Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230808_053500_Instagram.jpg
 
Kukamilika kwa Mfumo wa Makasha (kontena) yanayotumia umeme kwa ajili ya kuhifadhi bidhaa ambazo zinaweza kuharibika kutokana na joto kumeelezwa kuwa kutawasaidia Wakulima na Wafanyabiashara mbalimbali wanaotaka kusafirisha bidhaa hizo kwenda nje ya Nchi kupitia Bandari ya Tanga, Kusafirisha bidhaa hizo bila kuharibika/kuoza.

Afisa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Bandari ya Tanga Habiba Godigodi amesema hayo wakati wa Maonesho ya Wakulima Nanenane Kanda ya Mashariki Mjini Morogoro ambapo amesema Bandari hiyo imeamua kuja na ubunifu wa mifumo ya kontena hizo ambazo kwa sasa ipo mifumo inayoruhusu kontena 50, hivyo hata mzigo ukikaa siku nyingi bidhaa haziharibiki.

Habiba amesema kuwa kulikuwa na changamoto kwa Wakulima wanaosafirisha bidhaa kama matunda, nyama, maua na nyingine zinazoharibika kushindwa kusafirisha bidhaa hizo kutokana na kutokuwepo kwa njia sahihi ya kuhifadhi bidhaa hizo hivyo Bandari ya Tanga imetengeneza eneo maalum la kuhifadhia kontena zenye mfumo wa umeme ili waweza kuhifadhi wakati wanapotaka kusafirisha bidhaa hizo.

Moja ya kati ya changamoto ambazo Wakulima na Wafanyabiashara hukutana nazo wanaposafirisha bidhaa zao kama matunda, vyakula , maua n.k ni kuharibika/kuoza pale zinapokaa kwenye kontena, hivyo kontena hizo za umeme zitasaidia kuondokana na changamoto hiyo.
Screenshot_20230808_053735_Instagram.jpg
 
Jeshi la Niger limelifunga anga na kuyatuhumu Mataifa ya kigeni kujiandaa kwa mashambulizi wakati huu ambapo utawala wa kijeshi umekaidi muda wa mwisho wa kumrejesha Rais aliyeondolewa madarakani, Mohammed Bazoum.

Jeshi hilo limeonya kuwa yeyote atakayejaribu kuitumia anga hiyo atakabiliwa na majibu ya haraka na ya nguvu.

Msemaji wa Viongozi wa kijeshi walioshiriki mapinduzi hayo, Amadou Abdramane, ameonya kuwa kuna kitisho cha uvamizi kinaandaliwa kutoka katika Taifa jirani na kuongeza kuwa anga ya Taifa hilo itafungwa hadi pale taarifa nyingine itakapotolewa.

Jana usiku (Agosti 6), Televisheni ya Taifa ya Niger ilitoa tangazo hilo ikiwa zimesalia saa kadhaa kabla ya muda wa mwisho uliwekwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ambayo inawashinikiza vinara wa mapinduzi kumrejesha madarakani Rais Bazoum au vinginevyo wakabiliwe na nguvu za kijeshi.

Viongozi wa kijeshi wanahisi Mataifa mawili ya Afrika ya Magharibi yanajiandaa na uvamizi ingawa hawajayataja lakini pia katika taarifa hiyo wamewataka Raia wa Niger kulilinda Taifa lao.
Screenshot_20230808_053858_Instagram.jpg
 
Askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) kutoka Pori la Akina Mpanga, Kipengere kwa kushirikiana na Askari kutoka Hifadhi ya Taifa Ruaha na Vyombo vingine wamefanikiwa kuwadhibiti kisha kuwaua Simba wawili (Dume) waliokuwa wakizua taharuki kwa kujeruhi na kuua mifugo katika maeneo mbalimbali ya Mikoa ya Njombe na Iringa.

Mkuu wa Hifadhi ya Mpanga Kipengere Donasian Makoi amesema wamefanikiwa kuwaua Simba hao katika Kitongoji cha Lole kilichopo Kijiji cha Makungu Wilayani Mufindi ikiwa zimepita siku kadhaa tangu walipotoroka Hifadhini July 21,2023 na kusababisha hasara kwa kushambulia ng'ombe 14 na nguruwe watano katika maeneo mbalimbali ya Wilaya za Wanging'ombe, Njombe na Mufindi.

"Tumefanikiwa kuwaua lakini pia kwa kushirikiana na Maafisa Maliasili wa Wilaya hizo zote tulikubaliana kuchukua taarifa za wale Wahanga wote walioliwa mifugo yao ili Serikali iweze kuwalipa kifuta machozi"

Makoi ametoa wito kwa Wananchi kuendelea na shughuli za uzalishaji mali ili kukuza uchumi wao kwa kuwa tayari Simba hao wamekwishadhibitiwa huku pia akiwaomba waendelee kutoa taarifa pindi wanapotokea wanyama waharibifu kwenye makazi yao.
Screenshot_20230808_054149_Instagram.jpg
 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu Abdallah Shaib akiwa na Watu wengine leo wamefika nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita na kuzuru kaburi lake.

Kabla ya kuzuru kaburi la JPM, Mwenge huo ukiwa Wilayani Chato umekagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi 7 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 13.

Mwenge pia umezunguka katika Wilaya tano na Halmashauri sita ndani ya Mkoa wa Geita ambapo umepitia miradi 59 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 29 na kutembea umbali wa kilometa 770 .

Mbunge wa Jimbo la Chato Mhandisi Medard Kalemani pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Chato Deusdedith Katwale wamemshukuru Kiongozi wa Mbio za Mwenge huku wakimuomba kufikisha salamu za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka miradi pamoja na fedha ndani ya Wilaya hiyo.
Screenshot_20230808_054629_Instagram.jpg
 
Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Dkt. Benson Bana amethibitisha kuwa Watu wasiojulikana nchini Nigeria wamemteka nyara Mtanzania ambaye ni Frateri wa Shirika la Wamisionari wa Afrika (White Fathers), Melkiori Mahinini (27) ambaye ni Mzaliwa wa Parokia ya Kabanga Jimbo la Kigoma.

Mtanzania huyo alikamatwa katika Jimbo la Minna nchini Nigeria, August 03,2023 akiwa na mwenzake Raia wa Burkina Faso, Padri Paul Sanogo ambapo Watekaji wamedai Naira mil 100 (Tsh. mil 314.4) ili wawaachie huru wote wawili.

Akiongea na @AyoTV_ Dkt. Bana amesema “Tukio la kutekwa ni kweli limetokea tangu Aug 03 mwaka huu, sisi tunaokaa huku hatushangai ni uhalifu ambao sio Mgeni umeshazoeleka hapa Nigeria Watu kutekwa Nyara kisha Ndugu zao wanadaiwa kikombozi (pesa), wakishamteka Mtu wanatangaza wanataka kiasi fulani, na hawa walipowateka hawa walitangaza wanataka Naira mil 100 (Tsh. mil 314.4)

“Kwa kawaida wanateka sababu ya fedha, Ndugu yenu akitekwa mnajikusanya kuona mtaanzaje mazungumzo nao, watakuwa na Mawakala wao wanaoweza kuzungumza kisha Watu wanakombolewa, Kijana wetu huyu Shirika lake la Dini linaeleweka, sisi kama Ubalozi dhamana yetu ni kulifuatilia kwa ukaribu”

“Maisha ya Mtanzania popote alipo katika eneo letu la uwakilishi ni kipaumbele chetu namba moja, kwahiyo tunafuatilia kuona Vijana hawa wanakombolewa, visa vya Watu kukamatwa kuuawa vipo vingi Nigeria, Watekaji mara nyingi wanataka pesa na mkichelewesha wanaweza kuwadhuru ili kuwaonesha wapo serious”
Screenshot_20230808_054734_Instagram.jpg
 
Serikali ya Ufaransa imetangaza kusitisha msaada wa fedha kwa ajili ya maendeleo na msaada wa fedha za bajeti kwa Taifa la Burkina Faso mara baada ya Nchi hiyo kutangaza kuunga mkono Mapinduzi yaliyofanyika nchini Niger.

AFP wameripoti kuwa uamuzi wa Ufaransa unakuja baada ya Burkina Faso na Mali kutangaza kuwa zinaunga mkono kitendo cha Wanajeshi kumpindua Rais wa Niger huku zikisema endapo ECOWAS itaivamia Niger ili kumrudisha Rais madarakani basi na wao watatangaza vita na ECOWAS na watapigana kuisaidia Niger.

Msaada wa Ufaransa kwenye maendeleo ya Burkina Faso unakadiriwa kuwa ni USD mil 530 na msaada wa Ufaransa kwenye bajeti ya Burkina Faso kwa mwaka jana ulikuwa ni Euro mil 13.
Screenshot_20230808_054844_Instagram.jpg
 
Mtu mmoja amelazwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizito wilayani Mikumi na wengine wametibiwa na kuruhusiwa baada ya basi la kampuni ya New Force walilokuwa wakisafiria kutoka Kyela kwenda Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Agosti 7, 2023 jioni eneo la Msimba kwenye mteremko na kona za Iyovi Mikumi ambapo amemtaja majeruhi kuwa ni Elinipenda Kishimbo (26) aliyeteguka mkono.

Kamanda Mkama amemtaja dereva wa basi hilo kuwa ni George Obedi (48) huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa ni uzembe wa dereva huyo kwa kuwa alitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila ya kuchukua tahadhari na hivyo kukutaka na gari jingine uso kwa uso.

