Makapuku Forum

Makapuku Forum

Michezo na burudani ..azamu yaambulia goli moja yatwaa kombe la mapinduzi mnyama kaambulia nafasi ya pili ....
6b16b6b9ce239ba09dd7bab24af6481f.jpg
61a3f4ca604a13c141ec1d1e63ddf925.jpg
8126272feea9acf2f5b8bfc8ab50772b.jpg
334841f3ecd477176ac4e65b7534ad84.jpg
173bf35bcd48b467da3cd23d7b297ad0.jpg
902c5c95e2240820335b71791c088dd9.jpg
d7fe9ea3ae144f13a15c26fdb26cfd8a.jpg


Happy birthday Bailly5
 
Kuna mwanamke tajiri alikuwa akiendesha gari lake, katikati ya njia gari likaharibika, akateremka na kuomba lifti, lakini magari yalikuwa yanampita bila kusimama

Alisimama muda mrefu barabarani bila mtu kumsaidia, Mvua ikaanza kunyesha, akaanza kuogopa isije kufika usiku naye yuko barabarani, baada ya muda mfupi akaona gari bovu linakuja akalisimamisha, lakini alikuwa na wasiwasi kuhusu dereva asije kuwa mtu wa hovyo.

Mwisho akaamua kulisimamisha lile gari na yule dereva akasimama, mwanamke akapanda wakaondoka. Akamuona yule mwanaume anaonyesha ni mtu masikini mwenye shida, yule mwanamke akamuona yule mwanaume ni mtu wa heshima, akajilaumu ndani ya nafsi yake kwa kumdhania vibaya, Mwanamke akamuuliza yule mwanaume jina lako nani? Na unafanya kazi gani? Yule mwanaume akamjibu 'Mimi naitwa Adam na kazi yangu ni dereva.'

Baada ya muda wakafika Mjini, yule mwanamke akamwambia 'naomba usimamishe gari Mimi nitashuka hapa,' Yule mwanaume akasimamisha gari, Mwanamke akamuuliza kuhusu nauli yake kiasi gani? Yule mwanaume akamjibu: Nimekusaidia sitaki kitu halafu akaondoka zake.

Yule mwanamke akashangaa sana jinsi yule mwanaume alivyo na utu, mwanamke akaona Coffee Shop akaingia, akamuita Mhudumu, wakati Mhudumu anakuja akawa anamuangalia anavyotembea, alikuwa amechoka sana kwa Ujauzito.

Yule mwanamke akamuuliza kwa nini unajihangaisha? Yule Mhudumu akamjibu najihangaisha ili nipate pesa ya kujiandaa, maana karibuni nitajifungua. Halafu akaenda kumletea kahawa aliyoagiza. Yule Mwanamke akanywa kahawa yake mpaka akamaliza. Halafu akamuita Mhudumu ili amlipe, Mhudumu akachukua pesa akaenda mpaka kwenye meza ya malipo, halafu akachukua chenchi iliyo baki ili amrudishie yule mwanamke.

Chenchi ilikuwa ni pesa nyingi ambayo yule mwanamke angeweza kunywa vikombe zaidi ya 10. Yule mhudumu alipofika ktk meza ya yule mwanamke hakumuona, akatizama kulia na kushoto mwanamke hayupo,alishaondoka, akaona kwenye meza kikaratasi kimeandikwa, chenchi iliyobaki ni zawadi yako, alifurahi sana mpaka machozi yalimtoka, alivyokuwa anachukua ile karatasi akaigeuza upande wa pili akaona imeandikwa
"Na hapo chini ya meza kuna zawadi ya mwanao"
alitizama chini ya meza akaona kuna pesa nyingi, pesa kama za mshahara wake wa miezi 6, alitamani apige kelele kwa furaha, aliomba ruhusa kazini mapema ili arudi kwake.

Aliporudi akawa anapiga kelele anamtafuta mumewe, Mume kusikia zile kelele alishangaa sio kawaida yake kurudi muda huo, alidhani kuwa labda mkewe anaumwa na uchungu, lakini sauti ya kelele ilikuwa ni sauti ya furaha, mke akamuita Mumewe Adam uko wapi mume wangu?
Mke akaendelea kusema Mungu ametuteremshia neema yake nimepata neema kwa mwanamke mwenye kheri, shida zetu zimekwisha Hallelujah!!!

Je, mnamjua Adam wenyewe ni nani? Adam ni yule aliyempa lifti yule mwanamke na ndio mumewe.

Ukifanya WEMA unajifanyia Mwenyewe utakurudia na ukifanya UBAYA unajifanyia Mwenyewe.

NIWATAKIE SIKU NJEMA. C&P
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom