Tetesi: Makinikia yameanza kusafirishwa tena?

kedekede

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
5,298
7,646
Wakuu,
Kwa niliyayona jana na juzi sitasalimia naenda moja kwa moja kwenye maandiko yangu.

Nilisafiri kwenda kijijini mara moja kwenda kutafuta mazao kwani wakulima nikafika kijiji kimoja kinaitwa Ilogi huku Kakola mkoani Shinyanga. Nikiwa katika mizunguuko nikakuta malori haya makubwa Semi Trailer yanaelekea Mgodini bulyanhulu.

Nilishangaa kidogo maana nilihesabu nikafika 40 nikaacha kuendelea kuhesabu vumbi lilikuwa kubwa sana.Hiyo ni juzi jioni.Nikajisemea ngoja niendelee na kuhangaikia yaliyonileta niachane na mambo ya watu.

Jana mchana nikiwa nakula wali samaki nikaona vumbi limeanza nikasema niangalie kunani.Hamadi Malori yakaanza kuelekea kahama au Mwanza mimi sijui maana yalitokea upande wa mgodini yakawa yanapita kijiji cha Kakola,mimi nilikuwa Kili Time. Baada ya kuhesabu Malory yakafika 52 niliamua kuacha nikaamua kuawadadisi watu waliopo jirani yangu.

Majibu niliyopewa yalinihuzunisha sana sana sana. Niliambiwa ni Makinikia yameanza kusafirishwa na yale maalory yalikuwa yamebeba huo mchanga kwenda kuuprocess nje ya Tanzania. Majirani zangu waliniambia mchanga uliokuwa umezuiliwa kipindi cha Rais Wangu usitoke sasa unatoka maana hayupo Tena.

Machozi yalinilengalenga nikajiuliza swali ambalo sikupata jibu. Nimekuja ili Mnijibu Nyie.

JE HII NI KWA FAIDA YA NANI?AU NI SAWA NA NDEGE AINA YA KANGA MWENYE CHONGO AU JICHO MOJA KILA AKICHAKUA/FUKUA ANAWAFUKULIA WAZIMA(WENYE MACHO YOTE MAWILI?)

Jioni Tena malory yakaanza kuingia kutoka mjini kwenda mgodini, sikuona sababu ya kuhesabu niliamua kuondoka maeneo yale ambapo ningeweza kuhesabu malori nakaingia Minza ambapo malory huyaoni maana hayapiti maeneo hayo.

Leo sitakaa maeneo ya barabara kuu najua yatapita tu malori yanayotibua nafsi yangutena.

Je hiki ndicho tulichokuwa tunakitaka? Nani anafaidika? Kwa manufaa ya nani? Au ndio wamepewa Ruksa kama wawekezaji? Au wapiga dili wameanza?
 
Majibu niliyopewa yalinihuzunisha sana sana sana.Niliambiwa ni Makinikia yameanza kusafirishwa na yale maalory yalikuwa yamebeba huo mchanga kwenda kuuprocess nje ya Tanzania.Majirani zangu waliniambia mchanga uliokuwa umezuiliwa kipindi cha Rais Wangu usitoke sasa unatoka maana hayupo Tena.
Acha uongo, Magu hakuwahi kuzuia huu mchanga usisafirishwe, ilikua kiki tu. Au kile kishika uchumba kilikua cha nini? Unataka kusema SAMIA ndio karuhusu?
 
Una uhakika yameanza kusafiri hayo maroli baada ya kifo cha rais wako uliyesema? Waulize vizuri hao wenyeji wako hapo Kili time ni linii exactly yalianza upya kusafirisha huo mchanga hayo maroli.
Nina zaidi ya miezi miwili nimekuja 22 march,sijawahi kuyaona Malori ya mchanga na kama yalikuwepo yalikuwa ni moja au mawili,hii ni kama exodus!Kili Time ni Bar ipo kakola sio kampuni ya kusafirishia!
 
Acha uongo, Magu hakuwahi kuzuia huu mchanga usisafirishwe, ilikua kiki tu. Au kile kishaka uchumba kilikua cha nini? Unataka kusema SAMIA ndio karuhusu?
Mgodi ulifungwa lini wa Barric?Na ukafunguliwa lini?Na kwa nini Ulifungwa kwa miaka mitatu na ukafunguliwa recently?
 
Unajua kedekede kwa mtu mwenye kujua uchimbaji wa haya makampuni ukizungumzia habari za mchanga wa makinikia ukaanza kuhusisha sijui wanaiba dhahabu na madini mengine (Marehemu Rais alisema hadi tani inafika kwa yanayoibiwa) huwa anakuchukulia tofauti sana. Nikushauri kitu kidogo sana kwa kuwa umesema upo Kakola, hebu tafuta mtaalam wa madini mzalendo aliyepo kwenye hiyo kampuni ya Buli, hebu muulize kwa undani kabisa akufafanulie nini kinatokea mwanzo hadi mwisho kuhusu hayo makinikia. Itakusaidia sana na pengine utaacha kuumwa roho kwa kitu cha kufikirika

Usitafute mzungu, tafuta Geologist wa kitanzania tu. (Au utaamini nae anatumika na mabeberu?)
 
