Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

Unajua mkuu hatukatai yule ndio mwenye mji lakini "kiubinadamu" unaliona liko sawa? Tuache unafiki, na utakuta hapo alisema marehemu alikuwa mwema na mchapa kazi wakati walitamka ni jipu.
JAMANI MWENYE CLIP YA MANENO ALIYOYAONGEA MAKONDA PALE MSIBANI ATUPIE HUMU.
 
Si umbeya, nadhani iwe fundisho kwa binaadam. Huwezi kuadhiri mtu akiwa hai halafu akifa umseme vizuri.
hili gazeti lina taarifa za umbea sana, sasa hii nayo ni habari ya kuweka front page ili ipeleke ujumbe gani kwa jamii?
e
 
Kweli kitendo cha makonda kwenda kwenye ule msiba "ni upuuzi na kutofikiria kulikotukuka"
Sidhani kama kuna ndugu alifurahishwa na uwepo wake pale. Ikumbukwe kuwa msiba ule haukua shughuri rasmi kumfanya makonda ahudhurie kama mtumishi wa serikali.
Kitendo cha makonda kumsakizia Kabwe kwa Magu, kiliondoa uhalali wa makonda kufahamiana iwe kirafiki au kiserikali. Wawili hawa tayari walikuwa maadui kifamilia na kijamii. So simply he deserved to be ashamed of na what this lady treated him is quite acceptable.
Makonda juha tu na ningefurahi sana angetokea mtu akampopoa mawe au walau kumpiga kipepsi tu ili next time ajifunze kutenda uungwana!
 
Sasa simiyu yetu hiyo mahakama ya mafisadi mbona itakuwa vurugu hayo makesi yatakayo funguliwa huko si itabidi jumba jeupe nalo lisombwe kumbuka kuweka unafiki pembeni CAG ataitwa majumba na boti chakavu nafikiri umenisoma eeee
 
JAMANI MWENYE CLIP YA MANENO ALIYOYAONGEA MAKONDA PALE MSIBANI ATUPIE HUMU.
Mimi binafsi sitaki kuisikiliza maana najua binadamu tulivyo...maneno tunayozungumzaga msibani ni yale yale haijalishi ulikuwa mzuri au mbaya.
 
kwani marehemu aliwahi kufanya ubinadamu? nikumbushe....
Akizungumza katika maombolezo hayo, waziri Simbachawene aliwapa pole wafiwa kwa msiba huo na kutoa salaam za rambirambi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Magufuli.

”Tumepata pigo kama serikali, hakika atakumbukwa kwa mema na mchango alioutoa enzi za uhai wake, nitaungana na wafiwa kuelekea Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kumpumzisha mpendwa wetu,” alisema Simbachawene.

Source: Mamia Wauaga Mwili wa Kabwe Dar
 
Angetumia busara na kutoenda, angetuma mwakilishi kama mwenzake.

Angefanya hivyo pia wangepatikana wa kumsema....Katika mambo mengi niliyojifunza JF ni kuwa kila jambo lina pande mbili kwa watu...Kuna wanaosapoti na kuwakuwa na wanaopinga...Kila jambo....So kikubwa ni mtu kufanya kile unachokiona sahihi kwa upande wako....Na yeye ndo ameamua hvyo
 
Ni ujinga tu wa huyu makonda

Anajua fika kwenda kwake pale anawaongezea wafiwa maumivu

Kiherehere cha nini kujipeleka...si angeenda mkuu wa wilaya

Huu ni ukosefu wa Ubinadamu

Lile lilikuwa suala la kifamilia....Alitakiwa tu kutumia common sense
Mkuu kunawatu mpaka kesho tunasema elimu yao haijawasaidia ndo huyu bwana,hafanyi mambo yake kama yeye bali anaiga enzi ya Baba riz alikua kajikita kweli kwenye michezo na tulikua tunamsikia sana radio clouds kwa kuhamsisha michezo kwakua yule mkuu alikua akifanya hivyo.Leo ndo anajitia kuvaa uzalendo eti nae mpenda maendeleo,kwanini asianze ndangu mwanzo.UGOPA SANA KUFUATA UPEPO UTAPOTEA.
 
Sioni cha kujadili hapa sioni kosa la makonda kisheria yeye ni mtendaji tu je marehemu alisingiziwa? Jamani watanzania tusipende kujadili saanaa habari nyepesi kama hii kutopewa mkono mbona kawaida tu mitaani majirani tu hawasalimiani ndugu hawazikani sioni habari hapo waandishi hawa jamani
MKUU MSIBA ULE SIO SEHEMU YA KAZI ZA BWANA MAKONDAKTA, ALIPASWA TU KUTUMIA COMMON SENSE NA KUTUMA MWAKILISHI.
 
Akizungumza katika maombolezo hayo, waziri Simbachawene aliwapa pole wafiwa kwa msiba huo na kutoa salaam za rambirambi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Magufuli.

”Tumepata pigo kama serikali, hakika atakumbukwa kwa mema na mchango alioutoa enzi za uhai wake, nitaungana na wafiwa kuelekea Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kumpumzisha mpendwa wetu,” alisema Simbachawene.

Source: Mamia Wauaga Mwili wa Kabwe Dar
Hahaa.. Marehemu hata akiwa jambazi nguli husifiwa, we vepe
 
Hakutakiw kwenda angetuma mwakilishi wake! Ana misifa ya kitoto na kijinga! Akikua ataacha!! Amemharibia sifa Rais hakuwa na style ya kufanya kazi kitoto namna ile! Time will tell
 
Back
Top Bottom