Makapuku Forum

1988 - Katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza mara baada ya miaka takribani 10 huko Pakistan, Benaziri Bhutto anachaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Nchi hiyo.

Mwisho wa siku wakamuua kwa kutegesha bomu kwenye gari
Naipenda kauli yake "Unaweza kumuua mtu lakini sio fikra zake,unaweza kumfunga mtu lakini siyo fikra zake"
........
 
1974 - Paul Scholes anazaliwa.

Kiungo wa zamani wa Man Utd na timu ya taifa ya England. Ni zao la akademi ya Man Utd na alitokea katika " The class of 92 " kikosi cha vijana kilichochukua ubingwa wa F.A wa vijana akiwa na akina Gary na Phil Neville, Beckham, Nick Butty na Ryan Giggs.

Anatajwa kama moja ya viungo bora kabisa kuwahi kutokea Uingereza.

Alijua kupiga pasi za mbali zenye macho, kumiliki mpira na kupiga mashuti hasa mipira iliyokuwa nje ya 18 ( rebound ).

Alistaafu soka klabuni Man Utd mwaka 2011 kabla ya kurudi tena mwaka 2012 baada ya timu yake kukumbwa na majeruhi katika idara ya kiungo.

Leo hi ukiniuliza mchezaji gani aliyestaafu ningependa arudi Man Utd, probably atakuwa Scholes.
 

The class of 92
.........
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…