Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Wabunge wawili vijana wanaoheshimika na jamii ya Bongo Fleva, Joseph Mbilinyi (Sugu) na Joseph Haule (Profesa Jay) na wakali wa Hip Hop wa muda wote Tanzania, wamekiri kuwa ilikuwa ni kilio chao siku zote, kutaka wasanii wafikie hatua iliyofikiwa na Diamond.
Professor Jay amefunguka na kusema kuwa anafurahishwa sana na jitihada binafsi zinazofanywa na Diamond kiasi kwamba sasa amekuwa msanii mkubwa Afrika, jambo linalomtia moyo, hasa akikumbuka siku kijana huyo kutoka Tandale alipomwaga machozi mbele yake.
“Ni jambo jema kabisa kwamba Diamond sasa anatubeba wasanii wote, lazima tumpongeze maana anakoelekea, ndiko tulikokuwa tukipigania miaka yote.”
Professor Jay amefunguka zaidi kuwa Diamond aliwahi kulia mbele yake, kufuatia Diamond utoamini kuwa ipo siku atafikia level kama za Professor Jay, wala kufanya wimbo na Proffesor Jay.
“Nilipomuuliza analia nini, [Diamond] aliniambia hakuwahi kuwaza maishani mwake kama kuna siku anaweza kufanya wimbo na Profesa Jay, hakuwahi kuamini kama anaweza kufikia levo zangu, jambo hili lilinigusa sana na najua mimi ni mmoja wa wasanii waliom-inspire kuupenda na kuufanya muziki,” alisema mkongwe huyo aliyemshirikisha Diamond katika kibao chake cha Kipi Sijasikia.
Jay alisema Diamond anawa-inspire vijana wengi kutokana na juhudi zake na mafanikio anayoyapata ni ishara kwamba ukiwa na nia na kitu utafanikiwa kama utajibidisha.
Aidha Professor Jay amefunguka zaidi na kumsifu Diamond kwa kupata shavu la kuwa mmoja wa wasanii watatu wanaofanya muziki barani Afrika, ambao watapanda katika jukwaa la ukumbi maarufu wa Barclays Centre, jijini New York nchini Marekani, Julai 22, mwaka huu wenye uwezo wa kuingiza watu 20,000 katika tamasha lililopewa jina la One Africa
“Ninaufahamu huo ukumbi ni mkubwa sana kwa kweli, kumuona mtu kama Diamond anakwenda kufanya shoo pale ni jambo la kufurahisha sana. Kwa maoni yangu, muziki wa Bongo unakwenda kubatizwa rasmi pale, kwamba sasa tunaingia katika ramani halisi ya dunia kimuziki,” anasema Profesa Jay.
Kwa upande wake, Sugu alisema siku zote alikuwa katika harakati za kutaka msanii wa nchi hii aheshimike, hatua ambayo Diamond amefikia.
“Natambua uwezo wake na jitihada zake, mimi sizungumzii tu muziki, bali biashara ya muziki, tunataka tuwe na ma-CEO wasanii, watu ambao tunaweza kutengeneza ajira kupitia muziki. Katika hotuba yangu kama Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, nimeitaka serikali kutoa mwongozo kwa redio na televisheni nchini, kupiga asilimia 80 ya muziki wa nyumbani na unaobaki ndiyo uwe wa nje.
“Maana huwezi kufahamika kimataifa bila kwanza kufahamika nyumbani, tunataka hivi kwa sababu tunahitaji kuwa na akina Diamond wengi, akina Samatta (Mbwana, mwanasoka) wengi, kwa hiyo ni lazima serikali itoe fursa hizi, siyo mtu anajibidisha mwenyewe, akipata mafanikio mtu wa serikali anajitokeza kumpongeza kana kwamba walijihusisha naye.
“Diamond anafanya vizuri sana na kwa kweli tunajivunia, tunataka tuwe kama wenzetu Nigeria, kule kuna akina P Square, Davido, 2Face Idibia na wengine wengi wanafahamika kimataifa, au DRC wapo akina Koffi Olomide, Fally Ipupa, Feregora, Werasson na wengine na sisi tunatakiwa tuwe na kina Diamond, Ali Kiba, AY, yaani tuwe nao wengi,” anasema Sugu.
Source: Tanzania Today