Makapuku Forum

Makapuku Forum

7a482aaccee0f9d71aa10ec36318f051.jpg

Chemsha bongo
....
 
Mfano wa wazi kabisa, Pele anatajwa kama mchezaji bora wa wakati wote kisa kachukua kombe la dunia mara tatu hiyo ikiwa moja kati ya sababu.

Katika hizo mara tatu, Mara ya kwanza kachukua mwaka 1958 pale katika ardhi ya Sweden akiwa kinda wa miaka 17 hivyo kwa hesabu nyepesi hakuwa tegemeo ndani ya timu.

Mara ya pili akachukua mwaka 1962 katika michuano iliyofanyika pale Chile, Pele alicheza mechi mbili tu kabla ya kuumia na kukosa sehemu kubwa ya michuano hiyo huku akirudi mechi ya fainali. Shujaa wa michuano akawa Garrincha wa Brazil.

Mara ya tatu, Pele alibeba kombe la Dunia mwaka 1970 pale Mexico. Brazil safari hiyo walikuwa hatari sana, walikuwa na timu inayotajwa kama timu bora ya wakati wote, safari hii Brazil shujaa wao akiwa ni Jaizinho ambaye alifunga goli katika kila mechi yaani kuanzia ile ya ufunguzi mpaka ile ya fainali. Brazil ilienea mastaa kama Tostao, Carlos Alberto, Coldoado na wengineo.

Hapo tunapata jibu, Pele hakuwahi kuwa hata mfungaji bora achilia mbali mchezaji bora wa mashindano hayo.
Bali alizungukwa na mastaa waliokuwa wana uwezo sana.

Pia katika levo ya klabu Pele hakuwahi kucheza Ulaya, ambapo ndio kuna soka la ushindani hasa ukilinganisha na Amerika ya Kusini na Amerika ya kaskazini hivyo akashindwa kukutana na mabeki wa shoka na wakatili waliosifika katika miaka hiyo ya 1960-1970's. Hivyo hizo goli 1000 alizifunga kwa mabeki wachovu.

Unamuitaje mwanasoka bora wa wakati wote?
Sipend kuwazungumzia wachezaji ambao macho yangu mawili hayakuwashuhudia..
 
Back
Top Bottom