Makapuku Forum

Makapuku Forum

Sehemu ya 1

Hapa duniani ni vitu viwili tu vinaweza kukuuwa hata leo. Ukiendekeza mapenzi na pesa utakufa hata leo mchana. El Mencho alikuwa anaogopwa na kila mtu katika nchi ya Mexico, sio kuku tu wa nchi hiyo hata Marais wa nchi hiyo walimwogopa El Mencho. El Mencho alikuwa akisema simtaki huyu utaondoka ama utakufa ukiwa mbishi. Chaguo lilikuwa lako ufuate matakwa ya El Mencho uishi kwa amani ama ukatae ubaki kilema ama ufe. Na ubabe wote huo lakini udhaifu wake mkubwa ulikuwa wanawake. Ulikuwa ukiweka dili la pesa na mwanamke, El Mencho atachagua mwanamke kwanza. Kumbe ndio ilikuwa njia yake ya maangamizi.

Majina yake kabisa yanayojulikana kwenye nyaraka rasmi ni Nemesio Oseguera Cervantes. El Mencho lilikuwa jina la utafutaji. Alizaliwa mwaka 1966 katika mji wa Aguililla ulioko jimbo la MichoacƔn huko Mexico. Makuzi yake hayakuwa tofauti na makuzi ya watoto wengine. El Mencho alipelekwa shule. Alipofika darasa la 5 alikataa shule. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa matatizo. Baada ya kuacha shule akaanza kazi za mashambani. Akiwa na umri wa miaka 14 akawa analinda mashamba ya bangi. Maskini, El Mencho ndio alikuwa toto tundu tayari.

Miaka ya 1980 El Mencho alizamia na kuingia Marekani kwa njia za panya. Huko alianza kuingiza madawa ya kulevya katika Jiji la California. Matukio haya yalifanya awakwe kwenye radar za mamlaka ya nchi hiyo. Alifanya matukio kadhaa ya uhalifu na wakati mwingine mamlaka kumrudisha nchini kwao. Mwaka 1992 alikamatwa tena na madawa ya kulevya akafungwa kifungo cha miaka 5 jela. Alikaa gerezani miaka 3. Hapo El Mencho alikuwa na umri wa miaka 30.

Baada ya kutoka gerezani alirudi kwao Mexico. Huko akawa askari polisi. Kumpa kazi ya upolisi mtu kama El Mencho ni sawa na kumpa shamba la mahindi ng'ombe akulindie. Inawezekana hata mabua usiyaone. Baada ya muda aliacha kazi ya upolisi, kisha akajiunga na genge la wauza madawa ya kulevya la Milenio Cartel. Ili viongozi wakuu wa genge hilo wamwamini, El Mencho aliamua kumwoa ndugu yao Rosalinda GonzƔlez Valencia. Kuanzia hapo El Mencho akawa hashikiki tena..!

Sehemu ya 2 Post inayofuata..!
Screenshot_20260224_204215_TikTok.jpg
 
Sehemu ya 2

Akiwa katika genge la Milenio kazi kubwa ya El Mencho ilikuwa ni kumlinda kiongozi wa genge hilo Armando Valencia Cornelio. Mwaka 2003 mapigano makali yakazuka kati ya Genge la kina El Mencho na genge lingine hasimu. Mapigano yalikuwa makali sana. El Mencho na wakwe zake wakakimbilia Jalisco kutoka MichoacƔn. Huko wakajijenga na kuimalisha utawala wao.

Mwaka 2009, El Mencho akaamua kuanzisha Genge lake mwenyewe. Genge hilo likaitwa Genge la Kizazi Kipya la Jalisco (The Jalisco New Generation Cartel). Hatimaye Genge hili likayapiku magenge mengine ya kihalifu na kuwa top top. Kazi za genge hili zikawa ni pamoja na uuzaji wa madawa ya kulevya, ulanguzi wa silaha, utakatishaji wa fedha, uhalifu mtandaoni na matukio mengine ya uhalifu.

