Heshima kwenu wakuu.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nimeona leo niwashauri Watanzania wenzangu wanaopenda kufanya maamuzi bila kufanya utafiti.
Wazo/ ushauri huu nimeamua kuuleta hapa baada ya tukio baya la kujaribu kuutoa UHAI wa kijana mmoja asiye na hatia jijini Arusha leo mchana.
TUKIO LENYEWE
majira ya saa 6:30 mchana nikiwa maeneo ya GOLDEN ROSE hotel,
Niliona kijana mmoja akijaribu kuvuka barabara kwa haraka.
KILICHOFUATA
baada ya baadhi ya watu walipomwona akivuka haraka, walianza kupiga kelele za mwizi mwiziii, ghafla nilimwona rafiki yangu jina kapuni naye akitoka na chuma mkononi mwake naye alianza kulifuata kundi hilo linalomfukuza kijana.
KIJANA AKAMATWA
kwa wale wenyeji wa Arusha maeneo ya golden rose lina watu wengi, hivyo huyo kijanahaikuwa vigumu kukamatwa na ghafla walianza kumshambulia kwa vyuma ngumi na mateke.
TUKIO LILIVUTA HISIA
Baada ya kuona hivyo ghafla moyo wangu ulifadhaika kwa kuona kijana anauawa mbele ya macho yangu, hivyo nilitamani KUJUA sababu inayompelekea umauti kwani sikuona kama atapona.
Nilianza kuwahoji waliokuwa mstari wa mbele kumpiga kwa kuanzia na huyu jamaa ninayemfahamu.
Hakunipa majibu ya kuridhisha, wapili na wa tatu wote hawakuwa na majibu
NILICHUKUA HATUA ZA KUHATARISHA UHAI KUMNUSURU
baada ya kukosa majibu ya kwanini wanataka kumuua ndipo nilipoamua kuingia ktkt ya kundi kubwa na kuwaomba wale wanaompiga kujiridhisha na hatua hiyo kabla hawaja muua.
Walinikasirikia wakidai huyo ni mwizi nami niliwahoji
Kaiba nini
Aliyeibiwa yu wapi
Ameiba k2 gn?
Walikosa majibu, wakatulia japo kabla ya kutulia walinikasirikia na kunitolea lughachafu, nami ckujali nilivaa ujasiri nikwaambia tumhoji
MAHOJIANO YAKAANZA
baada ya kuanza kuhoji tuligundua ni mtu alikuwa na haraka zake akikimbilia mteja anayemsubiri dukani baada ya kumpigia simu kuwa anamsubiri.
Ndipo umati uliponigeukia na kunipongeza kwa ujasiri.
SWALI
je ni watanzania wangapi wameuawa bila hatia?
Kuna gharama gani kuhoji na kujiridhisha kabla ya kuchukuahatua?
NINASHAURI TUSIFANYE MAAMUZI KABLA YA UTAFITI