Magufuli aliyazuia had walipo weka utaratibu alio ukubali yeye na yakaanza kusafirishwa kwa escort ya polisi mwanzo yalikua yanaondoka bila escort ya polisi na hapa kipind Cha kat kat yalisimama kwanza kutoka ila sahiv yameanza Tena lakin hata magu akiwepo yalitoka pia
 
Wakuu,
Kwa niliyayona jana na juzi sitasalimia naenda moja kwa moja kwenye maandiko yangu.
Nilisafiri kwenda kijijini mara moja kwenda kutafuta mazao kwan wakulima nikafika kijiji kimoja kinaitwa ilogi huku kakola mkoani shinyanga.Nikiwa katika mizunguuko nikakuta malori haya makubwa Semi Traller yanaelekea Mgodini bulyanhulu.
Nilishangaa kidogo maana nilihesabu nikafika 40 nikaacha kuendelea kuhesabu vumbi lilikuwa kubwa sana.Hiyo ni juzi jioni.Nikajisemea ngoja niendelee na kuhangaikia yaliyonileta niachane na mambo ya watu.Jana mchana nikiwa nakula wali samaki nikaona vumbi limeanza nikasema niangalie kunani.Hamadi Malori yakaanza kuelekea kahama au Mwanza mimi sijui maana yalitokea upande wa mgodini yakawa yanapita kijiji cha Kakola,mimi nilikuwa Kili Time
Baada ya kuhesabu Malory yakafika 52 niliamua kuacha nikaamua kuawadadisi watu waliopo jirani yangu.Majibu niliyopewa yalinihuzunisha sana sana sana.Niliambiwa ni Makinikia yameanza kusafirishwa na yale maalory yalikuwa yamebeba huo mchanga kwenda kuuprocess nje ya Tanzania.Majirani zangu waliniambia mchanga uliokuwa umezuiliwa kipindi cha Rais Wangu usitoke sasa unatoka maana hayupo Tena.Machozi yalinilengalenga nikajiuliza swali ambalo sikupata jibu.Nimekuja ili Mnijibu Nyie.
JE HII NI KWA FAIDA YA NANI?AU NI SAWA NA NDEGE AINA YA KANGA MWENYE CHONGO AU JICHO MOJA KILA AKICHAKUA/FUKUA ANAWAFUKULIA WAZIMA(WENYE MACHO YOTE MAWILI?)
Jioni Tena malory yakaanza kuingia kutoka mjini kwenda mgodini, sikuona sababu ya kuhesabu niliamua kuondoka maeneo yale ambapo ningeweza kuhesabu malori nakaingia Minza ambapo malory huyaoni maana hayapiti maeneo hayo.Leo sitakaa maeneo ya barabara kuu najua yatapita tu malori yanayotibua nafsi yangutena.
Je hiki ndicho tulichokuwa tunakitaka?Nani anafaidika?Kwa manufaa ya nani?Au ndio wamepewa Ruksa kama wawekezaji?Au wapiga dili wameanza?
Vipi ulipata ile noah yako.maana tuliambiwa yana thamani ya trilioni 3000
 
Mkuu yan siku zote hizoo hujui km yanasafirishwa hata kabla shujaa hajasepa zake?? Halaf vitu vingine mjifunze kutafuta facts, yale ma report ya makanikia kipindi kile hayako realistic kbs. Akili za kuambiwa mix na zako chief utaumia moyo bure for no reason.
 
Unajua kedekede kwa mtu mwenye kujua uchimbaji wa haya makampuni ukizungumzia habari za mchanga wa makinikia ukaanza kuhusisha sijui wanaiba dhahabu na madini mengine (Marehemu Rais alisema hadi tani inafika kwa yanayoibiwa) huwa anakuchukulia tofauti sana. Nikushauri kitu kidogo sana kwa kuwa umesema upo Kakola, hebu tafuta mtaalam wa madini mzalendo aliyepo kwenye hiyo kampuni ya Buli, hebu muulize kwa undani kabisa akufafanulie nini kinatokea mwanzo hadi mwisho kuhusu hayo makinikia. Itakusaidia sana na pengine utaacha kuumwa roho kwa kitu cha kufikirika

Usitafute mzungu, tafuta Geologist wa kitanzania tu. (Au utaamini nae anatumika na mabeberu?)
Mtu mweusi ni dhaifu Sana mbele ya Pesa,hata mererani mbona kuna njia za Chini kwa chini.Linda juu chini mali inaondoka.
 
Mkuu yan siku zote hizoo hujui km yanasafirishwa hata kabla shujaa hajasepa zake?? Halaf vitu vingine mjifunze kutafuta facts, yale ma report ya makanikia kipindi kile hayako realistic kbs. Akili za kuambiwa mix na zako chief utaumia moyo bure for no reason.
Sasa sote tujiulize,nchi hii kweli tutafika!?Kwani Delilah yy anasemaje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom