Mbeya: Mwalimu anayetuhumiwa kumshushia kipigo Mwanafunzi aliyedokoa maandazi ashikiliwa na Polisi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Kufuatia kuripotiwa kwa tukio la Laurence Nicholaus Mwangake, Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Rohila, Mbalizi kulazwa Hospitali ya Ifisi tangu Februari 12, 2023 ikidaiwa amejeruhiwa kwa kipigo, watuhumiwa wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano.

MWANAFUNZI_ALAZWA,_YADAIWA_NI_KIPIGO_CHA_WALIMU,_CHANZO_NI_KUDOKOA.jpg
Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya, Ernest Hinju anaelezea klichotokea:
"Taarifa zinaeleza Mwanafunzi alidokoa maandazi manne, walinzi wakamuona, wakamkamata na kumzuia kwenye chumba cha darasa wakiwa na Mwalimu aliyefahamika kwa jina la Petro Kamili, ambapo wakamdhibiti kwa kumfungia katika chumba hicho.

"Inaelezwa kuwa kitendo cha kudhibitiwa katika chumba huku Mwanafunzi akiwa na rekodi ya kuogopa kuchapwa, akaruka kwa nia ya kutoka kwenye darasa hilo kupitia dirishani, kitendo kilichosababisha apate majeraha kadhaa kwa kuwa kuna kioo ambacho kilimjeruhi.

"Baada ya tukio hilo kujulikana kwa Mkuu wa Shule, akaamua kumhoji mwanafunzi ambaye amedai kuwa alinyimwa chakula, hivyo wakati wa kulala akashindwa kuvumilia akaenda kudokoa maandazi hayo maandazi manne kwenye duka la Shule.

“Mkuu wa Shule akawasiliana na Polisi kwa hatua zinazofuata za kiusalama.
"Pia niweke sawa maelezo tuliyopata yanaeleza kuwa siyo Walimu wanne na walinzi wawili waliomshambulia mwanafunzi kama inavyosemwa, bali mhusika ni Mwalimu mmoja na mlinzi mmoja ambao hivi ninavyozungumza wanashikiliwa na Polisi tangu jana (Februari 14, 2023) kwa mahojiano.

“Sisi pia tunaendelea kufuatilia kwa kuwa Mwalimu anadai yeye hakumchapa bali Mwanafunzi alijirusha mwenyewe dirishani, hivyo muhimu kwa sasa ni kuangalia afya ya Mwanafunzi wakati uchunguzi unaendelea kwa kuwa Mwanafunzi anasema yake na Mwalimu anasema yake pia.”

RPC ANENA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Benjamin Kuzaga amesema: "Taarifa inaandaliwa kuhusu tukio hilo, ni kweli hilo suala lipo na wahusika wawili tunawashikilia ambao ni Mwalimu na Mlinzi, nitatoa taarifa kamili muda si mrefu."

=====
TAARIFA YA POLISI
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Sekondari Loiler iliyopo Mji Mdogo wa Mbalizi Mkoani Mbeya aitwaye Peter Emmanuel (29) Pamoja na Mlinzi wa Shule hiyo aitwaye Haruna Issa (30) Mkazi wa Iwala kwa tuhuma za kumshambulia kwa viboko sehemu mbalimbali za mwili mwanafunzi wa Shule hiyo wa kidato cha IV aitwaye RAULENCE NICHOLOUS (16) Mkazi wa Mwangake.

Ni kwamba mapema Februari 12, 2023 huko katika Shule ya Sekondari Loiler mwalimu huyo kwa kushirikiana na mlinzi wa Shule hiyo walimtuhumu mwanafunzi RAULENCE NICHOLOUS kuiba maandazi matano ambayo kila andazi ni Tshs. 300= hivyo jumla ya maandazi yote ni Tshs 1,500/= katika duka la shule hiyo na ndipo walimshambulia kwa viboko na kumsababishia majeraha sehemu ya paji la uso, mkono wa kushoto na magoti yote mawili.

Baada ya kumshambulia na kumjeruhi, siku hiyo yatukio majira ya saa 05:00 usiku walimkimbiza Hospitali Teule ya Ifisi kwa ajili ya matibabu. Jeshi la Polisi kupitia wasiri wake lilipata taarifa na kufanya ufuatiliaji na kubaini kutokea kwa tukio hilo na hatimaye kuwakamata watuhumiwa wote wawili.

Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada yakukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa jamii kuacha mara moja tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria.

Watuhumiwa watafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.

Imetolewa na,
BENJAMIN E. KUZAGA – ACP
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.

Pia Soma: Mbeya: Mwanafunzi alazwa baada ya kupata kipigo kutoka kwa Walimu wa Shule ya Sekondari Rohila, inadaiwa alidokoa maandazi manne
 
Kuna vita kubwa kati ya walimu na wanafunzi
Na wanaoleta hiyo vita ni wazazi wa kisasa na wanaharakati kutaka wanafunzi wasichapwe,mwanafunzi wa kileo yupo radhi afanye kosa hata la kujitakia akijua kuna mkuu wa mkoa atamtetea mama yake atamtetea even raisi wa nchi.

Tuliosoma 90s (huko nyuma sijui) tulikuwa na nidhamu kutokana na kwanza tulikuwa tukichapwa na walimu automatically ilijulikana mwalimu siyo mwendawazimu amchape mtoto bila sababu na mzazi anaitwa anakuchapa hadharani kwenye halaiki ya wanafunzi ili uwe mfano kwa wengine na hii ilitujengea nidhamu ya kutii taratibu za shule leo mtoto anajibizana na mwalimu akiadhibiwa kesho mwalimu anasimamishwa kazi,tutegemee watoto wetu kuwa na nidhamu mbovu hata huko majumbani mwetu kama tutatetea kila kitu.
 
Kwenye taifa la jeseon viboko havikamiliki mpaka damu ndo mana watu wanatii sheria hadi hivi leo. Kwetu Jeseon hata ukipigwa hadi kufa unafukiwa tuu ndo mana taifa linaakili. Nahamia kwetu kwa mtawala Baek dong so
 
Back
Top Bottom