Makinda: Weee sugu!!! Tusianze kutafutana!

Makinda: Weee sugu!!! Tusianze kutafutana!

hivi kabla ya Anna Makinda kuwa mbunge and forth alikuwa anafanya kazi gani?? ama profession yake ni nini hasa??

Alikuwa mganga wa kienyeji, akajipitisha pitisha ccm mpaka kapata ubunge
 
Kuna Wabunge wanastahili kuchapwa bakora hasa huyo mvuta bangi
 
labda anataka amwongezee mtoto kama aloko nao hawamtoshi na mume ndo hakubaatika kupata

Mkuu, hivi bi - Kiroboto ana mtoto ? Ni dhahiri angelikuwa na mtoto asingekuwa na roho mbaya kiasi kile.
 
Baada ya mbunge wa Mbeya mjini mheshimiwa Joseph Mbilinyi kumuambia waziri wa habari utamaduni na michezo kuwa ataondoa shilingi kama hatajibu kwa kina ni kwa nini kitabu cha waziri wa habari utamaduni na michezo hakija ongelea chochote kuhusiana na kutekwa, kuong'olewa kucha na macho kwa wandishi wa habari.

Spika akamuambia "Wee sugu, mheshimiwa Mbilinyi, tusianze kutafutana,.. Hatuna muda wa kupoteza hapa". Tuendeleee.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
huyu mama hajitambui kabisa
 
Duh! Mnaleta UMAMA bungeni? Mtu mwenyewe hana ata mtoto!

Maskini huyu mu bibi hivi ni kweli hana mtoto?hii imekaa je jamani ane mjua tupe data,lakini kama hana watoto basi ndio sababu yakuwa na hasira namna hii.....na je mume anae?leo namuona kama vile amevaa pete ya ndoa...naiamini jamii forums haikosi wenye data naombeni kunijuza mweee
 
Baada ya mbunge wa Mbeya mjini mheshimiwa Joseph Mbilinyi kumuambia waziri wa habari utamaduni na michezo kuwa ataondoa shilingi kama hatajibu kwa kina ni kwa nini kitabu cha waziri wa habari utamaduni na michezo hakija ongelea chochote kuhusiana na kutekwa, kuong'olewa kucha na macho kwa wandishi wa habari.

Spika akamuambia "Wee sugu, mheshimiwa Mbilinyi, tusianze kutafutana,.. Hatuna muda wa kupoteza hapa". Tuendeleee.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.

udhaifu wa kiti cha spika unaendelea kuongezeka kwa kasi kubwa sana.Mhimili wa umekosa dira na mwelekeo kiasi serikali inaendeleza madudu yake.Lakini kwa kuwa huu ni mpango wa Mungu tuiache ijikaange kwa mafuta yake yenyewe
 
Nafikiri ilibaki kusema.......Wee Sugu, kelele...alaah!
 
[h=3]Thursday, May 23, 2013 | 9:20 AM[/h]



KATIKA hali iliyoonesha sintofahamu, jina la utani la Mbunge wa Mbeya Mjini kwa ‘leseni’ ya Chadema, Mhe. Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’ lilionekana kumtatiza Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Anne Semamba Makinda.

Ilikuwa wakati Mbilinyi akizungumza kwa niaba ya kambi rasmi ya upinzani kuchangia bajeti ya Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo ya Mhe. Fenella Mukangara ndipo alipotibua mambo yaliyosababisha spika atatizwe na jina lake la Mbilinyi.

Mhe. Mbilinyi alipofika ukurasa wa nane wa hotuba yake yenye kurasa 54, Mbunge wa Mbozi Mashariki, Mhe. Godfrey Zambi (CCM) aliomba mwongozo (kuomba mwongozo ni kumtaka anayehutubia kuacha na kurudi kwenye kiti kisha aliyeomba aongee).

Ndipo Spika Makinda alipomtaka Mhe. Mbilinyi akatishe hotuba yake ili Zambi azungumze.

Hata hivyo, Mbilinyi aliendelea kutiririka kwa sekunde kadhaa kabla ya kutii amri ya spika.

Ilimlazimu spika kumwambia tena akisema: “We mheshimiwa Sugu…” kauli iliyoamsha kicheko kwa wabunge huku Sugu mwenyewe akiwa ameondoka kwenye kipaza sauti huku akimwekea spika alama ya vidole viwili inayotumiwa na Chadema.

Mhe. Zambi alitoa hoja kuhusu hotuba ya Sugu kujaa maneno ya uchochezi.
Spika Makinda kwa uwezo wake aliamua kuliahirisha bunge mpaka saa 10:00 jioni ya siku hiyo akimtaka Sugu kwenda kuondoa maneno yenye uchochezi katika hotuba yake.

Jioni ilipofika, Sugu akapewa nafasi ya kuzungumza ambapo alianza kwa kusema: “Mheshimiwa spika, natamka ndani ya bunge kwamba kuanzia leo jina la Sugu lisitumike.”

Spika akadakia hapo na kusema: “Tena imekuwa afadhali maana mi mwenyewe sijui ni Sugu au Suguru.”

Kauli hiyo ya Spika Makinda ilisababisha wabunge waangue vicheko.






Read more: JINA LA SUGU LAPIGWA 'STOP' KUTUMIKA BUNGENI....! - GUMZO LA JIJI
 
Hahahahaha!! Sugu kaliona hilo, maana point zake zitakuwa zinachukuliwa kama utani utani wakati anatema cheche za ukweli!!
 
Asingekata hili tungefika mahali ungesikia Mbunge anachangia hojaaaa na mwisho anahitimiza "Mheshimiwa Bi. Kiroboto naomba kutoa hoja"
 
Kwi! Kwi! Kwi! Kwi! Mimi nilidhani katimuliwa bungeni kwa sababu ya kumpa Kadi ya CDM Profesa J ! Kumbe hiiivyoo !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom