Tetesi: Makinikia yameanza kusafirishwa tena?

Leo yametoka malori ya makinikia 40,nimehasabu.Yanalindwa na mapolisi.Yanaelekea mjini.Nadhani bandarini wanajua.Hii ni exodus!
 
Wakuu,
Kwa niliyayona jana na juzi sitasalimia naenda moja kwa moja kwenye maandiko yangu.

Nilisafiri kwenda kijijini mara moja kwenda kutafuta mazao kwani wakulima nikafika kijiji kimoja kinaitwa Ilogi huku Kakola mkoani Shinyanga. Nikiwa katika mizunguuko nikakuta malori haya makubwa Semi Trailer yanaelekea Mgodini bulyanhulu.

Nilishangaa kidogo maana nilihesabu nikafika 40 nikaacha kuendelea kuhesabu vumbi lilikuwa kubwa sana.Hiyo ni juzi jioni.Nikajisemea ngoja niendelee na kuhangaikia yaliyonileta niachane na mambo ya watu.

Jana mchana nikiwa nakula wali samaki nikaona vumbi limeanza nikasema niangalie kunani.Hamadi Malori yakaanza kuelekea kahama au Mwanza mimi sijui maana yalitokea upande wa mgodini yakawa yanapita kijiji cha Kakola,mimi nilikuwa Kili Time. Baada ya kuhesabu Malory yakafika 52 niliamua kuacha nikaamua kuawadadisi watu waliopo jirani yangu.

Majibu niliyopewa yalinihuzunisha sana sana sana. Niliambiwa ni Makinikia yameanza kusafirishwa na yale maalory yalikuwa yamebeba huo mchanga kwenda kuuprocess nje ya Tanzania. Majirani zangu waliniambia mchanga uliokuwa umezuiliwa kipindi cha Rais Wangu usitoke sasa unatoka maana hayupo Tena.

Machozi yalinilengalenga nikajiuliza swali ambalo sikupata jibu. Nimekuja ili Mnijibu Nyie.

JE HII NI KWA FAIDA YA NANI?AU NI SAWA NA NDEGE AINA YA KANGA MWENYE CHONGO AU JICHO MOJA KILA AKICHAKUA/FUKUA ANAWAFUKULIA WAZIMA(WENYE MACHO YOTE MAWILI?)

Jioni Tena malory yakaanza kuingia kutoka mjini kwenda mgodini, sikuona sababu ya kuhesabu niliamua kuondoka maeneo yale ambapo ningeweza kuhesabu malori nakaingia Minza ambapo malory huyaoni maana hayapiti maeneo hayo.

Leo sitakaa maeneo ya barabara kuu najua yatapita tu malori yanayotibua nafsi yangutena.

Je hiki ndicho tulichokuwa tunakitaka? Nani anafaidika? Kwa manufaa ya nani? Au ndio wamepewa Ruksa kama wawekezaji? Au wapiga dili wameanza?

kwani nani alisaini mikataba?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom