Tamko la BAVICHA Serengeti kuhusu Uandikishaji wa BVR Nchini

Kamanda Francis

JF-Expert Member
Nov 30, 2013
834
140
TAMKO LA "BAVICHA SERENGETI MARA" KUHUSIANA NA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA WAPIGA KURA KWA MFUMO WA BVR NCHINI.

TAARIFA KWA VYOMBO VYOTE VYA HABARI NCHINI


Ndugu Waandishi wa habari,
Awali ya yote niwapongeze kwa juhudi na jitihada zenu mnazozionyesha katika kuhakikisha kwamba Wananchi waliomo ndani na nje ya mipaka ya Taifa letu wanapata habari zinazohusu Taifa lao kwa wakati mwafaka tena zenye uchambuzi wa kina na wa Uhakika zaidi.

Ndugu waandishi wa habari,
Natumai mnatambua juu ya Zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura kwa Mfumo wa Kielektroniki maarufu kama "BVR Systeam", linaloendeshwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Nchini hivi sasa.

Licha ya kwamba Zoezi hili linaendeshwa kimkakati na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa maelekezo ya wale wanaojiita vigogo wa CCM, Viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) chini ya Mwenyekiti wake Jaji Damian Lubuva, wameendelea kukaa kimya kama hawasikii wala kuona kinachoendelea Nchini kuhusiana na ukiukwaji wa taratibu za Uandikishaji unaofanywa na baadhi ya Watendaji wa Tume wanaoratibu Zoezi hili aidha kwa maelekezo ya wale wanaojiita vigogo wa CCM au kwa kufanya maksudi kutokana na kwamba wamezoea kuratibu shughuli za Kitaifa kwa misingi ya kubebana hata wanapokutwa na makosa katika utendaji wao mbovu.

Ndugu waandishi wa habari,
Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara, linalaani vitendo hivi vinavyofanywa na baadhi ya Watendaji wa Tume ya Uchaguzi wasio waaminifu na waadilifu katika Utendaji wao, hata wamepelekea Zoezi la kuandikisha Wapiga Kura kutiliwa shaka na Wananchi walio wengi katika maeneo ambayo Uandikishaji unaendelea hivi sasa.

Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara, linalaani kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kushindwa kushughulikia/kudhibiti tatizo la foleni/misururu ya Wananchi kwenye Vituo vya kuandikisha Wapiga Kura katika maeneo mbalimbali Nchini.

Pia Baraza linaunga mkono uamuzi wa Wananchi wa Mkoani Kagera kuusimamisha njiani msafara wa Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa Dr.Willbroad Slaa aliyeko ziarani Mkoani humo na kumweleza jinsi Watendaji wa Tume hii ya Uchaguzi walivyoamua kuondoa Vifaa vya kuandikisha Wapiga Kura (BVR Kits) kwenye maeneo yao kabla ya kumalizika kwa muda (Siku 7) zilizopangwa na Tume.

Hata pia BAVICHA Serengeti,
inaungana na Kauli ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini (CHADEMA) ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.Joseph Mbilinyi maarufu kama 'Sugu' aliyoitoa Bungeni juzi kwamba Wananchi wasikubali kuondoshwa kwa Vifaa vya Uandikishaji (BVR Kits) kwenye maeneo yao kama bado kuna Wananchi ambao hawajaandikishwa hata kama Siku 7 za Tume zimemalizika.

Ndugu waandishi wa habari,
BAVICHA Serengeti inatoa Rai kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti wake Jaji Damiani Lubuva, kuhakikisha kwamba inaongeza Siku za kuandikisha Wapiga Kura kwa kutumia Mfumo huu wa BVR, kutokana na mfumo wenyewe kuwa na vikwazo vingi vinavyopoteza muda wa kuandikisha idadi kubwa ya Wananchi kwa kila Kituo.

Aidha BAVICHA Serengeti,
inatoa ushauri kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhakikisha kwamba, inatoa muongozo bora wa kuwapata Watendaji wa Zoezi hili wenye Sifa na Vigezo stahiki katika Halmashauri za Wilaya zilizobaki ili kuongeza ufanisi katika Uandikishaji na kupunguza baadhi ya changamoto na vikwazo ikiwemo kuwapata Watendaji wenye ujuzi wa Vifaa hivi vya Kielektroniki.

Aidha, BAVICHA Serengeti,
inamtaka Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi aache kufanya Kazi au majukumu yake kwa maelekezo ya Viongozi wa CCM, bali ajikite katika kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu matatizo yanayowakabiri Wananchi kutokana na mipango mibovu inayoratibiwa na Tume yake katika kuandikisha Wapiga Kura zaidi ya Millioni 30 Nchini.

Kutokana na Utendaji huu mbovu unaoratibiwa na Tume hivi sasa na kuendelea kusababisha madhara makubwa kwa Wananchi ikiwemo vifo na baadhi kulala nje Usiku kucha wakilinda foleni ya kuandikishwa kutokana na kasi ndogo ya Uandikishaji ikilinganishwa na Siku zilizotengwa na Tume kwa kila Kituo,

BAVICHA Serengeti,
tunamtaka Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Damian Lubuva ajiuzulu nafasi yake ya Uenyekiti ili ishikiliwe na Mtu mwingine atakayelivusha Taifa kutoka katika kipindi hiki kigumu, hii ni kutokana na jinsi ambavyo ameshindwa kusimamia misingi ya Tume anayoiongoza.

Ndugu waandishi wa habari,
BAVICHA Serengeti tunahitimisha kwa kuzipa pole familia za wale wote waliolipotiwa na vyombo vya habari kupoteza maisha yao wakiwa katika foleni/misururu ya kuandikishwa kwenye vituo vyao.

Aidha, tunawapa pole wale wote waliopatwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakiwa kwenye foleni za kuandikishwa kwenye Vituo mbalimbali Nchini, hata ikalazimu wengi wao kukimbizwa kwenye Vituo vya Afya na Hospitali.

Mwisho,
BAVICHA Serengeti tunawakumbusha Watanzania wote kuwa mwaka huu 2015 ni mwaka wa neema kwa wanyonge kufunguliwa pingu na minyororo ya mateso waliyodumu nayo kwa miaka zaidi ya 50 sasa.

Pia mwaka huu 2015, ni mwaka uliotabiliwa na waasisi wa Taifa hili juu ya Wananchi kukombolewa na kuwa na Sauti ya maamuzi ya mwisho dhidi ya watawala.

Njia pekee ni kujiandikisha na kujitokeza kupiga Kura kwa wagombea wote wa UKAWA Oktoba 2015.

Imetolewa na;

Francis Garatwa Muhingira,

Katibu BAVICHA,
Wilaya ya Serengeti.

Leo 27/05/2015.

Ahsanteni sana!

 
UKAWA tumaini la Watanzania October 2015.

CHADEMA,
Tulianza na Mungu,
Tutamaliza na Mungu.

Piiiiiipoooooooozzzzz.
 
Hii tume ni sawa na ile ya kiviutu ya kipindi kile kule kenya,hakika hakuna kosa kubwa kama kuacha wapiga kura kabla ya kuandikisha
 
Hii tume ni sawa na ile ya kiviutu ya kipindi kile kule kenya,hakika hakuna kosa kubwa kama kuacha wapiga kura kabla ya kuandikisha

Njia pekee ni KUKABANA nao KOO mpaka Kieleweke, hakuna kuondoka na Vifaa kabla Wapiga Kura kumalizika Vituoni
 
Wakuu, Mwaka huu wa Uchaguzi 2015, tutashuhudia mengi sana, ila mwisho wa Siku, UKAWA wataiongoza Nchi kwa Kura za kishindo.
 
UKAWA wataimaliza CCM kabla ya Saa 4:00 Siku ya Uchaguzi 25/10/2015. Mwanasheria wa CHADEMA "Mabere Marando" atatangaza Matokeo Saa 10:00 Jioni kabla ya Uchakachuaji wa CCM.
 
Hayo ndio matatizo ya kutokuwa na tume huru ya uchaguzi. UKAWA, harakati zenu kutaka tume
huru ziliishia wapi? Ona matokeo yake sasa, na bado!
 
Back
Top Bottom