Makapuku Forum

Makapuku Forum

Gazeti la Nipashe lina habari ambayo imenigusa sana, infact inanihusu. Naomba kuelezwa ni kanisa gani limepiga marufuku ndoa za wazazi?
Nipo kijijini hakuna magazeti huku.
Kanisa lapiga marufuku ndoa wanawake waliozaa.

Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), limepiga marufuku kuanzia sasa ufungishaji ndoa madhabahuni kwa wanawake waliozaa.

Aidha kanisa hilo ambalo ni moja ya makanisa mawili makubwa zaidi Nchini limepiga marufuku pia wanawake wenye ujauzito kufunga ndoa madhabahuni kwa maelezo kwamba kufanya hivyo ni kukiuka maandiko ya Mungu.

Kutokana na uamuzi huo wa Kanisa, kuanzia sasa wanawake wenye sifa hizo hawataruhusiwa kukaa mbele madhabahuni na kufunga ndoa wakiwa wamevaa shela.

Badala yake, imeelezwa ndoa zinazohusu maharusi wanawake wa namna hiyo zitafungwa katikati ya ibada ya kawaida Wakiwa wamekaa na waumini wengine.

Imekuwa kawaida sasa kuona wanawake wenye ujauzito au walishazaa watoto baada ya kuishi na wanaume kinyumba au wakiwa wajawazito wakifunga ndoa madhabahuni.

Kwa mujibu wa tangazo wa tangazo lililosomwa kwenye sharika mbalimbali za KKKT hivi karibuni ni marufuku Wachungaji kufungisha ndoa za aina hiyo.

Umoja Wa ma Boyfriend wasumbufu Tanzania(UBOTA) ...Tunapenda kuwatangazia wana chama wetu kua bado kauli mbiu yetu ni ile ile "NTAKUOA MWAKANI" usijaribu wala kushawishika kuingia kwenye ndoa maana walio ndani ya ndoa wanataka kutoka....!!

*UBOTA OYEeeeeH*
Mhhhhmhhh

Similar Discussions

Back
Top Bottom