Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Maneno yakishindwa Weka Muziki

Habari za kutwa nzima ya leo Makapuku wenzangu. naamini kabisa tumekuwa na wakati mzuri jumatatu hii na sasa tunaenda kuikamilisha ili siku nyingine ianze. Ndiyo maisha, tunabadili tarehe tu na siku za juma zinabaki zilezile.

Nimekuwa na wakati mzuri leo, nashuku. Asante kwa wadau wote mnaopendezesha Jukwaa hili, wote kwa ujumla kwa michango tofauti tofauti, kuanzia wakati wa magazeti, sala, historia, UF, na chats za hapa na pale ilmradi tu kila mmoja anabaki kuwa na amani na forum hii.

Pole Bitoz kwa maumivu na ni habari njema kusikia unaendelea vizuri, hii ni kwa makapuku wote wanaougua na kuuguliwa.

lakini pia hongera kwa makapuku wote waliopata mishahara leo, waliokopa wakakopeshwa leo. Ni jambo zuri.
Sasa turudi kwenye ka-kipengele ka Muziki na hasa tukiangalia gitaa nami bila hiyana nakuletea kitu ambacho nachagua nikiamini kabisa utakipenda ukijipa muda wa kukisikiliza.

Leo tunaangalia 'country music'. Oh yeah, sauti nzito na gitaa la bass ndiyo tumeyazoea. Sitoangalia sauti nzito leo. Nitakusikilizisha sauti nzuri, tamu, mchanganyiko wa limau na sukari. Ndiyo, naamini unamjua ninayemleta kwako usiku huu, Dolly Parton.

Niandike nini ambacho hujawahi kukisikia kuhusu mwanadada huyu ambaye ni mmoja wa watu waliobahatika kuwa na uwezo wa kuimba na kupiga vyombo vingi vya muziki, gitaa likiwemo.

Ni mwanamke ambaye katika tasnia ya muziki anaweza kuwa katwaa tuzo nyingi sana kuzidi wanamuziki wengi maarufu unaowafahamu. Nyimbo zake zaidi ya 25 zilishika namba 1 katika chati za Billboard huko USA.

Hii ni mbali ya tuzo 9 za Grammy, 10 za Country na katajwa katika Academy mara mbili.

Kawa walivyo waimbaji wa country walio wengi, Dolly anajua kupiga gitaa. Nyimbo zake maarufu ni kama Jolene, The Coat of many colors, Pain of Loving You (ninaupenda huu). Love is like a butterfly.

Mtizame clip hii ya YouTube akicharaza gitaa kwa umahiri


Binamu asante
 
3/Greenland Shark
a45c8c081e3f22fc0bca0a30bedee8fb.jpg
beaf5ab453f981778459e1eca701e03c.jpg

Hawa ni papa wenye jeuri ya kuishi miaka 200 tena wana tabia ya kutafuna samaki wengine humo baharini
Yule mbishi zaidi kurekodiwa aliishi miaka 400
.......
Huo mdomo!!!
 
1/Immortal Jellyfish
aa83542fe281a589142e5e0e2367afb2.jpg
eea70345094e336074047e6fd80085e3.jpg
Tafsiri isiyo easmi ya immortal ni kuishi milele
Yaani Hawa samaki ni km vile huishi milele
Pindi wakijeruhiwa hujibadili na kurudi vilevile!!!
Kiufupi hawajui kufa kwa ugonjwa wala ajali labda wamezwe watafunwe
Hivyo ndo vinara wa kuishi miaka mwingi
..
.
.
.viumbe vya bahari ni ndo vinaongozi kwa kuishi miaka mwingi
Hii inadhihirisha Maji ni Uhai
Shukrani kwa mliosapoti mada
Tukutane kesho
Mwisho
..........
 
Pale penye kibao hicho ni pale darajani panaitwa mpakani,hapo ndipo alipofia marehemu aliyekua mwenyekiti wa FAT WA MKOA MBEYA MIAKA YA NYUMA SASA HV TFF...KWA AJALI YA GARI BUS SCANDNAVIA ENZI HIZO,SIKUMBUKI MWAKA..RIP
Asante kwa ufafaunuzi dada na pale panaonekana pana matuta makubwa na daraja


RIP Mwenye kiti wa FAT
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom