YANATOKEA NA YANAWAGUSA WATU.
Huyu mwanamke mzuri katika picha ana ujauzito wa miezi minne, lakini mumewe alifariki kwa ajali ya gari kabla mtoto hajazaliwa, na huku akimwachia mtoto mwingine mdogo.
Siku ya kumbukumbu ya ndoa yake aliamua kupiga picha na kuzitengeneza (photoshop) kuonekana kama bado yupo na mumewe aliyekwishafariki.
Alifanya hivyo ili kukamilisha familia yake na kujipa faraja kama zinavyoonekana hapo chini....Inasikitisha na inaumiza sana, usiombee kufiwa na umpendae.
Mpende sana mpenzi wako uliye nae, rekebisheni tofauti zenu hakuna ajuaye kesho, "life is too short to wake up with regrets."
Muda mwingine unaweza ukakubali ukweli kwamba Dunia haina Usawa!
Kazi yake Mungu haina makosa.
R.I.P