Makete Njombe: Mwanafunzi achoma moto bweni la wavulana na kuteketea kila kitu

Nimejiweka kwenye nafasi ya mzazi wa huyo mtoto sasa ndio umepeleka kijana akasome anachoma moto bweni kama mshikaki. Ugumu wa malezi sio utani I see unaweza kujichukulia sheria mkononi tu
mwalimu alikosa busara kumtembezea kichapo angempa ushauri nasaha.
 
atasajiliwa Ufipa pale kuna kikundi cha utekaji kinachoongozwa na Alfred Lwakatare na Yericko Nyerere, ndio kimemteka Ben Saanane
Kwani ripoti ya uchungunzi ya Jeshi la polisi kuhusu kutekwa kwa Ben imeishatoka? Kama tayari mkuu tuwekee jamvini nasi tuisome.
 
Lazima kwa kweli hii ni bangi tu. Sasa wenzake wamekosa pa kuishi na afadhali walikuwa hawamo ndani angeweza kuua wenzake huyu mtoto hatari kabisa
Nadhani kalidhamiria kuchoma hivyo vitu vya wenzake,sas akajikuta kachoma bweni zima,sijui kalichomea ndani
 
Nimejiweka kwenye nafasi ya mzazi wa huyo mtoto sasa ndio umepeleka kijana akasome anachoma moto bweni kama mshikaki. Ugumu wa malezi sio utani I see unaweza kujichukulia sheria mkononi tu

angekuwa marekani halaf angepata acces ya bunduki angeua watu wengi sana inaonekana ni kisasi na hasira za kupigwa na walimu na wanafunzi wenzake
 
Njaa hiyo.

Lakini pia suala la viwango vya uwezo wa kulea watato kwa walimu linatakiwa liangaliwe upya. Walimu wa zamani walisoma education psychology seriously sana. Haya yanaweza kuwa ni mchango wa kudharau taaluma na kuanza kututpia tupia tu walimu wa vodafasta,ili mradi anajua somo analofundisha. Education as a subject is more than teaching.

Tumshukuru Mungu watoto wote wako salama.
Una maana walimu hawapatiwi mafunzo vyuoni?
Walimu wa vodafasta kwa sasa hakuna tena, walishajiendeleza. Na waliokuwa hawajaongeza elimu wameondolewa.

Hiyo punishment aliyotoa mwalimu yuko sahihi. Waliokosea ni hao wanafunzi wenzie waliompiga.

Huyo mtoto kuiba karanga na biskuti kweli ni njaa. Inawezekana chakula hakitoshelezi hapo shule. Hasa kipindi hiki cha elimu bure shule hazipati pesa za kutosheleza mahitaji yote.
Serikali inatoa elimu bure, ihakikishe na wanafunzi wanapata chakula bora na wanashiba, si kila siku kupika kande tu.

Tuna bahari, mito, maziwa na mbuga. Baadhi ya wanyama pori wanaozaliana sana mbugani au samaki kutoka kwenye mito na bahari wanaweza kuvunwa kwa mpango maalum na kusambazwa kwenye hizi shule za serikali watoto wale chakula bora.

Serikali ina la kujifunza kwenye jambo hili ambalo inaweza kuliona ni dogo lakina madhara yake ni makubwa. Mabweni mangapi tunasikia yanaungua moto kila mara, inawezeka vyanzo ni pamoja njaa kwa wanafunzi.
 
Back
Top Bottom