Makapuku Forum

Makapuku Forum

IMG-20170429-WA0023.jpg
 
Wanasiasa wanatakiwa kujua kusoma na kuandika tu matokeo yake hawajui kuhesabu wakiandikiwa kwenye mikataba ISD 123 wanafikiri ni Tsh 1230
shukrani kwa magazeti

.
SHIMBA jana ndondi nani kupigwa?
.........
Pambano ni leo Jumamosi usiku saa nne huko UK. Huku kwetu itakuwa saa saba usiku J'pili.

Wanasiasa hao hata hesabu wanazijua sana. Tatizo ni vijisenti. Jamaa wanapiga hela ndefu sana (in US $) halafu wanakwenda kuziweka nje zinapoa kwanza. Imagine mzee wa vijisenti alivuta US $ milioni 3+ kwenye rada halafu anasema tena kwa kiburi na dharau kabisa kuwa hivyo ni vijisenti tu. Nchi hii ina walaji tena wenye meno ya chuma!
 
Amen asante Mungu kwa upendo wako,umetulinda na kutuamsha salama tembea nasi siku yaleo bariki kazi za mikono yetu bariki tuingiapo na tutokapo,tujaze upendo,furaha ,mshikamano tuchukuliane mizigo,ponya majeraha,ponya wagonjwa,fariji wafiwa ,wajane,wahitaji tutendee sawa na mapenzi yako tunaomba na kushukuru katika jina la Yesu Amen
Amen Mama.
 
Pambano ni leo Jumamosi usiku saa nne huko UK. Huku kwetu itakuwa saa saba usiku J'pili.

Wanasiasa hao hata hesabu wanazijua sana. Tatizo ni vijisenti. Jamaa wanapiga hela ndefu sana (in US $) halafu wanakwenda kuziweka nje zinapoa kwanza. Imagine mzee wa vijisenti alivuta US $ milioni 3+ kwenye rada halafu anasema tena kwa kiburi na dharau kabisa kuwa hivyo ni vijisenti tu. Nchi hii ina walaji tena wenye meno ya chuma!
Usisahau kutupa update

Acha wivu hiyo ni pesa ya mboga tu
By Tobaijuka
......
 

shululu asante sana kwa magazeti.

Salamu Makapuku, na baada ya kuwasabahi, nina swali dogo tu wala si la maana kivile wikend hii.

Hivi vyeti feki (ndo maana nimenukuu hili gazeti ) ni vipi? Siasa kando. Nataka kujua hivi vyeti feki ni vipi?

Hawa 9k wenye vyeti 'feki' ni rahisi tu kuwaondoa kazini usizoroteshe huduma za kijamii? (Haimaanishi kuwa nakubaliana na forgery/fraud ya aina yoyote).

Natamani tungekuwa tunavipa vichwa vyetu kazi yake, kufikiri, kabla ya kuibuka na dhana kama hizi za vyeti feki , hii itasaidia kuwa na sehemu moja ya kusimamia, fairness to both, na sio 'kunywa supu ya mbwa na kuilaani nyama yake'.

Baada ya kauli ya waziri, naliona zoezi hili kutokuwa fair, sababu ya ndimi mbili aka dabostandard. Unapomuhukumu mwizi usimwache aliyeibiwa
 
Asante sana mkuu. Maisha yetu hapa duniani kweli ni kama maua. Juzi nimeongea na schoolmate wangu mmoja akaniambia ana homa homa inamsumbua just now hata sijaamka vizuri napigiwa simu kuwa katangulia mbele ya haki. Jamaa mchacharikaji ndiyo tu kamaliza kushusha mjengo wa kufa mtu huku akiwa tayari sasa kuanza kutafuta mwenza. Just 29 yrs old huyooo tayari keshatangulia.

Tufurahieni maisha hapa duniani lakini kamwe tusisahau kuwa tu wapitaji tu na harakati za kujitafutia mali na raha zingine zisitufumbe macho mpaka tukasahau hata kumkumbuka Mungu katika maisha yetu. Tukumbuke kuwasaidia binadamu wenzetu wanaoteswa na magonjwa na umasikini. Tuwatembelee mayatima. Tuwaliwaze wenye matatizo. Tuwe wanyenyekevu na zaidi ya yote tujiweke tayari kila siku ili tunapojikabidhi mbele yake Aliyetuumba tukawe na kibali machoni mwake kwa kadri ya Neema zake na upande wake kwetu. Muwe na siku njema makapuku.

Miye kuna dentist kakorofisha jino langu yaani linauma kuliko hata kabla sijaenda kwake. Jino lilikuwa na tobo (cavity) kaliziba sasa ananiambia eti si ajabu nikahitaji root canal. Hovyo kabisa. Leo naona nitashinda tu nimelala nikilisikilizia. Mniombee!
edfdb22be69e4f655595f6f071b7ba5f.jpg
Dah!!!.....pole kwa msiba wa schoolmate, ndio hivyo binadamu hatujui kesho yetu, muhimu kumtafuta Mungu muda wote maana hatujui siku wala saa.....pole pia kwa jino.....lifanyie rootcanal au uling'oe kabisa maana hamna option nyingine.....usilisikilizie!!!
 
Bashiteeee kapona
Ni uonevu tu. Hebu nije nisikie tena mtu anasema eti nobody is above the law. Nitaua mtu! Labda huko kwa wenzetu ambako hata kama we ni rais ukileta za kuleta unaburuzwa mahakamani na hata kufurushwa kutoka madarakani. Juzi juzi tu hapa rais wa Korea Kusini kafurushwa kama mwizi. Mwaka jana rais wa Brazil naye yakamkuta. JK sitamsahau kwa kugeuza gia angani na kugoma kutuachia katiba mpya. Angetuachia katiba mpya yaani angekuwa legend wa siasa za Tanzania!
68eb96e636764fc930c865d5b315d86a.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom