Makapuku Forum

Makapuku Forum

4/Curtis James Jackson III
7d4dd499f684e7108ae2a940f81948a6.jpg
dcadebd80d30fba9412538ef84fcc37e.jpg
801c59acd497cc7c177e8eba440a8c60.jpg
Nani asiyemfahamu huyu Mswahili?
Anajiita 50 Cent ana umri wa miaka 38
Utotoni alikulia katika umaskini uliotopea ikiwemo kulelewa na bibi yake.
Anewahi kutandikwa risasi lakini akapona.
Ana dili kibao za kuvutia mpunga
Ana utajiri wa USD 240 Milioni
.......
 
Furahiday; Muziki, Kula, Kunywa na Kufurahika.

Ni siku nzuri katika wiki, wengine huifanya kuwa nusu siku na wingine japo ni siku kama siku nyingine lakini hii ni Furahiday.

Tunafunga kazi, tunafunga ripoti, tunakusanya assignment na kupanga plans za kufanya tunapopumzika. Katika kufanya mipango, nami nina mipango yangu ambayo haiwezi kuwa na sawa na yako. Ila tukikutana hapa mida hii unaujua kabisa mpango ninaouleta hapa, muziki. Na hasa sauti ya gitaa katika muziki.

Kizuri zaidi mdau Sweetiepie kaahidi kuanza kuporomosha nyimbo siku za wikend ikihusisha mwisho wa mwisho wa wiki. Tusubiri.

Jioni hii hebu tubakie hapa hapa Afrika na kuwatizama wapigaji gitaa maarufu wa miziki ya bendi na hata 'binafsi'. Na tunamwangalia gwiji kweli kweli aliyekubalika na wote waongea kiingereza, kifaransa, kiswahili na ligha nyingine nyingi za kiafrika. Huyu ni Francois Luambo Luanzo Makiadi almaarufu Franco.

Kwa tuliokuwa tunakuwa miaka ya 90 tunakumbuka namna nyimbo za gwiji huyu zilivyotawala vituo vya radio nchini. wimbo wa Mario kwa mfano, ulikuwa na sifa kubwa hapa nchini kama ilivyo kwa karibu ukanda wote wa kusini mwa Afrika.

Franco anajulikana pia kwa kuwa na nyimbo ndefu sana, wimbo Kimpa Kisangameni unapanda mwendo kasi toka Masasi kwenda Lindi na ukifika Mnazi Mmmoja ndo kwanza korasi ya kwanza ndo inaishi na wimbo unakorasi zinazofuatana, Kulwa, Dotto na Shija.

Alitoa album zaidi ya 150 na nyimbo alizotunga yeye ziko kama 1000+. Huyu ndiye Franco rafiki wa iliyokuwa Zaire ya Mobutu.

Alifariki mwaka 1989 na serikali ilitangaza siku nne za maombolezo huku kituo cha redio ya taifa kikipiga nyimbo zake asubuhi hadi jioni.

Hapa tumwangalie na wimbo wake Mario, mwingine aliyeimba nanye ni almaarufu Madillu System, lakini kikubwa sikiza alivyokuwa akidonoa gitaa lake kwa mtindo wa Afro-Cuban , kupanda na kushuka kwa tone ya nyuzi.

Wikend Njema Makapuku

Bandiko zuri changamshi as usual. Wengi hudhani kwamba Mamou pengine ndiyo wimbo wake bora kabisa kisanaa. Vocals zake na Madilu wakijibizana zinaweza kukutia simanzi na kukusisimua hata kama hujui kinachoimbwa. Mwanafunzi mmoja wa Musicology alikuwa anadai hivyo katika tasnifu yake ya Masters katika Chuo Kikuu kimoja huko Ujerumani. Nilishindwa kufuatilia hoja zake za kitaalamu kwa sababu sijui cho chote kuhusu taaluma ya muziki.
 
Mjengo ulikuwa wa Tyson huo na alipofulia ndiyo huyu dogo akaununua. Shida ya hawa ni kwamba wengi wao wana matumizi mabovu na wana madeni ya kutisha. Kuna siri nyingi katika utajiri wao huu ndiyo maana wengi wana matatizo ya kodi kwa sababu huwa wanaogopa ku-file tax returns wakiogopa utajiri wao halisi kujulikana. Sababu hii hii ndiyo inamfanya Trump agome kabisa kutoa makaratasi yake ya kodi. Ni tajiri lakini wengi wanaamini kuwa siyo tajiri kama anavyojigamba. All in all they did good!
 
Msaada kwa mtu mwenye shida, hata kama uwe mdogo namna gani, unaweza kuleta furaha ya kweli na hata kubadilisha mtazamo wa maisha yake. Tujenge tabia ya kuwasaidia wenzetu wasio na kitu na kuwafariji wagonjwa wanaoteseka huko mahospitalini. Huu ndiyo dini ya kweli!
84c83dd694f97c38efa1a611ef23d79f.jpg
Sinaga tabia ya kurundika vitu
Kila mwaka naelekea kijijini kwetu huko lazima niwaachie nguo,viatu n.k
Samtaimu naweza nikaendana sendo pea moja na vaitu pea moja tu hapo lazima niwaachie ama sendo au vitu
Kijijini kuna dhiki balaa wapo ambao kuvaa chupi tu ni anasa
Umeandika naneno mazito sana
....
 
