shululu
JF-Expert Member
- Jan 26, 2015
- 28,137
- 109,912
Josee anatakiwa kubeba lawama za wazza1985 - Wayne Rooney anazaliwa.
Ni staa wa Man Utd na timu ya taifa ya England. Anajulikana kama " Wazza " akifananishwa na kiungo matata wa enzi hizo Paul Gascoine " Gazza ". Ni shabiki mkubwa wa Everton.
Ni moja kati ya wachezaji wa Kiingereza aliyekuwa na kiwango kikubwa katika enzi zake.
Ameshinda kila taji kwa level ya klabu.
Anakumbukwa kwa goli la Tik Tak dhidi ya Man City katika ligi kuu na goli lilichaguliwa goli bora la miaka 20 ya EPL.
Ndiye mfungaji bora wa wakati wote katika timu ya taifa ya England huku klabuni akiwa amebakiza magoli 9 awe mfungaji bora wa kihistoria wa klabu hiyo.
Kwasasa ameanza kupoteza makali yake, ikashiria mwisho wa zama umewadia.