Jul 13, 2021
5
4
MAKATO YA MIAMALA YA SIMU

Kwa kipindi cha hivi karibuni suala la makato ya simu limekua gumzo nchini na kuibua sitofaham na kauli za utata kutoka kwa baadhi ya viongozi, huenda walioanzisha tozo hizo hawakua na lengo baya ila naweza sema kwamba hawakufanya upembenuzi yakinifu pamoja na kumzingatia zaidi mwananchi ambae ndie mlengwa wa tozo hizo, viongozi wa Serikali wanasema hii ni kodi ya uzalendo lakini je ni kweli wao wametanguliza huo uzalendo?

Inasemekana kwamba wabunge wanapokea mamilioni ya pesa kama mshahara huku posho zao za kwenye vikao ni sawa na kima cha mshahara wa mfanyakazi wa kawaida kima hichi ni laki 2 hadi 2 na nusu kwa kila kikao haijalishi amechangia ama hajachangia hoja

Kubwa zaidi eti mbunge huyu ana bima anayolipiwa na Serikali ya familia yake hadi gari analotumia na kujaziwa mafuta bure na Serikali lita 100 kwa mwezi ama mwaka

Mbaya zaidi ni kwamba mbunge ama kiongozi huyu hakatwi kodi hata shilingi.

Hoja yangu ni kwamba kukatwa kodi ya uzalendo kwa kila mwananchi sio jambo baya ila ubaya unakuja kwamba gharama ni kubwa tangu mwanzo ila wananchi walinyamaza kimya kwakuwa iliyofanya hivyo ni kampuni binafsi ambazo zinapandisha gharama kila muda zijiskiapo, hivyo basi Serikali ilipaswa kufanya upambanuzi yakinifu wa kumpunguzia gharama kutoka katika mitandao hii ya simu kabla ya kuongeza kodi yao hii ingefanya kutokuonekana athari yeyote baada ya kuanzisha kodi yao.

Pili - Ikiwa kweli kuna kodi ya uzalendo tunahitaji kila kiongozi nae ahusike katika makato ya mshahara wake na kiongozi yeyote atakaeshindwa kutatua changamoto za watu wake walau kwa 60% alipe fidia kiinua mgongo chake baada ya kumaliza muhula wake kwa kula pesa za wananchi bure bila ya kuwatatulia shida zao hii ingeisaidia pia serikali yetu kwa kuhakikisha lile lengo la kufanya uchaguzi na vyama kuweka viongozi katika mikoa,kata na majimbo linafikiwa kwa 100%.

Tatu - Serikali ipunguze kodi kwa upendeleo zaidi kwa makampuni na wawekezaji wa ndani hii itavutia uwekezaji zaidi,italeta unafuu pia kwa wananchi ambao ndio watumiaji wa mwisho

Nne - Serikali ipunguze vat ikiwezekana iiondoe kabisa kusema kweli mimi hii sijaiona umuhimu wake zaidi ya kumuongezea gharama mwananchi ambae ndie mtumiaji wa mwisho, inawezekanaje kitu ununue leo kwa 1000 ila ukija kununua tena kitu kilekile kwa pesa ile ile uambiwe badala ya kizima unapewa nusu,hivi inaingia akilini hii?

Tano - Serikali ihakikishe inaziba mianya yote ya upotevu wa mapato na kuwachukulia hatua wote wale wanaohusika na wizi wa mali za umma washitakiwe na wazirudishe bila kuangaliwa mtu usoni wala kuonewa muhali kutokana na ukubwa wa cheo chake

Sita na mwisho kwa kumalizia ni lazima viongozi wetu wawe wabunifu kabla ya kuanzisha tozo mpya kwa wananchi ni lazima wahakikishe rasilimali zetu tulizonazo zinatumika kwa ufanisi na zinamneemeesha kila mwananchi bila ya ubaguzi na pia ni lazima kuondosha muhali miongoni mwetu,watambue kuwa kitendo chochote cha rushwa ni adui wa maendeleo yetu.

Mwisho na kwa msisitizo tunaomba watumie hekima viongozi wetu pale unapotokea mvutano baina yao na wananchi wawe na maneno matam pia kama kipindi kile cha uchaguzi,waswahili husema maneno matam yaweza hata kumponya mgonywa bila ya sindano wala ya dawa dozi.

Shukran
 
Back
Top Bottom