Makapuku Forum

Yanga ya mwaka 1993 iliyoshiriki Kombe la Chalenji huko Kampala ilikuwa na Edward Edibily Jonas Lunyamila ambapo alikuwa gumzo sana unaambiwa magari ya huko mengi yaliandikwa Jina la staa huyo baada ya kumfunika staa wa kiganda Majid Musisi.

Yanga ilikuwa na akina Keneth Mkapa, Said Mwamba Kizota na mastaa wengineo.
 
Hiki kikosi sijawahi kukishuhudia kikicheza
Zaidi nasikia tu simulizi japo nimewahi kuwashuhudia baadhi tu hasa Kizota na Lunyamila
.....
 
Historia kuntu kabisa, Asante musollin
 
Chini ya kocha Rauli Shungu
 
yanga hii nahisi ndio iliimbwa na Pepe kale
Hiki kikosi sijawahi kukishuhudia kikicheza
Zaidi nasikia tu simulizi japo nimewahi kuwashuhudia baadhi tu hasa Kizota na Lunyamila
.....
 
Majid Mussisi. SC Villa

Jackson Mayanja. Express

Wawe timu ya taifa beki no 2au 3 kazi unayo
 
Hiki kikosi sijawahi kukishuhudia kikicheza
Zaidi nasikia tu simulizi japo nimewahi kuwashuhudia baadhi tu hasa Kizota na Lunyamila
.....
Nimekisikia tu, huyo Constantine Kimanda alikuwa ni Mkongomani, unaambiwa ni beki wa kati wa aina yake.

Said Nassoro Mwamba Kizota enzi hizoakicheza kama Straika, baada ya kasi kupungua akarudi kucheza Sentahafu ambapo hapo ndipo alipopewa jina la Kizota kutokana na aina yake ubabe na undava hali iliyofanya kuogopwa sana na Washambuliaji wengi.

Ikumbukwe Said Mwamba Kizota alipewa jina hilo la Kizota kama utani kutokana na eneo la Kizota lililopo Dodoma ambalo lilikuwa linaogopwa na viongozi wengi waliokuwa wanafanua makosa enzi ya utawala wa Jk Nyerere kwani hapo ndipo ofisi za chama zilipokuwa hivyo ukifanya kosa unaitwa Kizota mjini Dodoma ili uhukumiwe.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…