Makapuku Forum

Makapuku Forum

Manii ya nguruwe yanatoka kwa awamu tatu kuu ndani ya hizo dakika:

- Awamu ya Kwanza (Pre-sperm): Majimaji ya wazi yasiyo na mbegu yanayosafisha njia.

- Awamu ya Pili (Sperm-rich): Sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa mbegu za kiume (hii ndio sehemu muhimu zaidi ya utungisho).

- Awamu ya Tatu (Post-sperm/Gel): Majimaji mazito kama jeli au kamasi. Kazi ya jeli hii ni kuziba mlango wa uzazi wa jike (cervix) ili kuzuia mbegu zisimwagike nje baada ya dume kushuka.
Screenshot_20260729_205230_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_205254_InstaPro%20.jpg
 
Kula kinyesi, japo ni tabia ya asili ila pia kunaweza kueneza minyoo na magonjwa kwa haraka kati ya nguruwe.

Kwa mfugaji Ili kuzuia au kupunguza tabia hii, hakikisha: Banda linasafishwa mara kwa mara, wanapata chakula chenye viwango sahihi vya madini na vitamini pia banda lina nafasi ya kutosha.
Screenshot_20260729_205525_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_205545_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_205615_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_205634_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_205703_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_205730_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_205748_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_205811_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_205830_InstaPro%20.jpg
 
NB: Ukweli kuhusu matope: Nguruwe hawana tezi za jasho (sweat glands), hivyo hujigaragaza kwenye matope ili kupunguza joto la mwili na kujilinda na jua au wadudu.
Screenshot_20260729_210023_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_210045_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_210106_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_210126_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_210146_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_210208_InstaPro%20.jpg
 
Kama unasumbuliwa na ndoto hizo, jitahidi kurekebisha mtindo wa maisha (kupunguza stress), kufanya meditation, na kuepuka kutumia simu au kuangalia habari mbaya kitandani..ni baadhi ya tabia nzuri kuelekea kupata ndoto nzuri na zenye afya.
Screenshot_20260729_212355_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_212418_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_212437_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_212456_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_212513_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260729_212533_InstaPro%20.jpg
 
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (NEC), imemteua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na aliyewahi kuwa mbunge wa Siha, Mkoa wa Kilimanjaro, Aggrey Mwanri kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara akichukua nafasi ya John Mongella.

Uamuzi huo umetolewa leo katika Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika Zanzibar leo.View attachment 3639439
Sawa.
Kila la kheri kwake mzee w Siha
 
Jeshi la Polisi Tanzania limesema kutokana na hali ya usalama Nchini kuwa shwari, Vyama vya Siasa na Wadau wengine wenye nia ya kufanya mikutano wanaruhusiwa isipokuwa kwa kuwasilisha taarifa kwa Wakuu wa Polisi wa Wilaya husika kama Sheria inavyoelekeza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai 29, 2026 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Makao Makuu Dodoma, awali lilikuwa likitoa tahadhari kuhusu baadhi ya Watu waliodaiwa kupanga na kuhamasisha vitendo vya kihalifu kwa kutumia maandamano yasiyofuata Sheria ikiwemo kupanga mauaji, kuchoma moto shule, kulipua transfoma za TANESCO, kufunga barabara na kupora silaha za Askari.

Jeshi la Polisi limesema kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama, lilifanikiwa kuwafuatilia na kuwakamata baadhi ya Watuhumiwa, huku wengine wakiendelea kutafutwa.

Aidha, Polisi imewashukuru Wananchi kwa ushirikiano wao na kusisitiza kuwa kutokana na hali ya usalama kuendelea kuwa shwari, Vyama vya Siasa na Wadau wengine wenye nia ya kufanya mikutano waendelee kuwasilisha taarifa kwa Wakuu wa Polisi wa Wilaya husika kama Sheria inavyoelekeza.

Jeshi hilo pia limetoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa taarifa za viashiria vyovyote vya uhalifu au mipango ya kufanya vitendo vya kihalifu ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.View attachment 3639442
Sawa.
Kazi nzuri kwenu
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru wanafunzi 17 na Mhitimu mmoja wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati mbalimbali Jijini Dar es salaam waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kughushi nyaraka na kujipatia mikopo ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kwa njia ya udanganyifu.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Romuli Mbuya baada ya kukubaliana na hoja za Wakili wa Utetezi, Peter Madereka kwamba hati ya mashtaka ilifunguliwa kinyume cha Sheria kwa kuwa haikuambatana na nyaraka zote za ushahidi kama inavyotakiwa.

Hata hivyo, Upande wa Mashtaka ulidai kuwa Sheria inaruhusu ushahidi kuwasilishwa siku nne kabla ya kusomwa kwa hoja za awali, lakini Mahakama haikukubaliana na hoja hiyo na kuiondoa hati ya mashtaka, hivyo kuwaachia huru Washtakiwa wote.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya kuachiwa huru, washtakiwa hao walikamatwa tena na askari.

Kwa mujibu wa mashtaka yaliyokuwa yamewasilishwa Mahakamani, Washtakiwa hao walikabiliwa na jumla ya makosa 47, yakiwemo kughushi nyaraka, kutoa nyaraka za uongo na kujipatia mikopo ya HESLB kwa njia ya udanganyifu.

Ilidaiwa kuwa kati ya Juni 2024 na Novemba 2025 waliandaa na kuwasilisha nyaraka za uongo kupitia mfumo wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu (OLAMS), wakidai wao au wazazi wao wana ulemavu ili waweze kupata mikopo ambayo hawakuwa na sifa ya kuipata.

Baadhi yao walidaiwa kujipatia mikopo ya kati ya shilingi milioni 1.8 na shilingi milioni 5.89 kwa kutumia taarifa hizo za uongo.View attachment 3639443
Aiseee.
Kazi wanyo
 
Mahakama ya Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga imemhukumu Isa Musini Rashidi kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kusafirisha kilo 75.15 za dawa za kulevya aina ya mirungi.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Azizi Khamis ambaye amesema Upande wa Mashtaka uliwasilisha ushahidi wa kutosha uliothibitisha kosa dhidi ya mshtakiwa bila kuacha shaka yoyote.

Upande wa Mashtaka ulidai kuwa Aprili 10, 2026 katika eneo la Kinyatu ‘A’, Wilaya ya Mkinga, Maafisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) walimkamata Isa akiwa anaendesha pikipiki aina ya Huoniao yenye namba MC 569 EYG, akiwa amebeba mifuko miwili yenye jumla ya mafungu 122 ya majani yaliyodhaniwa kuwa mirungi.

Uchunguzi wa Mkemia Mkuu wa Serikali ulithibitisha kuwa majani hayo yalikuwa mirungi yenye uzito wa kilo 75.15.

Katika kesi hiyo, Upande wa Mashtaka uliwasilisha Mashahidi watano pamoja na vielelezo 10, huku Mshtakiwa akikana mashtaka yote.

Baada ya kupitia ushahidi wa pande zote, Mahakama ilimtia hatiani Isa kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya na kumhukumu kifungo cha miaka 30 jela.

Mahakama pia imeamuru pikipiki iliyotumika kusafirisha mirungi hiyo itaifishwe na kuuzwa kwa mnada wa hadhara.View attachment 3639445
Aseee.
Miaka 30🙄
Pole yake
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila, leo Julai 29, 2026 amefanya ukaguzi katika mizani ya kupimia malori ya Malawi Cargo iliyopo Bandari ya Dar es salaam, ambapo amesisitiza kuwa Viongozi na Taasisi zinazohusika zinapaswa kutekeleza wajibu wao badala ya kutegemea kila maamuzi yatolewe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Baada ya ukaguzi huo, Chalamila ameagiza kuanza mara moja kwa operesheni maalum ya kuondoa malori yote yaliyopaki kandokando ya barabara, akisema hatua hiyo inalenga kupunguza msongamano wa foleni unaojitokeza mara kwa mara katika maeneo yanayozunguka bandari.

“Kila jambo tukisema Rais Samia, Rais Samia, tutakuwa tunamchosha,” amesema Chalamila.

Ameeleza kuwa maegesho ya malori ndani ya hifadhi ya barabara yamekuwa yakichangia kuziba njia, kuchelewesha usafirishaji wa watu na mizigo, pamoja na kuathiri mtiririko wa shughuli za kiuchumi.

Aidha, amezitaka Taasisi zote zinazosimamia barabara, usafirishaji na usalama barabarani kushirikiana kikamilifu kuhakikisha operesheni hiyo inatekelezwa kwa ufanisi na kwamba malori yote yanaegeshwa katika maeneo rasmi yaliyotengwa badala ya kandokando ya barabara.View attachment 3639447
Tunataka utekelezaji, Malaori yanasumbua sana
 
Mwanafunzi mmoja Nchini India amedai kudukua tovuti za Taasisi za Teknolojia za India, Indian Institute of Technology Kanpur (IIT-K) na Indian Institute of Technology Madras (IIT Madras) baada ya kukosa nafasi ya kujiunga na Shahada ya Usalama wa Mtandao (Cyber Security) chuoni hapo.

Mwanafunzi huyo aliacha ujumbe kwenye tovuti ya IIT-K uliosomeka, “Site is hacked, All I need is just a fair chance” (Tovuti imedukuliwa, ninachohitaji ni nafasi ya haki) ambapo amesisitiza kuwa hakulenga kusababisha madhara bali kuonyesha uwezo wake wa kiufundi.

Mkurugenzi wa IIT-K, Manindra Agrawal amesema Mwanafunzi huyo hakuchaguliwa kwa sababu hakuwa na uzoefu wa awali katika masuala ya usalama wa mtandao.

Hata hivyo, Taasisi hiyo imeamua kumwalika chuoni kwa ajili ya mtihani maalum wa kupima uwezo wake, na akithibitisha umahiri wake, atazingatiwa katika mzunguko ujao wa udahili.

Agrawal pia amethibitisha kuwa Mwanafunzi huyo alipata ufikiaji wa baadhi ya sehemu za tovuti rasmi za IIT-K na IIT Madras.

Amesema badala ya kufungua kesi mara moja, Taasisi hiyo itakutana naye ili kumshauri kwamba kuingia kwenye mifumo ya kompyuta bila idhini ni kosa la kisheria na halipaswi kurudiwa, huku ikitathmini pia uwezo wake wa kiufundi.View attachment 3639448
Aiseee.
Dogo Umetisha sana
 
Kula kinyesi, japo ni tabia ya asili ila pia kunaweza kueneza minyoo na magonjwa kwa haraka kati ya nguruwe.

Kwa mfugaji Ili kuzuia au kupunguza tabia hii, hakikisha: Banda linasafishwa mara kwa mara, wanapata chakula chenye viwango sahihi vya madini na vitamini pia banda lina nafasi ya kutosha.View attachment 3639462View attachment 3639463View attachment 3639464View attachment 3639465View attachment 3639466View attachment 3639467View attachment 3639468View attachment 3639469View attachment 3639470
Naona leo umeamua kutufukuza maimamu huku ndani.
 
Mshambuliaji Fiston Mayele ametangaza kuondoka Pyramids FC baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitatu.

Katika mtandao wa Instagram ameandika “Kwa pamoja tumeandika historia nzuri, tukishinda mataji, kupitia nyakati za furaha na kuunda kumbukumbu zisizosahaulika. Leo ni wakati wangu wa kuanza changamoto mpya. Naondoka katika klabu hii nikiwa na shukrani nyingi na heshima kubwa.”View attachment 3639449
Vizuri
Ila usije kuanguakia kwenye siasa za mpira za Kariakoo
 
Manii ya nguruwe yanatoka kwa awamu tatu kuu ndani ya hizo dakika:

- Awamu ya Kwanza (Pre-sperm): Majimaji ya wazi yasiyo na mbegu yanayosafisha njia.

- Awamu ya Pili (Sperm-rich): Sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa mbegu za kiume (hii ndio sehemu muhimu zaidi ya utungisho).

- Awamu ya Tatu (Post-sperm/Gel): Majimaji mazito kama jeli au kamasi. Kazi ya jeli hii ni kuziba mlango wa uzazi wa jike (cervix) ili kuzuia mbegu zisimwagike nje baada ya dume kushuka.View attachment 3639459View attachment 3639460
My wetu kazi anaiweza😅
 
Back
Top Bottom