Bandiko zuri changamshi as usual. Wengi hudhani kwamba Mamou pengine ndiyo wimbo wake bora kabisa kisanaa. Vocals zake na Madilu wakijibizana zinaweza kukutia simanzi na kukusisimua hata kama hujui kinachoimbwa. Mwanafunzi mmoja wa Musicology alikuwa anadai hivyo katika tasnifu yake ya Masters katika Chuo Kikuu kimoja huko Ujerumani. Nilishindwa kufuatilia hoja zake za kitaalamu kwa sababu sijui cho chote kuhusu taaluma ya muziki.

Sure, tunawaita waimbaji huru hawa, haina kutengeneza sauti, ni sauti yake halisi aliyoitunza vizuri. Franco, yapo maandishi yanasema japo alitoka katika maisha ya kawaida , baadaye muziki wake aliuchepusha na kufuata mambo ya matajiri, akiimba kuhusu 'cheating' (kuchepuka, right?) na mambo ya anasa anasa tu.
Yote kwa yote, jamaa alikuwa mkali na alijua kulipiga gitaa
 
Sinaga tabia ya kurundika vitu
Kila mwaka naelekea kijijini kwetu huko lazima niwaachie nguo,viatu n.k
Samtaimu naweza nikaendana sendo pea moja na vaitu pea moja tu hapo lazima niwaachie ama sendo au vitu
Kijijini kuna dhiki balaa wapo ambao kuvaa chupi tu ni anasa
Umeandika naneno mazito sana
....
Asante Madenge. Ni rahisi sana kujisahau. Ndiyo maana wengine hata huko vijijini walikotoka hawapakumbuki tena. Wanasubiri mpaka wafe ndo wapelekwe wakiwe kwenye masanduku ya bei mbaya.
 
Sisi ukoo mzima tuna utamaduni wa kukutana kijijini kwetu pamoja tukiwa na wanafamilia kila mwishoni au mwanzoni mwa kila mwaka
Hata sherehe zetu za harusi ni palepale kwa babu zetu hata uwe Profesa na hela zako
Ndo utaratibu tuliojiwekea
.........
 
Sure, tunawaita waimbaji huru hawa, haina kutengeneza sauti, ni sauti yake halisi aliyoitunza vizuri. Franco, yapo maandishi yanasema japo alitoka katika maisha ya kawaida , baadaye muziki wake aliuchepusha na kufuata mambo ya matajiri, akiimba kuhusu 'cheating' (kuchepuka, right?) na mambo ya anasa anasa tu.
Yote kwa yote, jamaa alikuwa mkali na alijua kulipiga gitaa
bhinamuuuu
 
Furahiday; Muziki, Kula, Kunywa na Kufurahika.

Ni siku nzuri katika wiki, wengine huifanya kuwa nusu siku na wingine japo ni siku kama siku nyingine lakini hii ni Furahiday.

Tunafunga kazi, tunafunga ripoti, tunakusanya assignment na kupanga plans za kufanya tunapopumzika. Katika kufanya mipango, nami nina mipango yangu ambayo haiwezi kuwa na sawa na yako. Ila tukikutana hapa mida hii unaujua kabisa mpango ninaouleta hapa, muziki. Na hasa sauti ya gitaa katika muziki.

Kizuri zaidi mdau Sweetiepie kaahidi kuanza kuporomosha nyimbo siku za wikend ikihusisha mwisho wa mwisho wa wiki. Tusubiri.

Jioni hii hebu tubakie hapa hapa Afrika na kuwatizama wapigaji gitaa maarufu wa miziki ya bendi na hata 'binafsi'. Na tunamwangalia gwiji kweli kweli aliyekubalika na wote waongea kiingereza, kifaransa, kiswahili na ligha nyingine nyingi za kiafrika. Huyu ni Francois Luambo Luanzo Makiadi almaarufu Franco.

Kwa tuliokuwa tunakuwa miaka ya 90 tunakumbuka namna nyimbo za gwiji huyu zilivyotawala vituo vya radio nchini. wimbo wa Mario kwa mfano, ulikuwa na sifa kubwa hapa nchini kama ilivyo kwa karibu ukanda wote wa kusini mwa Afrika.

Franco anajulikana pia kwa kuwa na nyimbo ndefu sana, wimbo Kimpa Kisangameni unapanda mwendo kasi toka Masasi kwenda Lindi na ukifika Mnazi Mmmoja ndo kwanza korasi ya kwanza ndo inaishi na wimbo unakorasi zinazofuatana, Kulwa, Dotto na Shija.

Alitoa album zaidi ya 150 na nyimbo alizotunga yeye ziko kama 1000+. Huyu ndiye Franco rafiki wa iliyokuwa Zaire ya Mobutu.

Alifariki mwaka 1989 na serikali ilitangaza siku nne za maombolezo huku kituo cha redio ya taifa kikipiga nyimbo zake asubuhi hadi jioni.

Hapa tumwangalie na wimbo wake Mario, mwingine aliyeimba nanye ni almaarufu Madillu System, lakini kikubwa sikiza alivyokuwa akidonoa gitaa lake kwa mtindo wa Afro-Cuban , kupanda na kushuka kwa tone ya nyuzi.

Wikend Njema Makapuku

Namkubali sana huyu Mzee japo sijafanikiwa kuishi zama zake. Kuna kibao chake aliimba kwa Kiswahili na Sam Mangwana pia nakikubali mno.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom