Makonda apiga simu Clouds Tv 360 kukemea ushoga

Makonda apiga simu Clouds Tv 360 kukemea ushoga

Najiuliza TCRA wako wapi? Waziri mwenye dhamana ndugu Nape atachukulia poa? Au kwa sababu ni washikaji watakausha?
NB: Hili jambo likifumbiwa macho jamii yetu itapata athari mbili;
1. Watoto wataona ni jambo la kawaida
2. Wapo watu na misimamo mikali hawatakubali hili liendelee sisi siyo kisiwa.
Watu wajue asili ya ndoa ni Mume na mke, fullstop.

Baada ya saa 3 ucku, watoto wanaonaje TV? Only in Tanzania
 
Mbona nasikia huko ndo mashoga walikojaaa..na mashabiki wengi nao nimashoga
 
Habari za asubuhi wandugu. Nimeambiwa kwamba jana usiku kwenye TV ya Clouds walikuwa na kipindi maalum ambacho kilikuwa kinazungumzia ushoga na walimkaribisha shoga mmoja ambaye aliletwa saa nzima ya kujifanyia promotion na kuoneshwa kote ambako station hiyo imefika.

Kitendo hicho cha kishenzi kinakwenda kinyume Kabisa na utamaduni na heshima tuliyonayo Kama watanzania, ambao wanalaani aina zote za ushoga. Ninatumaini vyombo vinavyohusika vitachukua hatua kali sana dhidi ya shoga huyo na wale wote waliomfanyia promosheni. Imagine vijana wengine ambao Ndiyo wapenzi wa station zao wanaona picha gani?

Mimi bado ninayo maswali mengi sana kuhusu utangazaji wa Clouds media, ambao kwa kiasi kikubwa umekuwa ukikiuka maadili ya tasnia ya utangazaji na unajiuliza kama iko haja ya kuendelea kuwa na stations zinazochochea mmomonyoko wa maadili kwa kiasi hiki. Huko nyuma vimewahi kusikika visa vya watangazaji kutukanana na hata kupigana wakati kipindi kinakwenda live! Hatua zichukuliwe sasa dhidi yao maana hatujui kesho watakuja kutuletea nini!
 
Mashoga wapo, kama makahaba na watumiaji madawa ya kulevya.

Wafanyakazi wa Afya tunajua haya zaidi, kwa kuwa wanakuja kutibiwa kwetu.

Ni - me/na - fanya kazi kwenye GOT/NGO'S.

Hizi ni "SUPPORTIVE PREVENTIVE METHODS" dhidi ya maambukizi ya VVU.

KWA MFANO;

1. Watumiaji madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano wanaambukizana VVU kwa kuchangia sindano, hivyo wanapewa syringes special ambazo ni unreceycled huku wakiendelea na matibabu ya METHADONE & ushauri. Tunajua vita dhidi ya Addiction yoyote ile sio lelemama.

2. Ni MSM (Men who have sex with Men); Wako kwenye risk kubwa ya kuambukizana VVU & tunao kwenye CLINIC zetu. Ndo ikaja njia ya kuwapa hivyo vifaa kujikinga lakini muda huo huo WANAENDELEA na matibabu & ushauri nasaha.

3. Makahaba wenye VVU; Hawa hupewa dawa & condoms pia. Najua wateja wa makahaba mpo hapa.

Nk....

SIUNGI MKONO USHOGA hata kidogo ILA kuwepo katika SEKTA ya afya kumenifundisha mambo mengi katika umri huu mdogo.

Ukikaa na kuzungumza na hayo makundi 3 niliyotaja, unaweza kutoa machozi.

Cha msingi vita hii IANZIE kwenye NGAZI YA FAMILIA.
 
Kipindi kilihusus nin zaidi... content ya kipindi ndio hasa itanipa picha
 
Ndugu usitake kututaka kutuaminisha hayo mnayoyafanya huko kwenye NGO zenu kuwa yana faida, kwanza kabisa tuangalie fedha mnazolipwa huko zinatoka wapi na masharti ya hao wanaotoa hizo fedha nichukulie mfano wa hili shirika au NGO inayoitwa SAUTI, shirika hili linafadhiliwa na USA na wanaofanya kazi katika shirika hili fedha zao wanazipata direct kutoka kwa wasimamizi na hazipiti kabisa katika mikono ya serikali na ni nyingi za kumwaga.
1. Kama mna nia njema na hizo NGO zenu kwa nini hawa MASHOGA wakati mnafanya registration zao hamuweki annuani au ukazi wa eneo lake sahihi? yaani huwa mnawaorodhesha kuwa wametoka maeneo tofauti na walipo.

2. Kwa nini katika ujumbe wa elimu mnaotoa kwa hao MASHOGA mmekatazwa kabisa kuwashawishi waache tabia hiyo? kuna nini kinachoendelea hapo yaani mnagawa hayo mafuta, Kondom ili watumie tu huku mkifurahia hicho wanachokifanya.
 
Tuangalie hili la ndoa ya jimsia moja limeshahalalishwa sema wanaanza kutafuta namna ya kulitangaza ka hivo. Fatilieni mradi uko funded na USAID unalenga kupunguza maambukiz ya virusi vya ukimwi kwa makundi kama wanaojiuza mashoga na wasagaji ambapo wanashauriwa waache wasipoachwa wanapewa vilainishi. Sasa Kuna atakaeacha na anaona hivo vilainishi. Na mradi mkubwa miaka mitano na selikali ilishaupitisha. Kinachokuja Ni nn hapo ka sio kuueneza ushoga na usagaji
 
Well done Paul Makonda

1467186226546-jpg.361133
 
Back
Top Bottom