idawa
JF-Expert Member
- Jan 20, 2012
- 25,284
- 38,312
Mwanafunzi mmoja anahisiwa kuchoma bweni la wanafunzi zaidi ya 140 na kuteketea kila kitu kwenye shule ya Sekondari Mang'oto iliyopo wilayani Makete mkoani Njombe.
Tukio hilo limetokea jana muda wa saa mbili usiku wakati wanafunzi wakiendelea kujisomea madarasani.
Chanzo inasemakana, Mwanafunzi huyo kabla alihisiwa juzi usiku tarehe 11/3/2018 alivamia kibanda cha mwalimu kilicho jirani na shule hiyo na kuiba baadhi vitu vikiwemo karanga na biskuti....
Jana asubuhi ndipo Mwalimu alipogundua kibanda chake kimebomolewa usiku, katika kufanya upelelezi ikaonekana huyo mwanafunzi usiku wa jana wenzie walimuona akila biskuti na karanga ambazo zilihisiwa moja kwa moja zilitoka kibandani humo.
Baada ya kupewa kibano na walimu mwanafunzi huyo akakiri kuwa ni kweli alihusika na uvamizi huo.
Baada ya kukiri hivyo inasemekana wanafunzi wengine walimpa kipigo kando na alichopewa na walimu.
Baada ya kupewa kipigo hicho,jana mchana inasemekana alishinda porini akipanga mipango yake ya kulipa kisasi kwa wanafunzi wenzie waliompiga.
Ndio akaja na wazo la kurudi usiku mida ya saa Mbili na kukusanya kila kitu cha wanafunzi waliochangia kumpiga akakusanya magodoro, daftari, vitabu na nguo zao na kuzipiga kiberiti.
Bahati mbaya ule moto ukashika ukuta, na kuunguza bweni lote na kila kitu kilichomo ndani.