Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mbona hicho ni KINGONGO(tafsiri ya ngongo utapata usiku kupitia Fix za Bitoz)

...........
Embu ngoja nisubirie hizo fix
371f7e95513c45d8eb2a1123cb15ceb9.gif
 
"PAID IN FULL WITH GLASS OF MILK"

Mwaka 1870 katika kitongoji cha Camdem, mji mdogo wa New Jersey nchini Marekani kijana mmoja kutoka familia maskini alikua akiuza vitu vidogo vidogo mtaani ili kujipatia mahitaji ya shule. Alipita nyumba kwa nyumba akigonga geti na kuuliza kama wenyeji walihitaji kununua kwake.

Ilimhitaji kuamka kila siku saa 11 alfajiri ili azunguke mtaani kufanya biashara kabla ya kurudi nyumbani na kujiandaa kwenda shule. Na alipotoka shuleni jioni aliendelea na biashara yake kabla ya kurudi nyumbani na kujisomea.

Katika umri mdogo wa miaka 12 alishapitia changamoto nyingi za maisha. Mfumo huu wa maisha haukuwa rahisi kwake lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kuongeza bidii shuleni akiamimi ipo siku atafanikiwa.

Siku za weekend alizitumia kufanya biashara na kwenda kanisani. Siku moja (weekend) akiwa mtaani hakufanikiwa kuuza chochote, kwa hiyo hakuwa na fedha. Akiwa amechoka sana kwa kutembea kutwa nzima pamoja na kuchomwa jua alihisi njaa. Kwakuwa hakuwa na fedha hakuweza kununua chochote kwa ajili ya kutuliza njaa yake. Akahisi mwili kukosa nguvu na akatamani ajipumzishe chini ya mti.

Baadae akapata wazo. Akasema atagonga mlango wa nyumba moja aombe chakula. Alipogonga akatokeza binti mmoja kufungua geti. Kwahofu yule kijana akaogopa kuomba chakula akaomba maji ya kunywa.

Yule binti akaingia ndani na kumletea glasi ya maziwa badala ya maji. Yule kijana akashangaa imekuaje. Lakini kwa kuwa alikua na njaa akanywa kwanza kisha akamuuliza "unanidai bei gani kwa maziwa haya?"

Yule binti akamwambia "sikudai chochote". Kijana akamuuliza "kwanini?" Yule binti akamjibu "mama yangu aliniambia nisikubali malipo kwa kufanya jambo la utu (never accept payment for a kindness)"

Yule kijana akaomba yule binti amtajie jina lake akamtajia. Akamshukuru kisha akaendelea na safari yake.

Takribani miaka kama 30 hivi ikapita. Kijana yule ktk safari yake ya maisha akafanikiwa kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama (Gynecologist), katika hospitali kubwa duniani ya Johns Hopkins iliyopo mjini Baltimore huko Maryland nchini Marekani. Kijana huyo aliitwa Dr.Howard Kelly.

Siku moja Dr.Howard akiwa ktk shughuli zake za utabibu akaletwa mwanamke mmoja aliyekua amedhoofu mwili kwa sababu ya maradhi. Alikuwa akisumbuliwa na magonjwa ya kina mama. Baada ya kuhangaika muda mrefu katika hospitali ndogo hatimaye akapewa rufaa ya kwenda Johns Hopkins Hospital ili kukutana na madaktari bingwa (Specialists).

Baada ya kusoma maelezo ya mgonjwa Dr.Kelly akafanikiwa kumtambua yule mwanamke. Ni yule binti aliyemsaidia glasi ya maziwa kipindi kile akiwa mtoto. Zaidi ya miaka 30 iliyopita.

Baada ya matibabu yaliyotumia zaidi ya miezi sita kitandani hatimaye yule mwanamke akapona. Lakini akakuta "bill" ya gharama za matibabu yake ni kubwa sana. Familia yake na ndugu zake wakaanza kulia maana hawakuwa na uwezo wa kulipa.

