Makapuku Forum

Francesc " Cesc " Fabregas - Namba 4

Kiungo huyu matata ni mpenzi wa jezi namba 4 kutokana na sababu kuu mbili.
Moja, Ni tarehe yake ya kuzaliwa.
Mbili, Ni jezi iliyokuwa inavaliwa na Pep guardiola ambaye amemtaja kama role model wake.

Arsenal


Barcelona


Chelsea


Fabregas kwa timu ya taifa ya Hispania, amekuwa akivaa jezi namba 10.
 
Andrea Pirlo - Namba 21

Pirlo amekuwa muumini mzuri wa namba 21 kwasababu ni tarehe ya kuzaliwa kwa baba yake mzazi.

New York Fc


Ac Milan


Juventus


Italy
Kweli,amedhihirisha hili,safi sana. Kuna watu ukiwauliza tarehe za kuzaliwa wazazi wao hawazijui wala hawajawahi uliza...tuwaenzi wazazi. Nimeipenda hii ya Pirlo
 
Xabi Alonso - Namba 14

Kiungo mkabaji huyu amekuwa ni muumini mzuri wa namba 14 kwa heshima ya gwiji wa zamani wa Uholanzi Yohan Cruyff aliyekuwa anavaa jezi namba 14.

Liverpool


Hispania


Real Madrid
Alonso alianza na namba 22 akiwa Madrid kabla ya kupewa namba yake pendwa.


Bayern Munich
Akiwa Bayern alianza na namba 3 kabla ya msimu uliofatia kupewa namba yake pendwa 14.


 
Good
 
Mario Balotelli - Namba 45

Straika Mario Balotelli amekuwa akivaa jezi namba 45 ambapo sababu kuu ni kuwa 4 +5 = 9.
Hivyo anapokuwa anavaa namba 45 ni sawa amevaa namba 9.

Pia alipovaa namba 45 kwa mara ya kwanza akiwa Inter Milan alifunga mechi nne mfululizo hivyo akaamua aendelee na namba hiyo.

Inter Milan


Ac Milan


Man City


Liverpool
 
Pia kuna mambo mengine ya namba yako kiroho kama unaamini hawa na wengine wanaamini,wengine mambo ya nyota hawawezi yasema
 
nilikua namsubili kwa hamu napenda sana vituko vyake
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…