Makapuku Forum

Makapuku Forum

1475907772234.jpg
1475907779356.jpg

Karibuni sana katika kuperuzi magazeti yaliyotufikia asubuhi ya leo
 
Ni kweli kabisa, Che Guevara ni mzaliwa wa Argentina lakini kwa mchango wake mkubwa alioufanya nchini Cuba, amezikwa huko Cuba kwa heshima zote.

Hii ni kudhihirisha watu wanajali na kuthamini nini umewafanyia na hawajali umetokea taifa gani?

Huku kwetu Dunia ya tatu, Watanganyika na Wazanzibar wamemfuta kwenye historia yao, kiongozi wa Mapinduzi mataukufu ya Zanzibar, Field Marshall John Okello eti kisa ni Raia wa kigeni, Ujinga ulioje??

Wanatuaminisha Karume ndio baba wa mapinduzi yale ya Januari 12 mwaka 1964. Upumbavu ulioje??
Hidtoria yetu haiko sahihi, waliopigania nchi hii hawatajwi ila wababe na wajanja ndo wamepewa heshima
 
Tatizo mwl hakupenda kukosolewa
Historia yetu imewazima na kuwasahau watu wengi sana katika Taifa hili eti tu labda walitofautiana na Waasisi wa Taifa hili kipindi hiko.

Mchango wa Oscar Kambona umesahaulika kabisa. Bila Kambona, mwalimu asingeendelea kuwa Rais wakati Jeshi lilipoasi Mwaka 1964 na Mwalimu kuamua kujificha zake Kigamboni akishindia mapapai.

Ni aibu sana kwa Taifa kuwasahau watu wa aina ya Kambona, Jumbe na wengineo.
 
Back
Top Bottom