Yule mama akafikia uamuzi kwamba ataenda kufanya kazi katika kipindi chote cha maisha yake kilichobakia na mshahara wake wote ulipwe hospitali ya Johns Hopkins hadi siku atakayokufa au atakayopoteza uwezo wa kufanya kazi.

Bahati nzuri Dr.Kelly ndiye aliyekuwa daktari mwandamizi hospitalini hapo (Medical Officer in charge). Alipopelekewa karatasi ya malipo na kuisoma akaamua deni lote alipe yeye.

Akarudi kwa yule mwanamke na kumwambia "huna haja ya kusononeka kwa sababu gharama zote unazodaiwa ulishazilipa miaka 30 iliyopita". Yule mama akastaajabu alilipaje miaka 30 iliyopita wakati alikua msichana mdogo tu.

Dr.Kelly akampa ile karatasi ya bill ikiwa imeandikwa "Paid in full with glass of milk". Yule mama akakumbuka tukio la zamani sana alipomsaidia kijana mmoja fukara aliyegonga getini kwao akiomba maji akampa glasi ya maziwa.

#Moral_of_the_Story;
Habari hii ni ya kweli na kwa mara ya kwanza aliiandika Dr.Howard Kelly mwenyewe kabla hajafariki. Baada ya Dr.Kelly kuandika imekuwa ikitumiwa mara kwa mara katika mafundisho ya kuhamasisha watu na kuwatia moyo kimaisha (inspiration talks and speech).

Jambo kubwa la kujifunza hapa ni kuwa, mara nyingi tunafanya mambo mbalimbali ktk maisha yetu na tunagusa mioyo ya watu. Katika mambo yote tufanyayo yawe mazuri au mabaya, yawe makubwa au madogo tunagusa mioyo ya watu wengine. Unaweza kufanya jambo leo ukaliona dogo lakini hujui limemgusaje uliyemfanyia.

Ipo nguvu kubwa katika mambo tufanyayo. Dr.Kelly aliona thamani ya glasi ya maziwa aliyopewa miaka 30 iliyopita. Pengine yule mama asingekaa akumbuke kama aliwahi kumpa mtu maziwa. Lakini Dr.Kelly alikumbuka kwa sababu yeye ndiye aliyetendewa. Mara nyingi mtendaji anaweza kusahau lakini anayetendewa sio rahisi kusahau.

Maisha unayoishi leo yanatokana na mambo uliyoyafanya jana. Na maisha utakayoishi kesho yatatokana na vile ulivyo leo. Je leo ukoje? Au jana uliishije?

Yawezekana hupati kazi tangu umalize masomo yako japo una sifa zote muhimu, kutokana na ulivyoishi jana. Yawezekana umepata kazi baada tu ya kuhitimu, ukadhani una bahati au una akili sana. No! Ni kwa sababu ya jinsi ulivyoishi jana.

Unaweza kusahau uliyoyafanya, lakini baraka na laana zinatokana na yale tufanyayo hata yawe madogo. Jiulize unapokua ndani ya gari yako ukaona watoto wanakugongea kioo na kuomba msaada huwa unafanya nini? Huwa unasema nini? Mazuri au mabaya? Jiulize unapoona wagonjwa wasiojiweza mahospitalini umewahi kufanya lolote juu yao? Si lazima uwape fedha lakini je umewahi hata kuwaombea?

Unapoona wafungwa magerezani, watoto yatima, wazee wasiojiweza huwa unafanya nini? Huwa unasema nini? Je unajua kwamba kuna nguvu kubwa katika yale ufanyayo au usemayo? Je unajua kwamba mambo unayofanya au kusema leo yataakisi maisha yako ya kesho?

Usipuuze jambo hata likiwa dogo kiasi gani. Dr.Howard Kelly hakupuuza nguvu ya glasi ya maziwa aliyopewa miaka 30 iliyopita. "Katika maisha wekeza utu, acha alama ya wema kwa binadamu... huyu mwanamke alicha alama ya wema moyoni mwa Dr. Kelly"
Inspirational!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom