2009 - Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ( ICC ) yatoa hati kukamatwa kwa Rais wa Sudan Omar al Bashir kwa makosa yake ya Uhalifu dhidi ya Binadamu huko katika jimbo la Darfur.
Hati hiyo inamfanya Rais Bashir kuwa Rais wa kwanza aliyepo madarakani kutafutwa na Mahakama hiyo toka kuanzishwa kwake.
Lakini mpaka leo miaka 8 baadae, Omar Al Bashir hajakamatwa.