Makapuku Forum

Makapuku Forum

Picha ya mshale Tafadhali
0d35a36d6966bb04c5a8ca5669edf41d.jpg
 
ZABURI 91

5.Hutaogopa hofu ya usiku,wala mshale urukao mchana.

TUOMBE

Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi,asante sana kwa ulinzi mchana kutwa,tunaomba toba kwa yote tuliyokosea kwa mawazo maneno na matendo,uturehemu twakusihi.
tunajikabidhi mikononi mwako usiku wa leo tuepushe na hatari na ajali mbalimbali,tusigope hofu za usiku maana upo pamoja nasi usiku wa leo unatukumbatia,asante kwa kuwa utatupa kushinda.
Nakuomba uwaponye wagonjwa wote majumbani na hospitali zote nyoosha mkono wako kwa mpendwa wetu Bitoz BABA damu ya Yesu inene mema,apate uponyaji wa haraka na asipungukiwe.
Angalia wajane,yatima wape faraja kuu.
Malaika walinzi wazunguke vitanda vyetu kutulinda
Wabariki wasafiri wafike salama.
Asante Baba kwakuwa utatenda sawa na mapenzi yako ,tunaomba na kushukuru Amen
USIKU MWEMA MBARIKIWE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom