KERO Makato ya Mkopo na kutorejeshewa fedha

KERO Makato ya Mkopo na kutorejeshewa fedha

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mahali pa Kazi: Wilaya ya Meru, Mkoa wa Arusha

Ninatoa malalamiko yangu hadharani dhidi ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kuhusiana na makato ya mkopo yaliyofanyika kimakosa na kutorejeshewa fedha hadi sasa.

Historia ya Masuala ya Elimu na Ajira:

Mwaka 2010, nilichaguliwa kujiunga na Mtwara Teachers College pamoja na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Kutokana na Mtwara Teachers College kutoa udahili mapema, niliamua kujiunga na chuo hicho cha ualimu.
Nilipojiunga na UDOM mwaka 2018, sikuomba mkopo, bali nilijisomesha mwenyewe.

Baada ya kuhitimu chuo cha ualimu Mtwara mwaka 2012, niliajiriwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru mwaka 2013.

Baada ya kumaliza masomo yangu ya chuo kikuu UDOM mwaka 2021, bado nimekumbwa na makato yasiyo halali kutoka HESLB.

Tatizo la Mkopo:
Kuanzia Oktoba 2021 hadi Aprili 2022, HESLB waliendelea kunikata fedha kimakosa, licha ya kunipatia Temporary Stop Deduction Letter.

Nilipofuatilia haki yangu ya kurejeshewa fedha, niliambiwa nitoe Permanent Stop Deduction Letter, wakati:
Makato yalikuwa tayari yamesimamishwa kwa muda.

Hakuna maelezo ya kisheria yanayoeleza kwanini fedha zilizokatwa kimakosa zishikwe hadi sasa.

Nimewasilisha malalamiko rasmi mara kadhaa, lakini sijapata majibu wala mrejesho wowote, jambo linalonitia hasara na kuninyima haki yangu ya msingi.

Naomba kwa heshima lakini kwa msisitizo:

Nirejeshewe fedha zote nilizokatwa kimakosa (Oktoba 2021 – Aprili 2022).

Nipatiwe majibu ya maandishi yenye msingi wa kisheria.

Haki ya wanufaika wa mikopo iheshimiwe na kulindwa.

Mawasiliano:
📧 anaeljkivuyo@gmail.com

Haki ikinyimwa kimya kimya, sauti ya umma huwa suluhisho.
 
Jamaa ni headache kwenye refund Mimi waliwahi kunikata mara Moja Wala sikufuatilia
 
Back
Top Bottom