Makapuku Forum

cc: demi

Sent from my HUAWEI Y300-0100 using JamiiForums mobile app
 
Siku hizi hasikiki sana
 
5/Bryan Williams
Ana umri wa miaka 45
Anajulikana zaidi kama Birdman
Huyu anavuta mkwanja kutokana na mikataba yake minono aliyosaidi mfano Cash Money ,pia ana biashara kibao pamoja na majumba ya jifahari
Ana utajiri wa USD 230 milioni
.......
 
Furahiday; Muziki, Kula, Kunywa na Kufurahika.

Ni siku nzuri katika wiki, wengine huifanya kuwa nusu siku na wingine japo ni siku kama siku nyingine lakini hii ni Furahiday.

Tunafunga kazi, tunafunga ripoti, tunakusanya assignment na kupanga plans za kufanya tunapopumzika. Katika kufanya mipango, nami nina mipango yangu ambayo haiwezi kuwa na sawa na yako. Ila tukikutana hapa mida hii unaujua kabisa mpango ninaouleta hapa, muziki. Na hasa sauti ya gitaa katika muziki.

Kizuri zaidi mdau Sweetiepie kaahidi kuanza kuporomosha nyimbo siku za wikend ikihusisha mwisho wa mwisho wa wiki. Tusubiri.

Jioni hii hebu tubakie hapa hapa Afrika na kuwatizama wapigaji gitaa maarufu wa miziki ya bendi na hata 'binafsi'. Na tunamwangalia gwiji kweli kweli aliyekubalika na wote waongea kiingereza, kifaransa, kiswahili na ligha nyingine nyingi za kiafrika. Huyu ni Francois Luambo Luanzo Makiadi almaarufu Franco.

Kwa tuliokuwa tunakuwa miaka ya 90 tunakumbuka namna nyimbo za gwiji huyu zilivyotawala vituo vya radio nchini. wimbo wa Mario kwa mfano, ulikuwa na sifa kubwa hapa nchini kama ilivyo kwa karibu ukanda wote wa kusini mwa Afrika.

Franco anajulikana pia kwa kuwa na nyimbo ndefu sana, wimbo Kimpa Kisangameni unapanda mwendo kasi toka Masasi kwenda Lindi na ukifika Mnazi Mmmoja ndo kwanza korasi ya kwanza ndo inaishi na wimbo unakorasi zinazofuatana, Kulwa, Dotto na Shija.

Alitoa album zaidi ya 150 na nyimbo alizotunga yeye ziko kama 1000+. Huyu ndiye Franco rafiki wa iliyokuwa Zaire ya Mobutu.

Alifariki mwaka 1989 na serikali ilitangaza siku nne za maombolezo huku kituo cha redio ya taifa kikipiga nyimbo zake asubuhi hadi jioni.

Hapa tumwangalie na wimbo wake Mario, mwingine aliyeimba nanye ni almaarufu Madillu System, lakini kikubwa sikiza alivyokuwa akidonoa gitaa lake kwa mtindo wa Afro-Cuban , kupanda na kushuka kwa tone ya nyuzi.

Wikend Njema Makapuku

 
Utakuta mtu unatunza nguo za zaidi ya mika mitano iliyopita, huwezi kuzigawa (endapo zipo kwenye hali nzuri), stoo limejaa makorokoro ambayo huyatumii iwe ni viti, radio, magodoro, mashuka, viatu, masufuria, na mazagazaga kibao)
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…