Makapuku Forum

1941 - Bobby Moore anazaliwa.

Beki na kepteni wa zamani wa West Ham na timu ya taifa ya England.

Ndio kepteni pekee wa England kubeba kombe la Dunia walipofanya hivyo mwaka 1966 katika mashindano yaliyofanyika kwao Uingereza.

Ndio kepteni mdogo zaidi katika historia ya Soka la Uingereza baada ya kupewa Unahodha akiwa na miaka 22 tu.

Alifariki Dunia mwaka 1993, kwa heshima yake Jezi namba 6 haivaliwi tena kwenye klabu ya West Ham.

Waingereza wamejenga sanamu yake nje ya Uwanja wa Wembley kama njia ya kumuenzi.
 
1948 - Marcelo Lippi anazaliwa.

Kocha wa zamani wa Juventus, Inter Milan, Napoli, timu ya taifa ya Italy na sasa timu ya taifa ya China.

Ndio Kocha aliyewapa Italy Kombe la Dunia la Mwaka 2006 katika mashindano yaliyofanyika Ujerumani ambapo Fainali Italy anamfunga Ufaransa kwa matuta.
 
1969 - Lucas Radebe anazaliwa.

Beki wa kati wa zamani wa Kaizer Chiefs, Leeds United na timu ya taifa ya Afrika Kusini.

Ni wakati alipokuwa Leeds United iliyokuwa inashiriki EPL, Radebe alijitengenezea Jina kubwa katika Dunia ya mpira.

Alichaguliwa kuwa kepteni wa Leeds United na kumfanya kuwa Mwafrika wa kwanza kuwa nahodha katika timu ya ligi kuu Uingereza. Alikuwepo kwenye kikosi kilichofika nusu fainali ya Uefa Champions League mwaka 2001 akiwa na akina Rio Ferdinand, Alan Smith, Mark Viduka, Harry Kewell nk

Alitwaa ubingwa wa mataifa ya Afrika mwaka 1996 katika ardhi ya Nyumbani.
 
Milele aminaa
 
Ubingwa wenyewe wa mbeleko....watachukua tena siku wakiwa wenyeji
....
 
Ujumbe mzur

Uwe na siku njema
Cc:mshauri
 
Nakumbuka zaidi tukio la Zidane kumtwanga kichwa Materazzi na kupigwa RED CARD
Italy ilishinda kwa penalties
....
 
1984 - Edward Sokoine anafariki Dunia katika Ajali ya gari huko Dumila, Mkoani Morogoro.

Leo ni miaka 33 tokea kifo chake.

Alikuwa ni Waziri Mkuu wa Tanzania mara mbili, kipenzi cha Wanyonge na watanzania wengi.
Vita yake dhidi ya Uhujumu Uchumi ilipamba moto kiasi cha kufanya walanguzi kumuogopa vibaya.

Alifariki baada ya gari alilopanda kupata ajali ya kugongwa na gari la Mkimbizi wa Afrika Kusini aliyejulikana kama Dumisane Dube.

Alitajwa kama mtu ambaye angemrithi Nyerere kwenye Urais mwaka mmoja baadae 1985 mara baada ya Nyerere kutangaza kung'atuka.

Ajali yake mpaka leo imebaki kuwa na utata wa hali ya juu.

Chuo Kikuu cha Kilimo na Ufugaji mjini Morogoro, Sokoine University of Agriculture ( SUA ) , kimepewa jina lake kama kumuenzi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…