa wilaya.. Yaani kiwilaya hakuna mamlaka mengine ya juu zaidi
Ukiwa RC wewe ndio rais wa mkoa hakuna nafasi ya juu zaidi kimkoa kuzidi hiyo.. Vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko chini yako na una amri ya kimamlaka juu yao
Ukiwa katibu mwenezi wa chama huna madaraka ya kimamlaka na cycle ya watu inayowajibika kwako ni ndogo sana.. Na huna say ya mwisho kwenye lolote.. Ni lazima upokee maagizo kutoka juu
Kwenye hiyo nafasi ya kichama hakuna kamati ya usalama yenye kukusikiliza wewe ..na huna uwezo wa kusweka watu ndani utakavyo!

Makonda alipaishwa kipindi cha mkono wa chuma usioogopa kitu naye akapaa na kuenea vema.. Maguvu na ubabe bila staha kwa mkubwa wala mdogo ndio vilikuwa hobby yake! Alijisikia furaha sana,kudhalilisha yeyote kutokana na madaraka ya kimamlaka aliyokuwa nayo

Sasa hizi ni nyakati tofauti sana na zile.. Na nafasi aliyonayo haina nguvu ya kuamrisha kama zile nyingine... Na kibaya zaidi ndani ya chama kuna mipasuko kama ardhi ya kiangazi.. Huko hakuna ubabe na kuamrisha.. Na kuteuliwa kwake kumezidisha mipasuko.. Kwahiyo ni mwendo wa mitifuano nyuma ya zulia na mitafutano...

Mpaka hapo keshapwaya pakubwa.. Badala ya kung'ara na kuwika anaweza kufunikwa na wanazi wa chama asisikike wala asifurukute kabisa.. Kwakuwa hata ndani ya chama ana maadui wa kutosha sana!

Kitakachomuokoa labda awe kawekwa hapo kwa muda ili kusoma upepo kabla hajapewa nafasi inayoendana na kaliba yake ya kupayuka, kudhalilisha na kutumia maguvu hata panapohitaji diplomasia

Akiachwa hapo atakonda mpaka atapepesuka mwisho tukamuokote MakondekoView attachment 2793723

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza kaendesha pikipiki bila helmet leo, SHERIA ifuate mkondo wake
 
Kabla hatujakutetea tunajiuliza baadhi ya maswali.

1, Wewe hukuuwa Watu?
2, wewe hukutesa watu?
3, Wewe hukubambikizia watu kesi za uhujumu uchumi?
4, wewe hukubambikizia watu (Gwajima na Mbowe) kesi za madawa ya kulevya?
5, wewe hukutukana Watu/ watumishi hadharani?
6, Wewe hukuhusika na kupoteza watu Ben sanane, Azori Gwanda?
7, Baba keagen hukuhusika na kushambuliwa kwa watanzania wenzako Mzee warioba na Mhe Tundu Lissu?
8, Baba keagen hukujimilikisha mali za watu (GSM)!kimabavu?
9, Baba keagen hukutuambia Kati ya watu wanaokula raha duniani na wewe ni mmoja wapo?
10, Baba keagen hukuhusika na tukio la kuvamia ofisi za Clouds media mchana kweupe?
11, Baba keagen hukuhusika na tukio la Nape kutolewa bastora hadharani?

BASHITE Damu ni nzito kuliko maji kwahiyo jihukumu kabla Mungu hajakuhukumu kwani hili lazima lifanikiwe kwa heshima ya Taifa.
FB_IMG_1698409929105.jpg
FB_IMG_1698409923439.jpg
FB_IMG_1698409904347.jpg
FB_IMG_1698409926458.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla hatujakutetea tunajiuliza baadhi ya maswali.

1, Wewe hukuuwa Watu?
2, wewe hukutesa watu?
3, Wewe hukubambikizia watu kesi za uhujumu uchumi?
4, wewe hukubambikizia watu (Gwajima na Mbowe) kesi za madawa ya kulevya?
5, wewe hukutukana Watu/ watumishi hadharani?
6, Wewe hukuhusika na kupoteza watu Ben sanane, Azori Gwanda?
7, Baba keagen hukuhusika na kushambuliwa kwa watanzania wenzako Mzee warioba na Mhe Tundu Lissu?
8, Baba keagen hukujimilikisha mali za watu (GSM)!kimabavu?
9, Baba keagen hukutuambia Kati ya watu wanaokula raha duniani na wewe ni mmoja wapo?
10, Baba keagen hukuhusika na tukio la kuvamia ofisi za Clouds media mchana kweupe?
11, Baba keagen hukuhusika na tukio la Nape kutolewa bastora hadharani?

BASHITE Damu ni nzito kuliko maji kwahiyo jihukumu kabla Mungu hajakuhukumu kwani hili lazima lifanikiwe kwa heshima ya Taifa.View attachment 2794692View attachment 2794693View attachment 2794694View attachment 2794695

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii sasa balaa..
 
Mimi Binafsi nahisi Kuna jambo Mungu anakuja kutufindisha Watanzania maana hili swala la Makonda linaenda kuleta habari njema na habari mbaya kwa pande hasimu ndani ya Chama na nje ya Chama, CCM oyeeeee
 
Hata wewe mshana Jr kumbe ni kanya boya?!,kwa taarifa yako kiongozi wa chama ni mkubwa kuliko kiongozi wa serikali.hapo juu wapo wanne tu,mwenyekiti wa chama taifa,makamu mwenyekiti taifa,katibu mkuu,na katibu wa itikadi na uenezi taifa.hao ni wakubwa na wapo juu ya serikali.
 
Tutofautishe nyakati
Tutofautishe nguvu
Tutofautishe ubabe
Tutofautishe uthubutu
Tutofautishe nafasi za kimamlaka serikalini na kwenye chama cha siasa

Ukatibu mwenezi wa chama ni tofauti kabisa na u DC ama u RC.. Ukiwa DC wewe ndio rais wa wilaya.. Yaani kiwilaya hakuna mamlaka mengine ya juu zaidi
Ukiwa RC wewe ndio rais wa mkoa hakuna nafasi ya juu zaidi kimkoa kuzidi hiyo.. Vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko chini yako na una amri ya kimamlaka juu yao
Ukiwa katibu mwenezi wa chama huna madaraka ya kimamlaka na cycle ya watu inayowajibika kwako ni ndogo sana.. Na huna say ya mwisho kwenye lolote.. Ni lazima upokee maagizo kutoka juu
Kwenye hiyo nafasi ya kichama hakuna kamati ya usalama yenye kukusikiliza wewe ..na huna uwezo wa kusweka watu ndani utakavyo!

Makonda alipaishwa kipindi cha mkono wa chuma usioogopa kitu naye akapaa na kuenea vema.. Maguvu na ubabe bila staha kwa mkubwa wala mdogo ndio vilikuwa hobby yake! Alijisikia furaha sana,kudhalilisha yeyote kutokana na madaraka ya kimamlaka aliyokuwa nayo

Sasa hizi ni nyakati tofauti sana na zile.. Na nafasi aliyonayo haina nguvu ya kuamrisha kama zile nyingine... Na kibaya zaidi ndani ya chama kuna mipasuko kama ardhi ya kiangazi.. Huko hakuna ubabe na kuamrisha.. Na kuteuliwa kwake kumezidisha mipasuko.. Kwahiyo ni mwendo wa mitifuano nyuma ya zulia na mitafutano...

Mpaka hapo keshapwaya pakubwa.. Badala ya kung'ara na kuwika anaweza kufunikwa na wanazi wa chama asisikike wala asifurukute kabisa.. Kwakuwa hata ndani ya chama ana maadui wa kutosha sana!

Kitakachomuokoa labda awe kawekwa hapo kwa muda ili kusoma upepo kabla hajapewa nafasi inayoendana na kaliba yake ya kupayuka, kudhalilisha na kutumia maguvu hata panapohitaji diplomasia

Akiachwa hapo atakonda mpaka atapepesuka mwisho tukamuokote MakondekoView attachment 2793723

Sent using Jamii Forums mobile app
Ambiere embu nieleweshe picha hii
 
HALI NDANI YA CCM siyo shwari baada ya Paul Makonda kuteuliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM katika kikao ambacho kilijaa masikitiko na lawama nyingi sana kwa nini na sababu zipi zinafanya apewe hiyo nafasi. Wajumbe wengi wa NEC wametafsiri kuwa ubabe ukitumika kumsimika kwenye nafasi hiyo na wakidai hana sifa za kuwa Mwenezi wa CCM kuna ambao walidiriki kusema bora angeridishwa Polepole au Shaka lakini siyo Makonda.

Chanzo chetu toka ndani ya kikao cha NEC zinasema wa kwanza kabisa kupinga uteuzi wa Makonda alikuwa ni waziri mkuu mstaafu Mzee Mizingo Pinda ambaye alisema " kijana huyu katukana wastaafu wote na kafanya kila aina ya makosa na uovu lakini leo anafaaje kuwa na cheo kikubwa kiasi hiki ndani ya chama" Pinda aliendelea kusema kama kuna ulazima sana wa kurudishwa kwenye serikali au kupewa madaraka basi atafutiwe cheo kingine lakini siyo kuwa mwenezi wa chama kwa sababu ana historia chafu na ya hovyo sana ndani ya chama na nje ya chama na kwa watanzania CCM haitaeleweka kuteua mtu mhalifu kiasi kile kuwa kiongozi tena wa nafasi ya mwenezi.

Hali ilikuwa mbaya zaidi pale wajumbe wengi walipoonekana kutoridhishwa na kuletwa jina la Makonda na wengine mpaka wakaonya kwa nini kunakuwa na mabadiliko ya nafasi ya Katibu Mwenezi wa chama mara tatu ndani ya miaka 2 tu? Kuna mjumbe alihoji kuwa "mwenyekiti ulituletea Shaka ulipoingia,baada ya muda ukamtoa ukamleta Mjema na sasa unamtoa unamleta Makonda shida ni nini"

Baada ya kuona majibizano ni makali sana na wajumbe hawataki kabisa jina la Mkonda tunataarifiwa kuwa Mwenyekiti akaamua kura ipigwe kwa majina mawili aliyopendekeza ambayo yalikuwa nai jina la CHALAMILA na MAKONDA na baada ya kupigwa kura Makonda akamzidi CHAKAMILA kwa kura moja na akawa mwenezi kama ulivyotangwazwa.

Baada ya kikao cha NEC tunaarifiwa Kinana na JK na kundi la vjana wao wanaojiita wamekulia kwenye chama walikubaliana kukutana Dar Es Salaam nyumbani kwa Kinana na kikao kilifanyanyika na moja ya mambo waliyoazimia ni kuwa MAKONDA PAUL hafai kuwa Mwenezi wa CCM na watahakikisha kazi yake inakuwa ngumu sana na wameshaanza chini kwa chini kupeleka sumu mikoani na wilayani kuwashawishi wana CCM kutompa ushirikiano atakapoanza kuzunguka mikoani na mawilayani kwa ajili ya kukitangaza chama.

Suala la pili ni kuwa wamempa jukumu Chenge kuhakikisha kanda ya ziwa CCM inakataliwa kwa kiasi kikubwa na dalili zianze kuonekana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 ili mwaka 2025 kwa pamoja wamtake mwenyekiti wao apishe mtu mwingine asimame kwenye urais kwa kuwa chama kimemkataa na kimepasuka kwa sababu ya maamuzi yake.

Kinana kapewa jukumu la kujiuzulu umakamu uenyekiti kabla ya mwezi December 2023 na aweke wazi kuwa hakubaliani na mwenyekiti kwenye maamuzi mengi na hasa ya kumteua Makonda kuwa Katibu Mwenezi na kuwa hakumshirikisha na hivyo bora akae pembeni kulinda heshima yake na heshima ya chama.

Kwa hiyo muda wowote kuanzia sasa Kinana ataomba kujiuzulu umakamu mwenyekiti wa chama na kukaa pembeni sasa kuratibu mipango ya kumuondoa Rais 2025 akishirikiana na akina Chenge na JK na January Makamba yeye kapewa jukumu la kukusanya fedha za kukamilisha mipango hiyo na anashirikiana na Luhanga Mpina sasa kuoroshesha na kuzunguka majimbo yote ya kanda ya Ziwa ambayo CCM ni lazima ishindwe ili kuwe na sababu ya kumtaka mwenyekiti wao asiwe mgombea 2025 na kwa kifupi wanajipanga kufanya mapinduzi na hawataki Rais Samia awe mgombea 2025.

Sasa wenye kusikia wasikie na wenye kukaa kimya wakae kimya lakini HABARI NDIYO HIYO..

#KigogoMedia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuwa waganga ni kawaida yao kuangalia mananzili yanasemaje kuhusiana na mtu husika kwa huyu naomba tuweke pembeni elimu falaq apewe miezi ndio watu warudi kumjadili sio kwamba nimekwepa swali lako ila tuliwache kwanza!
Iwe ipo kwenye mshtarihi,mirihi au zohali. Kikubwa nyota yamtu ikiwaka kwenye milango yake haizimiki
 
Unamjua Humphrey Polepole .... alikua mwenezi nae ... ndio utajua power ya iyo nafasi.
 
Tuvute subira kitambo kifupi kijacho tutasikia nyepesi za furaha mnooo .. Haya ni maono yangu.. Huko ndani kumekorogeka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom