1980 - Ronaldinho Gaucho anazaliwa.
Jina lake halisi ni Ronaldo De Assis Moreira.
Kiungo mshambuliaji wa zamani wa PSG, Ac Milan, Barcelona na timu ya taifa ya Brazil.
Anatajwa kama mmoja wa wachezaji bora wa wakati wote kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka.
Ameshinda kila kitu katika soka, Kuanzia Copa America mwaka 1999, Kombe la Dunia mwaka 2002, Uefa Champions League mwaka 2006, ubingwa wa La Liga mara mbili.
Pia ameshinda Ballon D'or mara mbili.
Alisifika kwa chenga zake za madaha, uwezo wa kukokota mpra na hata magoli adimu.
Mpinzani wake mkuu wakati anacheza alikuwa Zinedine Zidane wa Ufaransa, mpaka leo hakuna jibu sahihi kati ya Zidane na Ronaldinho nani alikuwa zaidi?