Makapuku Forum

NUKUU NO 1#

Wananchi pamoja na serikali yao ya Muungano wanazikaribisha nchi jirani na nchi yoyote itakayokuwa tayari kujiunga na umoja huo ili kufikia hatua inayotakiwa.
Hatuwezi kwa mara moja kuunganisha Africa yote, ila kwanza ni juu yetu kuungana kidogo kidogo mpaka kufikia kitu kimoja.

Haya yalisemwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Amani karume, July 30,1964 katika mkutano wa hadhara mjini Unguja, Abeid Amani karume alizaliwa Agosti 4,1905 na kuuawa April 7,1972
 
DECI, RIFARO
 
NUKUU NO 2#

Kwa kadri maisha yanavyokuwa ndivyo yanavyokupa nguvu zaidi ya kukabiliana nayo ili hatimaye kufikia kelele cha mafanikio
Maisha ni suala la mapambano, anayeshinda pambano ndio bingwa

Maneno haya yalisemwa na waziri mkuu wa zamani wa Cambodia, Lon Nol.
Lon Nol alizaliwa Nov 13,1913 na kufariki Dunia Nov 17,1985
 
NUKUU NO 3#

Nawasifu wanajeshi wote wa Tanzania kwa uhodari, ushupavu na moyo wao thabiti wa kulinda taifa letu

Nawaomba waendelee kuwa na moyo huo pamoja na kusaidia wakazi wa vijiji vya ujamaa vilivyoko jirani na kambi zao katika mipango yao ya kuzalisha mali

Maneno haya yalisemwa na Edward Sokoine, akiwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa, Agosti, 1972

Edward Sokoine alizaliwa Agosti 1,1938 na kufariki Dunia April 12,1984 amewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…