"Huyu dereva bila kujali kuwa eneo lile ni hatari alilipita gari lililopo mbele na kabla hajalipita likatokea gari jingine mbele alichoamua ni kwenda kulia zaidi mwa barabara na hivyo alishindwa kulimudu basi hilo hasa ukizingatia alikuwa kwenye mteremko mkali," amesema Kamanda Mkama.

Hata hivyo amesema kuwa tayari dereva huyo anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi huku na uchunguzi utakapokamilika taratibu za kumfikisha mahakamani zitafuata.
Screenshot_20230808_055214_Instagram.jpg
 
Inafahamika kuwa kwa sasa suala la usajili kwa kutumia alama ya kidole imekuwa kawaida sana na ili uweze kupata baadhi ya huduma basi inakubidi uweke alama ya kidole (Finger Print) na hii sio Tanzania tu bali hadi katika Mataifa mengine.

Inatajwa kuwa kila mtu huwa na alama za vidole ambazo ni tofauti na mwingine hata kama akiwa mzazi na mwanaye bado alama hizo haziwezi kufanana, watu hutumia alama ya kidole kupata vitambulisho , ‘kadi’ za simu na hata kutumia kama njia ya usalama wa kulinda vifaa vyao kama vile simu.

Lakini jambo hilo limekuwa tofauti kwa familia ya Apu Sarker iliyopo Bangladesh ambayo wanafamilia wamezaliwa bila kuwa na alama za vidole jambo linalosababisha wapate tabu kupata baadi ya huduma ikiwemo ‘kadi’ za simu, kitambulisho cha taifa na huduma nyingine.
Screenshot_20230808_055326_Instagram.jpg
 
#PICHA: Miili ya Ndugu watatu wa Familia moja ambao walifariki usiku wa kuamkia August 03,2023 baada ya gari (Toyota Prado) walilokuwa wamepanda wakitokea Dar es salaam kwenda Same, Kilimanjaro kugongana uso kwa uso na Scania lililokuwa linatokea Arusha kwenda Dar es salaam, imeagwa leo Lugalo Golf Course, Dar es salaam kabla ya kwenda kuzikwa katika makaburi ya Kondo Tegeta.

Miili ya Watoto hao wa Mr. Hashim Msuya na Mkewe inayoagwa leo ni wa Siah Hashimu Msuya (53), Diana Sukulu Mageta (47) na Dkt. Norah Msuya Mumburi (45), mwili wa Kaka yao (Dereva wa Prado) ambaye walipata nae ajali hiyo, Neech Hashim Msuya ambaye alikuwa Mfanyakazi wa Benki ya ABSA tayari umeshazikwa Jumapili katika Kijiji cha Msangeni Ugweno Wilayani Mwanga, Kilimanjaro.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila pamoja na Viongozi wengine wameungana na waombolezaji wengine kuaga miili hiyo.
#MillardAyoUPDATES
#RIPNduguZetu
Screenshot_20230808_190149_Instagram.jpg
Screenshot_20230808_190217_Instagram.jpg
 
Rais Samia ameagiza Mzee Hashimu Msuya na Mke wake ambao ni Wazazi wa Watoto wanne waliofariki usiku wa kuamkia August 03,2023 baada ya gari lao (Prado) kugongana uso kwa uso na Lori Mkoani Pwani, watibiwe kwa hadhi maalum (VIP Treatment) kwenye Hospitali za Muhimbili, JKCI na wasisumbuliwe kimatibabu kwenye Hospitali yoyote nchini.

Akiongea leo wakati wa Ibada ya kuuga miili ya Watoto watatu, RC wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema “"Mh.Rais wakati ananituma hapa alisema nimesoma kwenye mtandao Watoto wale walikuwa wanawalea Wazazi wao, walikuwa wanawapeleka Hospitali na akaniambia niongee na Prof.Janabi wa pale Muhimbili, niongee na Dkt.Kisenge wa JKCI kwamba Wazazi hawa wapate VIP treatment watakapokwenda Hospitali pale"

"Na jukumu hilo akaniambia waambie na Wakuu wa Mikoa wengine wote mahali popote watakapokuwepo Wazazi hawa wasiwe na mnyororo mpana wa kusumbuka mwisho wataanza kuwakumbuka Watoto wao kama sisi tutaendelea kutokuwa faraja yao"

Miili ya Siah Hashimu Msuya (53), Diana Sukulu Mageta (47) na Dkt. Norah Msuya Mumburi (45), imeagwa leo Dar es salaam na mwili wa Kaka yao (Dereva wa Prado) ambaye walipata nae ajali hiyo, Neech Hashim Msuya ambaye alikuwa Mfanyakazi wa Benki ya ABSA tayari umeshazikwa Jumapili katika Kijiji cha Msangeni Ugweno Wilayani Mwanga, Kilimanjaro.
Screenshot_20230808_192305_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom