Kitombise
JF-Expert Member
- Sep 24, 2013
- 8,652
- 25,849
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
SIMULIZI: ANTI EZEKIEL
MTUNZI: George Iron Mosenya
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
Nikatamani kumbeba lakini ningempeleka wapi, nikarejea njia niliyotoka, nikaifuata kwa muda na kukutana na tena na ile ofisi kubwa ya vioo.
96…..59….. nikasahau namba mbili za mwisho, maana ofisi ile ilikuwa imefungwa kwa namba za siri. Nikatimua mbio hadi kwa yule bwana, bado alikuwa amekodoa macho,
“Nimesahau namba mbili za mwisho ndugu yangu….namba za siri…TISA SITA TANO TISA…….” nikamtajia ili amalizie lakini hakuwa akiweza tena kusema , akabaki kukodoa macho, mkojo kidogo unitoke kwa kutamani aweze kusema ili nijue ni nini katika makablasha yale.
Nikamtikisa lakini hakuonekana kupatwa na hisia zozote zile!!
Mkojo ukachuruzika!! Sikuweza kuuzuia!!
Na hapo nikasikia vishindo kwa mbali!!!!
Hofu ikazidi.
Nikageuka huku na kule kama kuna mtu yeyote anayekuja, lakini nikaambulia kukutana na kiganja cha yule bwana kikigongagonga chini!!
Mlio huu nikaupokea kama vishindo kutoka mahali pengine
Mara Nikauona mkono wake ukijitahidi kuchora chini!!
Nikaona SIFURI MOJA.
Nikatimua mbio hadi kule kwenye ile ofisi tena.
Nikaingiza namba zile!!
Mlango ukafunguka!! Nikaingia ndani upesi hadi katika meza kuu.
“E.F.Kenton MANAGER!” meza ile ilipachikwa kibao kile, nikaingia katika makablasha na kusaka hicho alichonambia yule bwana.
Nikakutana na faili kubwa kabisa rangi yake nyeusi, nikalichukua na kulifunua ndani kidogo.
Naam! Lilikuwa lenyewe ambalo nilikuwa nalihitaji kwa ukombozi wa kizazi hadi kizazi. Maneno kadhaa yaliyoandikwa yalinivutia sana na kutamani kujua mwandishi wake aliandika nini cha ziada katika ukubwa wote ule.
Nikataka kutoka upesi ndani ya himaya ile na hapa nikakiri kufanya kosa kubwa katika sehemu ya hatari kupita zote.
Nilikuwa nimesahau namba za siri tena huku mlango ukiwa umejifunga kwa ndani!! Sikuwa nauwezo wa kumfikia yule bwana wa kujiita anti Ezekiel anitajie tena kwa umakini, nilichokumbuka ni ile SIFURI MOJA aliyoichora chini. Zile nne za kwanza zilikuwa zimeyeyuka.
Mungu wangu!!
Nikakibinyabinya kichwa changu kiweze kukumbuka zile tarakimu nne za mwanzo, lakini badala ya kuja tarakimu za kufungulia mlango, likawa linarejea lile neno kubwa kabisa katika faili nililokuwa nimebeba.
Hakika neno lile lilikuwa zito kuliko zile namba na lilikuwa la kushtua sana, huenda nd’o lilinipagawisha na kunisahaulisha juu ya namba za siri.
Nikatulia na kujifanya kuwa sina hofu ili nikumbuke zile namba.
Nikakumbuka kuwa kuna namba tisa na nyinginezo lakini mpangilio sikuukumbuka kabisa.
Nilijaribu mara kwa mara kubahatisha namba tofauti tofauti katika kile kitasa kinachotumia umeme, mara ya kwanza, ya pili hadi ya nne mambo bado yalikuwa magumu, na ilipofika mara ya tano mara king’ora kikaanza kulia.
Huku ikiandika neno nililolielewa “PASSWORD ERROR”
Hatari kubwa!! Nikaanza kuhaha huku na kulke katika ile ofisi nikitafuta namna ya kuweza kutoka nje kama ipo!!
Lakini ngome yote ilikuwa vioo vigumu tupu!!
Sikutaka kukamatwa nikiwa nimekaribia mwisho kabisa wa mchakato wangu! Sikuwa tayari kukamatwa huku nikiwa na ile nyaraka muhimu kabisa zaidi ya ile bahasha iliyopotea awali katika mazingira ya kutatanisha.
Nikatazama huku na kule na kukutana na na chuma kubwa ambalo sikujua matumizi yake lakini lilikuwa zito haswa.
Nikatua faili langu chini, nikakinyanyua kile chuma kizito kabisa. Kama zinavyokuwa filamu za mapigano nami nikaamua kuwa shujaa wa vita hiyo.
Navunja vioo!! Nikajiapiza, nikayauma meno yangu kwa nguvu kisha nikatimua mbio, chuma likiwa mkononi, nikajitosa kiume moja kwa moja hadi katika hifadhi hiyo ya vioo, nikakitupa kile chuma kwa nguvu zote. Nikasambaratisha vile vioo mbalimbali. Nikatua upande wa pili kwa kujitupa baada ya kile chuma kuwa kimenitoka mikononi mwangu.
Sikutaka kuyafikiria maumivu kwanza, nikainuka mbiombio nikikanyaga vile vioo kwa viatu vyangu, nikakifikia nilichokihitaji.
Faili likawa mkononi tena!!
Baada ya kulikamata lile faili mkononi ndipo nikayakumbuka maumivu makali usoni, mikononi na mgongoni. Kisha nikaona damu.
