Makapuku Forum

Makapuku Forum

3cf0707fdb6f949fa175631da0c38833.jpg



Kapuku ,

Ukiachana na akili za Mzee Wenger basi kingine kinachoiangusha arsenal ni kile kinachoibeba Bayern Munich..... Tofauti hapa ni creativity ya players on field, team work inapofeli basi unakuwa ni muda wa kupambana na ubunifu na individual skills kwaajili ya timu..... Hapa mpaka dk 90 arsenal walikuwa watiifu Bila ya ubunifu, Bila ya individual skills na Bila ya plan B ya mwalimu na kila kitu wakawaachia Bayern wafanye wao tu.

Mesut Mustapha Ozil huyu jamaa michezo mikubwa imekuwa ikimshinda mara kwa mara, na hata huu kabla ya kuanza Kila mtu ata arsen wenger alifahamu kuwa mchezo huu utaanza kumshinda Ozil kwanza...... Sababu hiyo tu ya Ozil na michezo mikubwa ndio mzee wetu angeitumia kuanza na Dany Welback katika nafasi ya Ozil sababu Ozil anaposhindwa kuchezesha timu huwa ni ngumu yeye kukaba..... Kwa maana kuwa Dany Welback anakupa opts ya kukaba wakati timu haina mpira ila pia kuforce wakati wa kushambulia na angeweza kuwa msaada wa kufikisha mipira kwa Alexis.

Mipango ya Bayern Munich ilianzia katika miguu ya humas na Martinez kwanza alafu ndio ikawafikia Alonso, Thiago na Vidal...... Humas na Martinez walikuwa huru kuanzisha mipango yote kwa sababu Arsenal walikuwa nyuma ya mpira na kumuacha Sanchez pekee kama lone streker. Kuna wakati Sanchez alijikuta yupo katikati ya wachezaji wanne wa Bayern Munich katika eneo la nyuma la Bayern na kuwapa mianya ya kufanya walichokipanga wao Bila kusumbuliwa... Hapa Arsenal muda mwingi wakikuwa wako nyuma wanakaribisha mashambulizi.

Kuumia kwa Koscielny kulipunguza nguvu kubwa ya ubora katika safu ya ulinzi ya Arsenal kutokana na uelewano baina yake na Mustaph....... na pia kuliwapa unafuu washambuliaji wa Bayern Munich.

Pamoja na kuwa na viungo wachafu wa kazi mbele ya safu ya ulinzi ( coquelin na Xhaka) Bado salama ya arsenal haikuwepo sababu kulikuwa na njia moja tu ya kudiffend, tofauti na Bayern waliokuwa na njia mbili kuu za kudiffend, ya kwanza ni kukaba kawaida na kwa nguvu pindi arsenal anapokuwa na mpira na ya pili ni kuposses mpira pindi wao wanapokuwa na mpira. Hapa Arsenal yeye alifanikiwa kukaba tuu kwa nguvu muda mwingi Bila kuwa na possession ili kujilinda kirahisi... Na ndipo salama ya Gabriel, Mustaph na Ospina ikawa inatia shaka maana muda mwingi mpira ulikuwa katika eneo lao la hatari.

Hector Bellarin alifakinikiwa katika jukumu moja tu la kumzuia Costa..... Hapa Costa anakuwa chini ya ulinzi wa Bellarin na mara kadha wa kadha Costa alionekana kuhama upande na ndio maana Leo hajapanga nafasi ya kufanya kile tulichokizoea katika upande wake..... Credit to Bellarin.

Bado ile dhana ya unyonge katika nyuso na mioyo ya Arsenal inaendelea kuishi tena na tena. Hapa arsenal wanashindwa kuwa huru kwa mara nyingine tena mbele ya wababe hawa wa Bundasliga. Nazani huu unaweza kuwa ni wakati wenu wa kudai mabafiliko kuliko nyakati nyingine nyingi..... 16 bora sasa imekuwa kama ugonjwa kwenye koti la mzee Wenger..... Ondoeni mawazo ya kuziba Ufa kwa kusajili world class players na badala yake jengeni ukuta kwa maisha mapya Bila mzee wenu mpendwa.

Thiago Alcantara Menzinho.... Miguu ya brazili, kichwa cha brazili ila passport tu ndio ya Spain. Huyu ndiye aliyekuwa mchawi wa Arsenal katika kiungo..... Alikuwa anafanya kile alichoshindwa kukifanya Mesut Ozil..... Thiago aliunganisha mawasiliano baina ya alonso na Vidal na kumfikia Lewandowisk, Roben na Costa kwa wakati.

Hili tatizo la kumfanya Alexis Sanchez awe lone streker na kumuacha pure #9 Olivier Giroud kama backup litaendelea kumtesa sana arsen wenger na Arsenal kwa ujumla. Tatizo lingine kubwa zaidi kwabeki ya Arsenal ni nidhamu ya ukabaji ndani ya box, katika mchezo huu kuna mipira imegusana na mikono ya beki zaidi ya mara Moja na hii ni hatari sana kwa timunidhamu ya ukabaji ya ndani ya box ni lazima ufiche mikono nyuma.

Kumbuka Pale alianz Arena ndipo huwa pahala pa Arsenal kutoka kifua mbele mara kadha wa kadha katika round 16 japo matokeo ya pale huwa hayaibebi arsenal. Sasa kazi itabaki London.

Tutamkumbuka sana Wenger siku tukivuka hii round bila ya koti lake. Mwenye namba za Yule refa anipatie maana watani wa jadi wanahitaji refa.

Bayern Munich 5-1 Arsenal.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom