Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kama mamba akipata chakula cha kutosha mfululizo, akiepuka magonjwa na maadui, anaweza kuishi miaka mingi sana!
Screenshot_20260730_193537_InstaPro%20.jpg
Screenshot_20260730_193712_InstaPro%20.jpg
 
Popo wanaona vizuri tu, lakini hawana uwezo mkubwa wa kuona usiku sawa kama binadamu ukitembea gizani.

Hivyo hutumia huo uwezo wao wa kipekee wa 'echolocation' usiku kwa ajili ya mambo mawili makuu:

1. Kusafiri kwa Usalama: Ili waweze kupaa kwa kasi bila kugonga miti, kuta za mapango, au vizuizi vingine kwenye giza.

2. Kuwinda Chakula: Ili kugundua na kukamata wadudu wadogo sana ambao wasingeweza kuonekana kwa macho usiku.
Screenshot_20260730_194717_InstaPro%20.jpg
 
Tafiti nyingi, zimeonesha kuwa hofu ya kusimama na kuongea mbele ya hadhara huwa inashika nafasi ya kwanza, ikiiacha hofu ya kifo (Thanatophobia) kwenye nafasi ya pili.

Uzito wa hofu hizi hutegemea sana mtu na mtu, lakini kijamii, hofu ya kuhukumiwa au kuaibika mbele ya wengine ina nguvu kubwa kiasi cha kumfanya binadamu aogope jukwaa kuliko kifo chenyewe.
Screenshot_20260730_194922_InstaPro%20.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Rahma Musa Tito (16), mkazi wa Kijiji cha Msoga, Wilaya ya Chalinze, kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi, Hadija Hemedi Shaha (51), ambaye alikuwa mkulima na mwenye ulemavu wa miguu yote miwili.

Kwa mujibu wa Polisi, tukio hilo lilitokea usiku wa Julai 28, 2026, majira ya saa 5:00, baada ya marehemu kumzuia binti yake kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya rafiki yake iliyokuwa ikifanyika karibu na Hospitali ya Msoga, iInadaiwa kuwa Mtuhumiwa alianza kumshambulia mama yake kabla ya kumchoma kichwani kwa kutumia kitu chenye ncha kali.

Aidha, asubuhi ya Julai 29, 2026, Fundi ujenzi aliyekuwa akidai malipo na kufuata mfuko wa saruji alifika Nyumbani kwa marehemu, baada ya kugonga mlango, alifunguliwa na Rahma Musa Tito, ndipo alipobaini mwili wa Hadija Hemedi Shaha ukiwa umelala sakafuni na ukiwa na majeraha kichwani yaliyokuwa yakivuja damu.

Jeshi la Polisi limesema Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano na hatua nyingine za kisheria zinaendelea huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea ili kubaini mazingira yote yaliyosababisha mauaji hayo.View attachment 3640018
Kuzaa si kupata🤨🤨🤨
 
Back
Top Bottom