Serikali ya Zanzibar haina wasi wasi na hatari zinazoandikwa na waandishi vibaraka kuhusu Zanzibar, lakini inaendelea na juhudi zake za mipango ya maendeleo kama kawaida. Wale wanaotoa propaganda za namna hiyo hawapendezwi namna Zanzibar inavyofanya maendeleo yake. Hayo yalitamkwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani karume, September 13,1971, ikulu ya Zanzibar, alipotembelewa na wanafunzi wa uandishi wa habari kutoka chuo cha uandishi wa habari Nairobi, Kenya