Ukiacha hiyo ya wa Izrael ambayo ni kama kuchanganya style nyingi za Japan/China na boxing, Warusi wao walikuja na yao ambayo ni mbaya zaidi. Hii hata USA wanasema wazi kabisa kuwa ni mbaya zaidi.
Komandoo huwa hana SILAHA maalumu. Komandoo ni mtu anayeweza kutumia kila kilicho karibu naye ili kujilinda. Kuna yule aliyehusika kutaka kumpindua/kumuua Nyerere ambaye alipozingirwa, bado alirukia Pick-Up iliyokuwa ikipita kasi na akaanza kuwarushia askari waliokuja kumkamata, chupa za bia.
Kuna mmoja ambaye yeye alikuwa zaidi kama JASUSI, hata nguo za jeshi alikuwa havai. Ila vita ya Uganda, alienda kupigana. Jamaa huwa akisema analala dakika kadhaa, basi dakika moja kabla, huamka kweli. Ni watu walio na uwezo wa hali ya juu na kunusa hatari inayoweza kuja.
Si rahisi Komandoo na Komandoo kupigana kwa sababu, mara nyingi wanapigana katika pande mbili tofauti. Kwa mfano, Komandoo wa Tanzania, siku zote walipigana nyuma ya front line ya Askari wa Amini, na wao wakiwa nyuma ya front line yetu. Hawa wanakuwa wanalipua magari yanayoleta chakula, kumwaga sumu na kutega mabomu sehemu wanazojua mtakuja nk nk.
USA ukiacha hao SEAL na sijui MARINES, wengine ni hawa waitwao The United States Army Special Forces
(Green Berets) . Hawa pana siku niliona kipindi wakielezea jinsi walivyokuwa wakivamia Bank na kuiba. Siku moja wakawazunguka Polisi kibao. Polisi walikuwa wakitokea na bunduki zao huku wakimimina risasi, jamaa wanageuka na kurusha risasi moja tu, Polisi kwishieni. Waliwamiminia risasi nyingi sana kama zile film za Hollywood ila mijamaa ilikuwa na roho ngumu kama PAKA. Baada ya kuwa wameshakula risasi nyingi sana (mmoja alichukua zaidi ya 20 kama sikosei) ndipo kwa shida sana yakafa yote. Polisi hawakuamini walichokiona siku hiyo na ikabidi wawahi kujua ni raia gani hao. Riport ilipokuja kuwa walikuwa ni GREEN BERET, basi kila mtu akatoa salute kwa Wanaume.
Kama nilivyosema, Warusi wana Style yao ambayo hufundishwa hata KUUMA kama ikibidi. Hii style ni kuwa haina formula na kila kitu kinaruhusiwa ili mradi uuwe au kuumiza sana. Hiyo kitu inaitwa SYSTEMA. Usiombe ukutane na mpiganaji wa SYSTEMA maana atakuumiza vibaya sana kama siyo kukuuwa. Warusi ukiacha kufundishwa kupigana kwenye SYSTEMA, pia wanafundishwa KUVUMILIA maumivu ya hali ya juu. Hapo wanakuwa kama GREEN BERET ila sema piganaji yao inaacha adui zao hoi.