Makombora kwa Forever Living Products (FLP)

Hivi na wale wanaotoa ushuhuda kuwa wamefanikiwa kupitia Forever kumbe ni danganya Toto!
 
Unachelewa kutajirika kijana, humu kuna failures wengi hutakaa upate ushauri wa maana.

Unamuuliza maskini mbinu za kutajirika?
 
Hivi na wale wanaotoa ushuhuda kuwa wamefanikiwa kupitia Forever kumbe ni danganya Toto!

Mimi waliniigiza mkenge nikaishia kuyanywa madawa mimi mwenyewe.... wewe chunguza walivyochoka wanachama wao hata hao wanaosema eti wametajirika hata siamnini kabisa fungua genge mkuu utajiri wa mkato hakuna
 
Usijaribu hii biashara inafaidisha wale wanachama wa mwanzo tu,ukiingia mkenge sana sana utakuwa unamnyanyua aliye juu azidi kupaa huku wewe ukiambilia ushuhuda na kutiwa moyo siku yako itafika.

Kwanza bei ya hizo dawa ipo juu sana ukifanya mchazo utaishia kununua mwenyewe.
 
Ok wakuu nafata ushauri wenu mi ngoja ni Hustle na hii hii kozi yangu ninayosomea Kwamsaada wa Mungu nitafankiwa.
 
Huwezi kutajirika haraka haraka, kumbuka kuwa mafanikio ni process ya muda mrefu katika maisha. Ukiingia jaribu kutengeneza network then utaanza kuona mafanikio
 
Kwanza si rahisi kupata ushauri ulio bora kwa mtu yeyote asiye lijua jambo husika vizuri, biashara hii ni halisi na unaweza kutajirika sana ila kuna changamoto kadhaa na ukizimudu basi utafanikiwa sana. Kwa ufupi biashara hii ni tofauti na zile za kununua na kuuza, ni biashara ya kushirikisha na kuonyeshana sehemu ya kununua bidhaa kwa matumizi yetu majumbani na si kwa nia ya kuuza kwani bidhaa ni ghali kidogo , katika manunuzi ya wale uliowaonyesha wewe na wale walionyeshwa na wale uliowaonyesha wewe basi utapata commission kutoka manunuzi yao pamoja na manunuzi yako mwenyewe. Kazi ni kuwaelewesha watu wakuelewe na waendelee kununua bidhaa hizo na ukiweza kuunda team imara kipato cha 1ml mpaka 10mil kwa mwezi ni kipato cha kawaida sana. Kwa wale wataalamu wa hesabu ingieni kwenye mtandao wa kampuni na someni policy ya biashara mtaona commissions ziko wazi sana na zinaeleweka vizuri wala hakuna kificho chochote. Kiukweli ni biashara ngeni ukanda wetu kwani sisi tumezoea biashara za kununua na kuuza.
 
Usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Sasa kama wewe uliyeingia ukashindwa kuifanya mwisho wa siku unakuja kuropoka unanunua dawa laki mbili, nani alikwambia Forever inatengeneza dawa? Chunguza na ufahamu unachotaka kukiongea halafu ukiongee mbele ya umma
 
Hivi na wale wanaotoa ushuhuda kuwa wamefanikiwa kupitia Forever kumbe ni danganya Toto!

Wale ni shida ukifika watakuwekea DVD za watu walio fanikiwa watakumbia huyu alikuwa anuza mkaa na sasa analiliki Range, mara huyu alikuwa fundi viatu kwa sasa anamiliki Hummer, Halfu wao mafanikio ni Gari kari na Nyumba basi ndi kikomo chao cha mafanikio. Hawawezi onyesha mtu kanunua TOYO wao ni magari tu tena ya Milioni 300 and above
 
Kwanza si rahisi kupata ushauri ulio bora kwa mtu yeyote asiye lijua jambo husika vizuri, biashara hii ni halisi na unaweza kutajirika sana ila kuna changamoto kadhaa na ukizimudu basi utafanikiwa sana. Kwa ufupi biashara hii ni tofauti na zile za kununua na kuuza, ni biashara ya kushirikisha na kuonyeshana sehemu ya kununua bidhaa kwa matumizi yetu majumbani na si kwa nia ya kuuza kwani bidhaa ni ghali kidogo , katika manunuzi ya wale uliowaonyesha wewe na wale walionyeshwa na wale uliowaonyesha wewe basi utapata commission kutoka manunuzi yao pamoja na manunuzi yako mwenyewe. Kazi ni kuwaelewesha watu wakuelewe na waendelee kununua bidhaa hizo na ukiweza kuunda team imara kipato cha 1ml mpaka 10mil kwa mwezi ni kipato cha kawaida sana. Kwa wale wataalamu wa hesabu ingieni kwenye mtandao wa kampuni na someni policy ya biashara mtaona commissions ziko wazi sana na zinaeleweka vizuri wala hakuna kificho chochote. Kiukweli ni biashara ngeni ukanda wetu kwani sisi tumezoea biashara za kununua na kuuza.
Acha kudanganya watu hapa, hii ni Pyramidi wale wa kwanza kabisa kuingia ndo wanapiga pesa, Halfu hii biashara inawalenda watu wa Maisha ya kati, ndo hao wanao weza kununua dawa ya meno kwa sh 12,000/ au 20,000/ kwa mtu wa kipato cha chini sio rahisi,

Kuna usanii mwingi sana na kudanganyana kwingi sana, kuna maigizo kibao huwa wanafanya hata yale magari amabyo wanajifanya kuzawadia watu huwa ni kanyaboya tu, tatizo wengi huwa hamjui ule mchezo.

Ishu nyingine ni kwamba hii biashara inapromote, importations na haikuzi hata kidogo uchumi wa nchi make hayo madawa yote ni Made in nje ya nchi.

Ishu nyingine wao wanaamini biashara ni ya kuuza madawa tu, kwao biashara zingine si biashara, yaani hata kama una mgahawa wa chakula kwao wanaona hiyo sio biashara wao wanaamini biashara ni kuuza madawa yao pekee
 
Kwanza si rahisi kupata ushauri ulio bora kwa mtu yeyote asiye lijua jambo husika vizuri, biashara hii ni halisi na unaweza kutajirika sana ila kuna changamoto kadhaa na ukizimudu basi utafanikiwa sana. Kwa ufupi biashara hii ni tofauti na zile za kununua na kuuza, ni biashara ya kushirikisha na kuonyeshana sehemu ya kununua bidhaa kwa matumizi yetu majumbani na si kwa nia ya kuuza kwani bidhaa ni ghali kidogo , katika manunuzi ya wale uliowaonyesha wewe na wale walionyeshwa na wale uliowaonyesha wewe basi utapata commission kutoka manunuzi yao pamoja na manunuzi yako mwenyewe. Kazi ni kuwaelewesha watu wakuelewe na waendelee kununua bidhaa hizo na ukiweza kuunda team imara kipato cha 1ml mpaka 10mil kwa mwezi ni kipato cha kawaida sana. Kwa wale wataalamu wa hesabu ingieni kwenye mtandao wa kampuni na someni policy ya biashara mtaona commissions ziko wazi sana na zinaeleweka vizuri wala hakuna kificho chochote. Kiukweli ni biashara ngeni ukanda wetu kwani sisi tumezoea biashara za kununua na kuuza.

Acha snema mkuu....
 
Ukiwa hulijui jambo fulani kwa undani jaribu kuvuta subira kidogo na ukubali kueleweshwa ili mshauriane vizuri katika jambo husika.
 
Back
Top Bottom