Makapuku Forum

 
Mkuu hii wiki ya kesho ni nzito sana ila Mungu atutie nguvu
 
Nashindwa niandike nini kuhusu msiba mkubwa uliotokea huko Karatu, kila ninapotaka kuandika ninafuta, macho yanalengwa na machozi na kuvifanya vidole visitii ninachotaka kuandika. Ni huzuni kubwa kwa wazazi, walezi, familia, shule na Taifa kwa ujumla.

Wakati tunajiandaa kuwapumzisha wanafunzi, walimu nawatumishi wa basi lililowabeba, tuburudike na wimbo huu wa tenzi za rohoni 'Karibu na Wewe' au kwa kiinglish 'Nearer My God to Thee'.

Wimbo huu ulipigwa na bendi iliyokuwa ikitumbuiza katika meli ya Titanic hata wakati inazama kabisa. wapigaji wa vyombo waliendelea kupiga hata pale maji yalipokuwa yamewafikia shingoni..

Nitaziweka kadhaa ambazo nimepata link ya YouTube.

Msiba huu ni wetu wote, tunaumia na hasa ukizingatia wapo wana JF kama PakaJimmy BlessedHope ambao wamepoteza watotot wao wa karibu na wengine wengi ambao msiba huu umetugusa kwa namna tofauti



 
It's a miracle
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…