Wakati genge la El Mencho linakuwa vivyo hivyo jitihada za Marekani zikawa juu, kama isingelikuw Marekani pengine El Mencho leo hii angelikuwa hai. Marekani inamtuhumu El Mencho kuwa anaingiza madawa ya kulevya hasa Fentanyl katika nchi hiyo. Kwa sasa dawa hizo zinaua karibu watu laki 1 kila mwaka huko Marekani. Marekani ikatangaza dau la fedha zaidi ya Shilingi bilioni 40 zitatolewa kwa mtu atakayefanikisha kukamatwa kwa El Mencho.

Ikaja tarehe 20 Februari mwaka huu. Mapenzi yakamponza El Mencho. Vikosi vya kijajusi vya Marekani na Mexico vilikuwa vinamfuatilia kwa karibu 'shoga' au tuseme 'BFF' wa mwanamke aliyekuwa mpenzi wa El Mencho. Siku hiyo BFF akamsindikiza mwanamke huyo kwenda kwa Bwana ake. Bwana ni nani sasa. Ni El Mencho. Maskini, kumbe za mwizi huwa ni 40.

Baada ya kumaliza haja zao. Wakaondoka. El Mencho akabaki

Kumbe yeye ndio kapelekewa moto. Marekani ikawahakishikia Mexico kwamba El Mencho alikuwa kwenye nyumba hiyo lakini alikuwa na ulinzi mkali sana. Alikuwa na jeshi zima. Amri ikatoka kwa Rais wa Mexico. Mashambulizi yakaanza.

Watu 70 wakapoteza maisha. El Mencho akakamatwa lakini alikua amejeruhiwa vibaya sana. Akapandishwa helikopta ya Jeshi kupelekwa hospitali. El Mencho akafia njiani. Utamu ukamponza. El Mencho amefariki akiwa na umri wa miaka 59.!
Screenshot_20260224_204215_TikTok.jpg
 
Sehemu ya 2

Akiwa katika genge la Milenio kazi kubwa ya El Mencho ilikuwa ni kumlinda kiongozi wa genge hilo Armando Valencia Cornelio. Mwaka 2003 mapigano makali yakazuka kati ya Genge la kina El Mencho na genge lingine hasimu. Mapigano yalikuwa makali sana. El Mencho na wakwe zake wakakimbilia Jalisco kutoka MichoacƔn. Huko wakajijenga na kuimalisha utawala wao.

Mwaka 2009, El Mencho akaamua kuanzisha Genge lake mwenyewe. Genge hilo likaitwa Genge la Kizazi Kipya la Jalisco (The Jalisco New Generation Cartel). Hatimaye Genge hili likayapiku magenge mengine ya kihalifu na kuwa top top. Kazi za genge hili zikawa ni pamoja na uuzaji wa madawa ya kulevya, ulanguzi wa silaha, utakatishaji wa fedha, uhalifu mtandaoni na matukio mengine ya uhalifu.

Wakati genge la El Mencho linakuwa vivyo hivyo jitihada za Marekani zikawa juu, kama isingelikuw Marekani pengine El Mencho leo hii angelikuwa hai. Marekani inamtuhumu El Mencho kuwa anaingiza madawa ya kulevya hasa Fentanyl katika nchi hiyo. Kwa sasa dawa hizo zinaua karibu watu laki 1 kila mwaka huko Marekani. Marekani ikatangaza dau la fedha zaidi ya Shilingi bilioni 40 zitatolewa kwa mtu atakayefanikisha kukamatwa kwa El Mencho.

Ikaja tarehe 20 Februari mwaka huu. Mapenzi yakamponza El Mencho. Vikosi vya kijajusi vya Marekani na Mexico vilikuwa vinamfuatilia kwa karibu 'shoga' au tuseme 'BFF' wa mwanamke aliyekuwa mpenzi wa El Mencho. Siku hiyo BFF akamsindikiza mwanamke huyo kwenda kwa Bwana ake. Bwana ni nani sasa. Ni El Mencho. Maskini, kumbe za mwizi huwa ni 40.

Baada ya kumaliza haja zao. Wakaondoka. El Mencho akabaki

Kumbe yeye ndio kapelekewa moto. Marekani ikawahakishikia Mexico kwamba El Mencho alikuwa kwenye nyumba hiyo lakini alikuwa na ulinzi mkali sana. Alikuwa na jeshi zima. Amri ikatoka kwa Rais wa Mexico. Mashambulizi yakaanza.

Watu 70 wakapoteza maisha. El Mencho akakamatwa lakini alikua amejeruhiwa vibaya sana. Akapandishwa helikopta ya Jeshi kupelekwa hospitali. El Mencho akafia njiani. Utamu ukamponza. El Mencho amefariki akiwa na umri wa miaka 59.!View attachment 3548193
Wakuu Vincenzo Jr na dosho12 hakuna movie ya huyu mwamba huko tuicheki kama ya chapo na escobar?
 
Asante sana Shunie kwa kuileta humu hii habari. Kilichofanyika inadhaniwa kinaweza kuathiri kombe la dunia kuchezwa Mexico. Tusubiri
 
Tangu utoto wake,

El Mencho alikuwa kijana mtata sana

Yaani ni Gusa UNATE, ukiingia kichwa-kichwa unakula nakozi ya kidevu na kupata aibu.

Kitambo hicho, akiwa na miaka 19 tu, alishawahi kuingia jela pale San Franscico, Marekani.

Ni baada ya kumpiga mtu roba ya mbao na kumuibia mazaga yake, siyo poa SWAHIBA.

Alivyoachiwa na kurudi Mexico, El Mencho aliingia kwenye mishe za Upolisi. Huwezi kuamini MTU Wangu,

Jamaa alikuwa POTI mtiifu mwenye mapenzi na kazi yake kwa miaka nenda rudi.

Ile kufumba na kufumbua, baada ya kusoma ramani juu ya namna polisi wanavyofanya operesheni zao za kila siku,

El Mencho akapiga chini kazi ya Upolisi, kisha akaingia mtaa na kuanzisha Genge lake la kuuza madawa ya kulevya.

Genge lake la Jalisco New Generation Cartel (CJNG) lilikuwa fasta kinoma na kupata umaarufu nchini Mexico.

Mbaya zaidi, jamaa alifanikiwa kutengeneza mtandao mpana na wenye nguvu zaidi wa kuuza NGADA kimataifa.

Hapo sasa akauteka utawala wa mishe zote za madawa kwa kupata mawakala kibao nchini Marekani.

Alipiga sana pesa kiasi ambacho Marais kadhaa wa Marekani,

Waliweka mezani dau nono la Dola Milioni 15 (Bilioni 36) kwa mtu yeyote atakayesaidia kukamatwa kwake

Hawakutoboa, jamaa alikuwa MAFIA kupita maelezo.

Kwenye tovuti zao za kijasusi, walimtaja El Mencho kama Gaidi Tishio Duniani ā€œThe Most Wanted Personā€

Kinachofurahisha na kushangaza,

Ni vile ambavyo Genge lake lilivyokuwa likisifika zaidi kwa mbinu zake hatari zilizofanana na mifumo ya jeshi la Serikali.

Kwa kifupi, jamaa alikuwa na utawala wake ndani ya nchi ya Mexico. Jeshi lake lilikuwa na uwezo wa ku—BATO na jeshi la serikali bila ya kupata tabu yoyote.

kama unataka kujionea venye wahuni wanaishi na kutekeleza majukumu yao ya kila siku, jichanganye kudondoka hapo Mexico.

Picha linaanza, kila nyumba ina mhuni; Siyo Baba, Mama wala mtoto, kila mmoja anamiliki chuma cha moto.

Hilo Poda linauzwa kama maji ya kandoro huku ndoto ya madogo wengi ni kuwa ā€œMaGoDiFAZA wa Kuuza NGADAā€ kama El Chapo au El Mencho.
 
Hao siyo wanajeshi wa jeshi la Serikali ya Mexico,

Hao ni wanajeshi wa Genge la ā€œEl Menchoā€ liitwalo Jalisco New Generation Cartel (CJNG)

Baada ya kuuawa kwa Bosi wao, jamaa wametangaza vita na serikali yao. Wamejiapiza kuichafua nchi na kuifanya ikose amani mpaka pale watakaporidhika wao.

Sema hawa wahuni wa ā€œEl Menchoā€ ni hatari sana

Jamaa wana kila aina ya silaha— Vifaru, RPG, Makombora ya Masafa Mafupi, Silaha za Kivita mpaka Drone za Kivita

Ukitazama hapo ni kama vile Wanajeshi wa Urusi waliopo kule Ukraine kumbe ni Wahuni wa El Mencho wanaopambana na jeshi la Mexico.

Huko Mexico kuna wahuni wameshindikana kiasi ambacho mpaka serikali inafyata mkia.

Screenshot_20260225_063818_InstaPro%20.jpg
 
Kibongo—bongo kuna mitaa ukipita,

Ni lazima utembee kikomando huku ukizungusha kichwa kila upande kwa ajili ya kukabiliana na lolote.

Mitaa ya Tandale, Mburahati, Buza na M/Nyamala ndani ndani huko, ukitembea kiboya, wahuni wanapita na wewe.

Unadhani hapo ndo umekutana na Wahuni MTU Wangu?

Bado hujaona ila kama unataka kuona zaidi, basi jichanganye kudondoka hapo nchini Mexico.

Picha linaanza rolimodo wao ni ā€œEl Chapoā€ — The Drug Lord aliyeiheshimisha mitaa na kupata tuzo nyingi zenye thamani isiyo na mfano.

Ni kama vile madogo wa hapa Bongo wanavyotaka kufanikiwa kama Mondi au Kiba kupitia mishe za muziki,

Ndivyo ambavyo madogo wa Mexico wanavyotaka kufanikiwa kupitia mishe za madawa ya kulevya.

ukifika hapo Mexico; Madawa ya kulevya yanapewa thamani kama madini yanavyogombaniwa pale Geita.

Mbaya zaidi ni vile ambavyo kila nyumba inahusika na mishe za kusambaza NGADA. Siyo Baba, Mama wala Mtoto, kila mtu amevurugwa na ni mhuni wa kuogopwa.

Ukijichanganya tu na kuingia kwenye mifumo yao, wanakupasua kichwa kwa maana kila mhuni anamiliki chuma cha moto.

Sijui unanielewa? Achana na wahuni wa bongo wanaotembea na BisiBisi na Visu vya Mchongo,

Kisha jua likizama wanaenda kwa mama zao kutafuna dona.

Wahuni wa Mexico ni hatari siyo poa

Huyo MHUNI hapo juu anaitwa Nemesio RubĆ©n Oseguera Cervantes, maarufu kama ā€œEl Menchoā€ā€”Chapo wa Kisasa.

Ndo ā€œSTAR Boiā€ mwenyewe ambaye ameuawa na wanajeshi wa Mexico kutokana na mishe zake za madawa ya kulevya.

Unaambiwa enzi za uhai wake,

Mwamba alifanikiwa sana kuwashawishi madogo kuingia kwenye Genge lake la Jalisco New Generation Cartel (CJNG) kwa kuwapa pesa ndefu zaidi ya mishahara ya serikalini.

Yaani ilifika hatua, madogo kibao walikuwa na ndoto ya kujiunga na genge lake kuliko kwenda kuwa wanajeshi wa serikali.

Aiseee, huyu jamaa alikuwa mnoma siyo poa

Licha ya kutokea kwa machafuko mengi haswa kipindi kile alichokamatwa mtoto wa El Chapo, Ovidio De Guzman lakini

Raia wengi wa Mexico wamekiri kwamba huu mziki unaoendelea kwasasa ni moto wa kuotea mbali.

Wahuni wamevurugwa, Mexico imechafuka
Screenshot_20260225_064257_InstaPro%20.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom