Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,081
- 464,013
Dar es Salaam. Unaweza kusema kusema ni moja ya maamuzi magumu ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu Watu (ACHPR) baada ya kutoa hukuma yenye kuitaka Serikali ya Tanzania kutowatumia wakurugenzi wa halmashauri nchini kusimamia chaguzi.
Amri hiyo ya ACHPR inaitaka serikali kufanyia marekesho ya sheria za uchuguzi na kupeleka ripoti ya utekelezaji wa marekebisho hayo ndani ya miezi 12 toka hukumu hiyo kutolewa.
Hukumu hiyo inatokana na kesi iliyofunguliwa Machi 13, 2020 na mwanaharakati Bob Wangwe kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wakipinga wakurugenzi hao kusimamia chaguzi.
Itakumbwa kuwa hii ni mara ya pili kwa wakurugenzi wa halmashauri kupigwa kusimamia uchaguzi japo uamuzi huo ulitenguliwa na Mahakama ya Rufani ya Tanzania.
Mahakama hiyo ya juu nchini iliwaruhusu wakurugenzi hao kuendelea kusimamia chaguzi kwa sababu wanakula viapo vya kukana uanachama wao wa vyama vya siasa kabla ya kusimamia chaguzi.
Mei 24, 2019, Mahakama Kuu ilifuta sheria iliyokuwa inawapa wakurugenzi hao mamlaka ya kuwa wasimamizi wa uchaguzi, lakini Oktoba 17, 2020 Mahakama ya Rufani ikatengua uamuzi huo.
Kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa jana, ACHPR imesema sehemu za vifungu vya 6(1), 7(2) na 7(3) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi vinakiuka Kifungu cha 13(1) cha mkataba unaoanzisha Mahakama hiyo.
Hivyo, imeamuru mlalamikiwa (Jamhuri) kuchukua hatua zote muhimu za kikatiba na kisheria, ndani ya muda muafaka na bila ya ucheleweshaji wowote usiostahili, kuhakikisha yanafanyika marekebisho ili kuondoa ukiukwaji wa ibara ya 13(1) ya mkataba.