Vioo vilikuwa vimenitakata vibaya mno na kile king’ora kilishanyamaza kimya!!
Ina maana hakuna walinzi humu ndani!!!! Nilijiuliza huku nikistaajabu maajabu hayo ya Michigani.
Niliendelea kuzurura huku na huko, hatimaye nikayaona mazingira hayo ya Michigan ambayo awali niliyaona katika picha alizonionyesha mama lao.
Michigani!! Neno likanitoka!! Nikajisikia natabasamu kwa ndani kuwa hatimaye nipo katika lile jumba la ahadi ya siku nyingi.
Roho ya kinyama tayari ilikuwa imenikaba nikahakikisha kuwa funguo wangu upo mfukoni. Nikatafuta kwa udi na uvumba mahali pa kutokea. Miguu pia ilikuwa imekatwa na vioo, kila nilipokanyaga niliacha damu, safari hii hata wale watoto waliokuwa wakinililia katika vioo walinihofia.
Niliutumia ule ufunguo wa maajabu kufungua huku na kule!!
Chumba kimoja nilipokifungua kikatoka kipande cha mtu ambacho kilikuwa bado kina nguvu!! Kikanirukia kwa ghadhabu, nikapiga mweleka chini.
Akanifuata kwa kasi, nikahofia juu ya faili langu.
“Mimi ni mtu mwema tafadhali, mimi ni mtu mwema!!” nilimsihi. Lakini hakuonekana kunielewa, akazungumza kiarabu!!
Lugha gongana!
Nikaiona hatari waziwazi!! Nikajaribu kumkwepa nikaishia kuegemea vioo. Akaja mbiombio nikaona isiwe tabu kwa sababu ni heri mtu mmoja afe kuokoa taifa zima.
Nikajifanya kumkimbia huku nikiwa na wazo moja tu.
Akaendelea kufoka kiarabu nisichokielewa na mimi nikazidi kukimbia, hadi nikalifikia lile jengo lililopalanganyikana, nikatupa faili chini, nikatwaa kioo kikubwa kilichovunjika upesi. Nikageuka na kukutana na jitu lile lenye nguvu likinijia kwa kasi.
Nikamsukumia kile kioo.
Naam!! Kikazama tumboni huku kikinichanachana mikono yangu vibaya sana. Nikaokota faili langu, likawa linaloa damu lakini sikutakiwa kusimama wala kujiuliza. Nikasahau kuhusu maumivu nikaweka riadha mbele.
Nikapenya huku na kule hadi nilipokutana na mlango mwingine, nikaufungua ule kwa ufunguo wangu! Nikakutana na mwanga hafifu kiasi fulani. Na ngazi kadhaa, nikazifuata hizo hadi nilipofikia kizibo ambacho kilikuwa kinafunguka bila ufunguo, nikasukuma juu, mwanga halisi wa dunia ukaingia ndani, nikachungulia nje kabla ya kutoka mzima mzima.
Nikakutana na hali halisi ya Iringa, funguo mfukoni faili langu mkononi. Nikawa duniani tena nisiamini kuwa nipo hai. Hali ile ya hewa ilinifanya nishindwe kutabiri muda halisi.
Nikatumia shati langu kujifuta damu zilizokuwa zinatiririka, kisha nikaanza kujiuliza hapo nilipokuwa ni wapi. Maana lilikuwa eneo jingine kabisa.
Nikaangaza kwa utulivu hadi nilipoiona barabara! Nikaifuata na kisha kuingia katika kichochoro kingine na kukutana na mfano wa chemchem, nikatwaa maji na kujinawisha usoni na popote palipoonyesha damu.
Hatimaye simu yangu ikanirejeshea fikra za msaada. Kutazama ilikuwa ikilalamika kuwa betri imeishiwa chaji. Nikafanya upesi kumpigia Jojina lakini hata simu haikuita ikawa imezima.
Sikuwa na muda wa kupoteza. Nikaruka matuta kadha wa kadha na hatimaye nikaupata uelekeo sahihi wa kuelekea Michigani kwa Masawe! Sikuliacha faili langu na sasa likiwa katika mfuko. Nilihitaji kujua nini chanzo cha haya yote.
Siku hii dukani pale umati ulijaa, nikastaajabu nini kinaendelea. Nikaomba kupita lakini watu walikuwa wabishi sana, nikajitahidi kupenya hivyohivyo. Hadi nikaufikia ukuta wa polisi ambao haukuruhusu mtu yeyote kupenya pale, mimi nikiwa na kihoro nikapenya huku nikiwa nusu nakimbia nusu natembe, risasi ikafyatuka na kuchimba pembeni ya mguu wangu, mara nikasikia napaishwa hewani. Sasa nikayasikia maumivu!!
Risasi ilikuwa imenichuna!!
“Mimi raia mwema jamani, mimi raia mwema!!” nikapiga kelele sana. Askari wakanisogelea wakiwa na hasira kali, wakataka kuchukua kilicho mikononi mwangu nikawa mbishi sana sikuwa nawaamini hata kidogo. Niliamini kabisa kwa jinsi sura yangu ilivyokwanguka kwanguka hakuna ambaye angeweza kunijua.
Kipigo kikazidi wakinisihi niachie na hapo nikamkumbuka mtu wa kunisaidia. Lakini kabla sijajua nitamfikia vipi nikakanyagwa teke mbavuni, mbavu za upande uleule ambao nilikuwa nimeshikilia lile faili.
Naam! Nikalainika na kuliachia lile faili huku macho yakianza kuona giza.

kumbe imebaki episode 1 ili riwaya iishe!